Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumapili, 1 Novemba 2015

JINNI KHAADIMUL~HAMMAAM

Jinni huyu ni miongoni mwa majini wa aina mbalimbali wenye kuwadhuru binaadamu.
Jinni huyu makazi yake makubwa  ni kwenye vyoo au mabafu yanavyotumiwa na binaadamu na hata vile ambavyo havitumiwi tena au vimebaki kama magofu,na jinni huyu ndiye chanzo cha balaa nyingi

Mtume Muhammad (s.a.w) alikuwa akijilinda kwa Allah kutokana na jinni mchafu tena wa hatari wakati wa kwenda chooni au bafuni alikuwa akisema hivi “Ewe Allah hakika mimi ninajilinda kwako kutokana na uchafu wa chooni pamoja na wachafu (mashaytwani)”, na wakati wa kutoka Mtume alikuwa akimshkuru Mungu kwa kusema “ Shukrani ni za Allah ambaye kaniondolea maudhi ya(shaytwani) na akanipa afya”, kwani ukipatwa na shaytwani huyu afya yako inaharibika na chooni ndio nyumba za shaytwani na makazi yao, kwa hiyo ziko adabu za kuingia chooni, lazima adabu hizi zizingatiwe na kila mtu ili kuepuka kukumbana na jini huyu 

ADABU ZA KUINGIA CHOONI 
a) Mtu aingie chooni kwa kutanguliza mguu wa kushoto na akitoka atanguliza mguu wa kulia.

b) Mtu asizungumze kwa sauti akiwa chooni ila kwa dharura, na wana wachuoni wakazitaja dharura hizo kuwa ni:

i) Kumtambulisha alie nje ajue kama wewe uko chooni ili nae asiingie humo, hapo itabidi ujikohoze kohoze.

ii) Kumuongoza mtu ambae ni kipofu au kumtahadharisha mtoto mdogo kutokana na jambo la hatari, hapo itakubidi useme tu.

c) Mtu asiimbe au kupiga makelele chooni

d) Mtu asivue nguo zake zote chooni kama hakuna ulazima wa kufanya hivyo ila avue eneo ambalo anataka kujisaidia tu (azipandishe kidogo kiasi cha haja).

e) Mtu akitoka salama chooni amshukuru Mungu kutokana na usalama huo

f) Nasimwage maji chooni wakati wa usiku ila awe kamtaja Mwenyez mungu kwa sauti ya juu akiwa nje mlangoni.

Hizi ni baadhi ya adabu za chooni ambazo adabu hizi mtu akizipuuzia ndipo jinni huyu mchafu hupata urahisi wa kumvamia na urafiki wa madhila ukaanzia hapo.


Khadimul-hammam, majini hawa wako wa aina mbili, kuna aina inayoonekana moja kwa moja chooni na iko aina isiyoonekana, aina inayoonekana hii ni aina ya hatari sana kuliko aina isiyoonekena.

DALILI ZA MTU ALIYEINGIWA NA JINI KHADIMUL-HAMMAAM:

Khadimul-hammaam ana dalili zifuatazo
:

a) Mgonjwa hupenda kuingia chooni na kukaa huko muda mrefu.

b) Baadhi ya wagonjwa hujikuta wanasinzia wakiwa chooni wanajisaidia.

c) Mgonjwa hupenda uchafu sana na kulala bila kuoga.

d) Kupenda Kuingia chooni wakati wa kiza.

e) Mtu kuchukia kusikiliza Qur-an na adhana,na hata nasaha zozote zinazohusu dini

f) Kuonekana nyayo kwenye mwili wa mgonjwa kwa rangi ya kijivu au nyekundu.

g) Maumivu kwenye maungio ya viungo pamoja na kupoza mwili.

Na ndio maana baadhi ya watu humuita jinni huyu kuwa ni subiani wa chooni. Na jinni huyu yuko ambaye humtokezea mtu huko huko chooni wakaonana ana kwa ana, na akimtokezea mgonjwa humfanyia haya yafuatayo:

- Humpiga mgonjwa

- Humtisha mgonjwa

- Huanza kumchezea chezea kama vile mume anavyocheza na mkewe kwa kumshika shika sehemu za siri na kumbusu.

Haya ndio mambo ambayo jinni huyu Khadimul-hammaam anapomtokezea mgonjwa huyafanya.

Baada ya kujua dalili zake, aina yake na vituko vyake, sasa tutaje dawa yake ya kumkomesha kabisa.

NAMNA YA KUMFUKUZA JINI KHADIMUL-HAMMAAM ASIYEONEKANA:

Tiba za kumkuza jinni huyu wa chooni ni kama zifuatazo:

a) Mgonjwa asomewe Suratul Baqarah nzima.

 b) Asomewe Suratul Qalam, sura hii humuunguza jinni huyu.

c) Mgonjwa ajilazimishe usafi wa mwili, nafsi, mavazi na sehemu anayoishi.

d) Mgonjwa lazima ajipake mafuta mazuri pamoja na uturi akiwa nyumbani tu.

e) Mgonjwa lazima ajilazimishe kuingia chooni kwa adabu za chooni.

Hii tiba ni kwa ajili ya jinni wa chooni asiyeonekana,ama jinni wa chooni 

anayeonekana kwa watu tiba yake ni hii ifuatayo:

a) Kusoma dua ya kuingia chooni kwa sauti.

b) Kabla ya kuingia chooni kiashirie choo kwa kidole cha shahada, kisha soma aya hizi kwa nia ya kumfukuza jinni huyu chooni. Na sura za kusoma wakati unaashiria kwa kidole ni hizi zifuatazo:
- Ayatul Kursiyyu mara tatu.

- Suratul Humaza mara saba.

- Suratul Zilzaalah mara tatu.

Na aya hizi uzisome kwa nia ya kumfukuza jinni wa chooni.
Ukifanya hivyo wakati wa kuingia chooni, Ins
haAllah hata kama ulikuwa ukimuona jinni huyo hutamkuta na atakuwa amekimbia