Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumapili, 26 Machi 2017

UKWELI KUHUSU NUKSI NA MIKOSI


Siyo ajabu kusikia mtu fulani hafai kushirikiana nae katika shughuli yeyote kwa vile ana nuksi na ukifanya ubishi ukashirikiana nae mambo yenu hayataendelea vizuri

 Au mwanamke fulani hafai kumuoa ukimuoa tu mambo yako yanaharibika.Siwezi kulipinga jambo hili kwani ni kweli wapo baadhi ya watu huandamwa na mikosi mara kwa mara na wapo wanawake ambao wakiolewa hutokea kama hayo yaliyoelezwa ya kuharibikiwa wanaume wao na ndoa zao na sio mmoja mwingine hufikisha idadi kubwa ya wanaume waliotokezewa na hali hiyo mpaka akaogopwa kuolewa kwa vile huharibikiwa mambo yao hao wanaume    
Maswali yakujiuliza                                                                                                              Ni kweli mwenyezi mungu anaweza kumtia nuksi mja wake?                                                                          Jibu sio kweli bali huwa kama ifuatavyo 

Mtu kama huyo kawaida huvamiwa na shetani wa kijini na endapo shetani huyo amemwingia kwa lengo la kufanya nae mapenzi basi jinsi mashetani walivyo wajinga huanza kujiskia wivu juu ya mwanamke huyo na kuona kama vile yeye ndyo ana mamlaka juu yake,na endapo mwanamke huyo atakuwa na mahusiano na binadam mwenzie basi shetani huyu anaumia sana na huanza kuleta kasoro za kimaumbile au kifikra ili mwanamke aonekane hafai na aweze kuachwa kwenye ndoa hiyo aendelee kufaidi yeye tu jini huyo.hali hii huwatokea hata wanaume pia, na nuksi hizi si kwenye ndoa tu bali shetani huyu atakuharibia kila anapoona pana manufaa na wewe iwe kikazi,kibiashara,n.k ili mradi uone tangu ulipokuwa na mtu fulani mambo yameharibika kabisa hivyo umuone hafai.

pia mashetani yanayotia nuksi na mikosi huweza kutumwa na wachawi kwa mtu yeyote wanayemkusudia amvurugie mipango yake,baada ya shetani huyo kulipwa malipo atakayohitaji kama vile damu.

Hivyo tunatakiwa tujue kwamba hakuna mtu aliyeumbwa na nuksi wala mikosi,wala hakuna mtu ambaye Mungu amemjaalia mikosi na manuksi ili ateseke,HAKUNA.Bali ni kazi ya shetani kuweza kutimiza ushetani wake

mfano wa haya ni kama vile alivyofanyiwa nabii Ayubu na shetani kwa kumuharibia mambo yake katika surat saad 41,basi unatakiwa kujua kama shetani aliweza kuwachezea hata manabii na mitume wa Mungu itakuwaje mimi na wewe?