Husda imeenea zaidi kuliko kijicho na kila mwenye kijicho ni hasidi makhsusi kabisaa,kwahiyo kila mwenye kijicho ni hasidi,na sio kila hasidi ni mwenye kijicho.
katika kuran kumetajwa surat lfalaq kujikinga na hasidi,na mwenye kijicho pia ameingia humo.
hii inatokana na ukubwa wa qurani,kuajizisha na ufasaha wake
HUSDA
Husda ni kutamani mtu aondokewe na neema aliyonayo hata kama yule anayetamani vile hapati wala hafaidiki na chochote..yenyewe inatokana na chuki,bughda roho mbaya nk
KIJICHO
Kijicho kinatokana na kuajabia yaani kuona jambo ni kubwa na kupendezwa nalo
Husda na kijicho hushirikiana katika kuathiri kwa namna ileile anavyopata madhara kwa aliyeonewa kijicho au aliyehusudiwa, na ukhitilafiana katika chanzo tu
Chanzo cha husda ni kuchomeka moyo na kuiona neema ni kubwa kwa aliyehusudiwa na kutamani neema hiyo imuondokee.
Chanzo cha kijicho ni mchocheo wa mtazamo wa jicho, kwahivyo huenda likamsibu hata asiyemhusudu katika vitu visivyo na roho au vyenye roho kama vile wanyama,mazao,mali nk,na pengine jicho lake huweza kumsibu hata yeye mwenyewe,kutazama kwake kitu kwa mtazamo wa kuajabia na kukodolea jicho pamoja na nafsi yake kubadilika basi kwa mabadiliko haya ndiyo humuathiri aliyeonewa kijicho.
Pia hasidi huweza kulihusudu hata jambo linalotarajiwa kufanyika hata kabla bado halijatokea na kwa upande wa kijicho ni kinyume chake kwani hawezi kulionea kijicho jambo lisilokuwepo.
Mtu hawezi kuihusudu nafsi yake wala mali yake lakini anaweza kuionea kijicho
Hasadi inatokana na mtu khabithi na mwenye chuki,lakini kijicho huenda kikatoka hata kwa mtu mwema kwa sababu anaweza akaajabia jambo bila kupenda liondoke kwa mwenyewe kama ilivyotokea kwa Aamir rabiia alipomsifu Sahli bin Hunaif na akapatwa na kijicho
Muislam anapokiona kitu kilichompendezea,akibarikie yaani akiombee baraka kitu hicho kiwe chake ama cha mwingine
MAJINI WANAWAONEA KIJICHO WANAADAMU
Majini nao ni viumbe ambao hawana tofauti na waanadamu ispokuwa kwa baadhi ya mambo tuu kama vile wao kuwa na uwezo wa kujibadilisha,kuishi miaka mingi nk,hivyo kama ilivyo kwa binadamu pia majini huwaonea binadamu kijicho,kwahivyo yampasa kila mtu ataje jina la mungu anapovua nguo zake,kujitazanma kwenye kioo,au jambo lolote ili ajiondolee madhara ya majini kutokana na kijicho au jambo lolote liwalo