NYOTA YA PUNDA AU KONDOO (ARIES)
- Hii ni nyota ya kwanza katika mlolongo wa nyota 12.
- Wenye nyota hii ni wale waliozaliwa kati ya tarehe 21st March na tarehe 19 April ya mwaka wowote.
- Sayari yao ni Mars (Mariikh)
- Siku yao ya bahati ni Jumanne
- Namba yao ya bahati ni 9
- Rangi yao ya Bahati ni Nyekundu.
- Asili yao ni Moto.
NYOTA YA PUNDA AU KONDOO KATIKA MAPENZI NA MAHABA
Kwa vile wao ni wenye nyota ya kwanza mara nyingi wenye nyota hii wanapenda kuwa mbele. Wanakuwa wakarimu na wenye pendo kwa wapenzi wao.
Ni watu wenye kupenda kushirikiana na watu wengine, wanapenda mikusanyiko ya jamii
na wacheshi. Ni watu wazuri kuwa nao karibu na mara nyingi wao wanakuwa ndio maisha na roho ya kundi wanalojihusisha nalo. Hivyo inatokana na tabia zao za asili za uchangamfu. Hata hivyo wakiudhiwa huwa ni viumbe wenye hasira kali.
Wenye nyota hii ni wepesi sana kuvunjika moyo na hii inatokea wakati wapenzi wao wanapowaangusha au kuwadharau katika mapenzi ambayo wao wanayachukulia kwa uzito mkubwa.
Pamoja na uchangamfu walio nao wenye nyota ya Punda wana moyo dhaifu usiovumilia matatizo na wanaweza kudhuriwa kirahisi katika mapenzi.
Wanaingia katika mapenzi na kupenda kirahisi. Mara nyingi wanawafanya wapenzi wao
ndio nguzo au kiegemezo na hapo ndipo matatizo yanapoanza.
Wasipopata njia ya kutatua matatizo ya kimapenzi huwa wanachanganyikiwa na wanafadhaika sana hasa wanapogundua kwamba wapenzi wao ni binadamu kinyume na walivyofikira wao.
Kwao wazo la kuwa waaminifu kwa mpenzi mmoja milele linapewa kipaumbele katika mambo ya mahaba, lakini wakiona mambo yanaenda kombo basi ni mwepesi sana kuondoka kwenda kutatufa mpenzi mpya sehemu nyingineyo.
Kwa ujumla wenye nyota ya Punda ni watu wenye mapenzi motomoto, tatizo lao kuwa hawapendi kusikiliza ushauri wa kimapenzi, na hawakubaliani na mambo nusu nusu. Ni watu wenye kutegemea mazuri wakati wote na hawakubali kushindwa. Hupenda kukimbilia
katika mapenzi bila kufikiri wanapohisi wamepata mpenzi wa kweli. Ni wepesi kuvutwa katika mapenzi na ni wenye miamko ya ghafla au misukumo ya kiwazimu ambayo wakati mwingine inawafanya waonekane wapumbavu.
NYOTA YA PUNDA KATIKA FEDHA
Wenye nyota hii wanapenda sana kutumia nguvu au kulazimisha na siyo waoga. Mipango yao ya kifedha wanayoipanga inakuwa na ubora wa hali ya juu inayopendeza na inayowavutia watu wengine. Hii inatokana na uwezo wao, shauku na vipaji vya kiakili kuhusiana na masuala ya fedha.
Hakuna sehemu yeyote ambayo mwenye nyota ya Punda atafanya shughuli yeyote bila watu kupendezwa na mipango yao. muda wote wako tayari kuchukua majukumu bila kujali chochote na mwisho wake mafaniko yanakuwa makubwa. Suala la kujiliza ni kuwa je
wanaweza kufanya hivyo kwa muda mrefu?
Jibu ni hapana watu wa Punda wanatambulika kwa tabia yao ya ufuatiliaji wa mambo, bila kuchoka lakini tabia yao ya kiburi katika mambo madogo madogo ya kibiashara na kikazi wakati mwingine huhatarisha mradi au kazi zao zote.
Wanapenda kutumia fedha kiholela bila kupata uhakika kwamba zitarudi au zipo. Hulka yao ya kuwa mbele na kupenda kuishi kiuaminifu huwafanya wakose kinga kwa wajanja wanao penda kuwatapeli.
Kitu kimoja ni kwamba Mungu amewapa uwezo wa kufanya kazi vizuri wanapokuwa wao viongozi au wasimamizi. Wanakuwa na nia na moyo wa kufanya mambo mapya, lakini ajabu ni kwamba hawana subira wala mbinu za utawala hasa katika masuala ya fedha.
Papara zao za kujua mambo zaidi mara nyingi husababisha utatanishi kwa watu wote wanaowazunguka na wanao wakilisha.
Kimaisha wenye nyota ya Punda wanapenda sifa na kuonyesha matunda ya kazi zao au uwezo wao kifedha kwa kununua magari mazuri, nguo zenye thamani kubwa na vito vya thamani ili waonekane pamoja na ukarimu wao wakati mwingine hubadilika na kuwa wabinafsi na wachoyo.
Kwa ujumla wenye nyota hii ni watu wenye ari na uwezo wa kuanzisha mambo na wanapenda kupata maendeleo ya kimaisha na kuwa na miradi mipya. NATAKA ndio neno lao kubwa. Wanahitaji sana fedha, uwezo na uvutio ni wakati mchache sana huangalia maslahi ya watu wengine. Huwa wanakabiliwa na tatizo la kuchagua fedha au mamlaka, hata hivyo mapenzi yao ya kuwa na uwezo huwa yanashinda.
{mospagebreak}
NYOTA YA PUNDA (AFYA ZAO)
Wenye nyota hii ni watu wenye nguvu na afya nzuri. Wakati wote wao wanakuwa hawana subira ya kungoja kufanya shughuli zinazowahusu. Ni watu ambao hawapendi kabisa kuugua au kupata maradhi. Mara nyingi wanakuwa na uwezo wa ajabu wa kupona maradhi yanyaosumbua.
Kwa vile nyota hii ya Punda inatwala kichwa maradhi yao mengi yanahusiana na kuumwa kichwa na homa za mara kwa mara ambazo hupotea kama zilivyokuja.
Tatizo lao kubwa la kiafya ni la Adrenalini (Hii ni Homoni inayotoka ndani ya mwili wakati mtu anaposhtushwa au kukasirika, ambayo inafanya moyo upige haraka na kuutayarisha mwili kupambana na khatari). Watu hawa wanafanya kazi bila kuchoka na inatakiwa nguvu zao zielekezwe sehemu inayohusika, ikitokea vinginevyo huwa wanakosa raha na kuwa na wasiwasi.
Wasiwasi huo unasababisha Adrenalini kumwagika kwa wingi wanakuwa wepesi kuudhika na kukasirishwa na kuwa na Hamaki au ghadhabu za haraka ambazo huwaletea matatizo ya mzunguko wa damu katika Ubongo na macho.
Watu wa Punda wanahitaji kufahamu kwamba wao hawana kinga hivyo mapumziko ni muhimu kwao. Wanatakiwa wapendelee kutembea kwa miguu au wajihusishe na michezo ili kuondoa mzigo wa uchokozi, hakami na hasira walionao.
Utaratibu maalum wa kula chakula vile vile ni muhimu, na wenye nyota hii wanashauriwa
kukiepusha na kahawa na sukari nyeupe ambao inaongeza mfadhaiko katka mfumo wa neva na tezi za Adrenalini. Ni wachache sana wenye nyota hii ambao wana matatizo ya uzito kwa sababu wanajishughuoisha sana na shughuli mbalimabli.
Kwa ujumla wenye nyota hii wanapokata tamaa huwa wanaathirika, na tbaia yao ya haraka haraka inawafanya wawe katika vita na miili yao wenyewe. Matokeo yake ni kuathirika kiafya. Wanatakiwa wajifunze tabia ya nyota ya Mizani ya ushirikiano. Tabia hii pamoja na kwamba itawapunguza kasi zoa katika utendaji lakini itawasaidia kudhibiti matatizo yao ya kiafya.
NYOTA YA PUNDA (MAISHA YAO)
Punda wanapenda sana kujihusisha na masuala ya kuwafanya waishi vizuri kama binaadamu wengine. Wanapenda sana vitu vyenye msisimko vya pekee na utaona hivyo katika nyumba zao.
Kuweka makazi ya kudumu kwa mtu wa Punda ni moja ya mitihani mikubwa ambayo ana lazima atekeleze lakini kwa watu wengine jambo hili wanalichukulia kama mojawapo ya mambo mengi ya kimaisha ambayo wakipata fedha anataka watekeleze.
Moja ya hulka za Punda ni kuthibiti namna nyumba zao zinavyoendeshwa. Hivyo inamaanisha kwamba wanahitaji kupata mwenzi mwaminifu ambaye atatekeleza yote atakayoagizwa kuyafanya hapo nyumbani. Vinginevyo tabia zao za kutokupumzika na tamaa ya kufanya mambo mapya itawafanya wapoteze hamu ya maisha yao ya nyumbani.
Wanapokuwa tayari wameweka mizizi yao wanakuwa waaminifu kwa familia zao. Hata hivyo kuna hatari kwamba wasipoweza kupata wanachokitaka hapo nyumbani wanaweza kusimama na kuondoka.
Hawawezi kuficha hisia zao kwa yeyote wanayemualika katika nyumba zao ukikosa atakuambia na hawategemei hata walioalikwa nao kuficha hisia zao vile vile.
Kutokana na shauku na hamu kubwa ya kuthitisha maisha yao, ni vizuri Punda wakawa waangalifu, wasiwe wajeuri au wakandamizaji katika nyumba zao.
Ni watu wanaozipenda familia zao na mara nyingi wanatumia nyumba zao kama sehemu ya kufanyia kazi badala ya mapumziko.
{mospagebreak}
NYOTA YA PUNDA (LIKIZO NA SAFARI)
Nyota ya Punda ni nyota yenye asili ya moto, maana yake ni watu wenye ari na nguvu zisizo na mipaka, na mara nyingi wanatatufa vitu vinavyowafurahisha. Wanapenda sana kusafiri aidha katika biashara au kwa kujifurahisha.
Wenye nyota hii wana tabia ya kujenga uhusiano mkubwa katika tabia fulani. Hii inapotokea wanapenda kutumia muda wao mwingi katika mazingira hayo ili wayaelewe vizuri. Wanajua kabisa sehemu au mji ambao watajisikia wako nyumbani.
Muda mwingi huwa wanapenda mazingira mapya na hii inawafanya kupata uzoefu mkubwa mara nyingi wanakuwa ni waalimu wazuri sana. Ukweli wa mambo ni kwamba walimu wengi wa shule wanaowaongoza wanafunzi katika safari za nje ni wenye nyota ya Punda.
Punda ni wasafiri majasiri na wanapenda vyombo vinavyokwenda kasi. Kwao ni bora kusafiri kwa ndege kuliko kupanda basi linaloenda polepole. Huwa wanapenda kusafiri daraja la kwanza kama wakikosa kabisa basi watasafiri daraja la pili.
Ukiwa katika likizo pamoja na mwenye nyota hii unaweza ukaudhika kwa sababu wao mara nyingi wanatafuta mambo mapya na wanakuwa hawatulii sehemu moja kwa kutegemea ujasiri wao.
Kwa ujumla kwa vile wenye nyota ya Punda ni watu wasiokuwa na subira kwa rafiki zao wa duniani hawapendi kungoja watu wakubaliane na mipango yao ya safari ambayo wanaweza kubadilisha bila taarifa. Kwa sababu hiyo mara nyingi wanasafiri peke yao, au wanaweza kujitenga mbali na walio karibu nao. Hivyo watu wa Punda wanashauriwa kuwa na subira ya kuwangoja wenzi wao katika likizo au safari zao.
NYOTA YA PUNDA (TABIA ZAO)
Tabia ya wenye nyota ya Punda ni wakali na wachangamfu, wenye hisi na wanaoweza kujieleza wakiwa na ari ya kufanya chochote. SASA HIVI hivyo ndio mambo wanayotaka kusikia.
Ni watu wasiokuwa na surbira, kila kitu kinafanyika kwa msukumo na haraka haraka. Wenye nyota hii ni viongozi majasiri ambao hawaoni karaha kuchukua majukumu. Wao
wakati wote wanajiona kwamba Wanajua sana.
Pamoja na kwamba wanakuwa wa kwanza kukamata mambo ya msingi ya jambo lolote wao wanakuwa wa mwisho kuliacha na ni wafuatiliaji wazuri.
Kwa upande mwingine watu hawa wewe wape njia ya kutatua tatizo au ya kufanya
jambo jipya, utashangaa jinsi watakavyolichambua na kulitekeleza jambo lenyewe.
Jambo la kushangaza kwa wenye nyota hii ni kwamba tatizo lao kubwa linakuwa kusitasita au kuchelewesha jambo. Pamoja na kwamba wao wanapenda mambo ya haraka lakini yakiwa hayawavutii basi huwa hawana haraka nayo.
Vile vile wanaweza kuwa butu. Mara nyingine hufanya makosa makusudi au kuwachokoza wafanyakazi wenzao kuonyesha ubinafsi wao ili wafanikiwe.
Kwa ujumla wenye nyota hii ni watu ambao wanajipendelea. Ni watu ambao MIMI KWANZA ndio tabia yao wanapenda waonekane kwamba wao ndio wanajua zaidi na tabia hiyo inawasaidia, ukweli wa mambo ni kwamba wenye nyota ya punda kila walitakalo wanalipata.
{mospagebreak}
TABIA YA PUNDA (KATIKA NGONO)
Wanapokuwa chumbani, tatizo kubwa la wenye nyota hii ni ubinafsi. Watu wa Punda huwa wanapenda kujishughulisha sana na mambo ya ngono na wanategemea kwamba wapenzi wao nao wajihusishe kikamilifu katika tendo hilo. Wakiona kwamba wapenzi wao
hawako makini wakati wa ngono basi hujihisi kwamba hawapendwi na hawatakiwi.
Wenye nyota hii ni watu wenye bashashi na wacheshi na hiyo inawafanya wawe ni watu wenye hisia kali na haraka, hivyo inakuwa vigumu kwao kufanya mambo kwa mpangilioi na pole pole. Hivyo inawafanya wasiweze kuwachezea wapenzi wao kabla ya ngono.
Hisia zao kubwa ni kufanya tendo la ndoa na ni wakati huo huo bila kungoja.
Kutokana na ubinafsi huwa wanasahau kabisa hisia za wapenzi wao. Kwa kweli ni watu ambao wanajipendelea sana katika tendo la ndoa na hiyo huwa inawaletea matatizo katika uhusiano wao wa kimapenzi.
Wakati wanapochagua mpenzi Punda wanashauriwa wahakikishe kabisa wanapata wapenzi ambao wana ashiki au nyege za haraka haraka kama wao.
Katika kipindi cha kubembeleza pendo (kutongoza) watu wa Punda wanatakiwa waonyehse tabia ya asili ya ukarimu na mahaba ili wapendeke na vile vile wajaribu kuachana na tabia yao ya asili ya hisia kali na ukali.
Wanaume wa nyota hii wanapenda sana kujiona kwamba wao ni mabingwa na mashujaa katika ngono.
Kwa ujumla watu wa nyota hii ni wenye kuhitaji sana ngono. Ni watu ambao hawataki kukataliwa. Wanaume wa nyota hii wana ashiki na hamasa za kufanya ngono kuliko kupenda na wanaliangalia hilo wanapotafufa wapenzi kwa wanawake nao wana hamu kubwa ya kufanya tendo la ndoa.
Hakika wenye nyota hii wanaweza kuwa wapenzi wazuri.
NYOTA YA PUNDA (KAZI ZAO)
Wote wake kwa waume waliozaliwa katika nyota hii wana kipaji cha asili cha uongozi na wasiwasi wa kushindwa katika utekelezaji.
Kwao kitu cha pili au wao wenyewe kuwa namba mbili. Wanawake katika hali ya ushindani ambapo wanaweza kutekeleza kazi zao katika spidi au haraka wanayoitaka ambayo mara
nyingi inakuwa mara mbili ya spidi ya kawaida, kila kitu kitakuwa sawa.
Wenye nyota hii huwa wanafanya vizuri shughuli zao za kazi au taaluma, mradi shughuli hizo ziwe zinazoleta athari. Hawapendi kuburuzwa wala kuishi bila kupata ushindani ni kawaida mara nyingi katika kazi zao hutokea migongano kati yao na wale wenye mamlaka
juu yao. Wanapenda sana kupambana na hali ya ushindani wa kikazi na mara nyingi huwa wakiasisi shughuli mpya au kutoa mawazo mapya. Vile vile wanapenda sana ushindani wa kutafuata kitu kilichopotea.
Watu wa Punda ni watu ambao wanaweza kuhisi jambo lolote, ni watu wanaopenda kutumia nguvu katika kazi na wakifanya kazi yoyote wanaifanya kwa moyo mmoja.
Wakiwa katika kazi, hupenda kufanya kazi peke yao au katika kazi hiyo wawe ni wasimamizi.
Kwa ujumla kwa vile watu wa Punda wanafanikiwa katika ushindani wanafurahi sana wanapofanya kazi ambazo zenye vipingamizi na ambazo utekelezaji wake unahitaji akili nyingi na nguvu.
Watu wa aina hii wakishindwa kutekeleza majukumu yao huwa wanavunjika moyo vibaya sana. Wanapenda sana kufanya kazi katika mazingira ambayo yanahitaji muda maalum kutekeleza mambo fulani.
{mospagebreak}
NYOTA YA PUNDA (FAMILIA ZAO)
Wazazi wenye nyota ya Punda wanakuwa wakarimu sana kwa watotowacheshi watafanya kila njia kuwahimiza wawe huru na watawaruhusu wafanye majaribio mbali mbali ya kimaisha na kuwahimiza kuchukua majukumu makubwa kwa gharama yeyote. vile vile watawahimiza watoto wao wawe na tabia ya ushindani badala ya kuwafundisha michezo.
Wazazi wenye nyota hii watawapa watoto wao nafasi kujisimamia wenyewe katika mambo yao. tatizo lao moja ni kuwa hawapendi watoto ambao ni vinganganizi na wanaohofia usalama wao.
Watoto ambao ni waangalifu waoge na wanaofanya mambo kwa kufikiria wanakuwa hawaendani sana na wazazi wenye nyota ya Punda kwa sababu Punda hawapendi watoto wenye haya, waoga na wepesi kutishwa.
Wazazi wa nyota hii wanaweza kuwa wakali, wasiokuwa na mbinu na wenye kauli za ukali ambazo zinaweza kuudhi mtoto yeyote mwenye moyo mdogo. Tabia hii mara nyingi inasababisha migongano kati ya mzazi na mtoto na kutokuelewena kunakuwa kukubwa.
Wazazi wa Punda wanashauriwa kujilinda katika kuwashinikiza watoto wao kwa nguvu na haraka na kuwaruhusu watoto hao wakue na wafanye vitu katika njia za kawaida.
Kwa ujumla wazazi wa Punda ni wenye msukumo lakini wanajivunia sana watoto wao ni wazazi wenye makaka na wanapenda sana utani kwa vile hata wao mioyo yao ni ya kitoto. Mzazi wa kike anapenda ushindani hasa katika mausuala ya maisha na kuishi lakini hata yeye anapenda utani hasa anapokuwa nyumbani.
NYOTA YA PUNDA (MAUMBO YAO)
Wenye nyota ya Punda ni wenye uso mrefu mpana paji lao la uso hutanuka likiambatana na fuvu lililokaa vizuri. Macho yao ni makali na yenye kuonyesha uzima na uhai na yaliyotumbukia kwa ndani.
Nyusi zao ni nyeusi zenye kuonekana wazi au zilizo dhahiri kama zimepakwa wanja. Pua
zao ni za bapa na midomo yao ni mipana.
Unapozungumza na wenye nyota hii naye atakusimamia wima mbele yako na kukuangalia moja kwa moja kwenye macho yako.
Tabia yao hiyo inawafanya waonekane wao ni wenye tabia za kigomvi au ushauri lakini ukiangalia kwa undani utagundua kwamba ni wakweli na wanaoweza kuaminiwa.
Hata hivyo kipindi cha kukusimamia wima inakuwa kifupi hasa anapokuona mpuuzi.
Kimaumbile ni watu wepesi na mwendo wao ni wa madaha. Miili yao kidogo imeinamia mbele ya misuli yao inaonekana imekakamaa, hiyo ni kwa sababu ya kujishughulisha sana bila kupumzika.
Sifa za wanaume wa Punda ni kwamba wako makini na wenye msimamo. Ni wembamba na miili yao ni yenye misuli iliyojikunja kunja.
Wanawake nao ni wembamba na maumbile yao siyo ya kupendeza sana, mikono yao na miguu yao ni yenye nguvu. Matamanio yao na uwezo wao huwa inawafanya wawe wanawake wenye tabia za kiume.
Kwa ujumla alama ya Kondoo ni pembe zake na mambo yote yanayohusiana na pembe hizo. Wenye nyota hii wanapenda kupambana na maisha. Kimaumbile athari zao huonekana mara moja. Kama vile kujiamini, namna wanavyosalimia watu na vicheko vyao. Vitendo vyao hivyo vinakujulisha kwamba huyu ni Punda.
{mospagebreak}
NYOTA YA PUNDA (VYAKULA VYAO)
Kama ilivyo katika tabia zao wenye nyota ya Punda vile vile wanapenda vyakula vya haraka haraka.
Ukweli ni kwamba mawazo yao mara nyingi yanakuwa katika maisha kuliko chakula pamoja na kwamba wanakuwa na hamu na uwezo mkubwa wa kula. Wanapenda chakula kizuri lakini kiwe cha haraka na rahisi kutayarisha.
Wanapenda sana kufanya karamu tafrija ambazo wana kipaji kikubwa cha kuzitayarisha na wanazifurahia. Katika karamu hizo vyakula vyao vinakuwa vya haraka ambavyo vinagawiwa wima wima bila kucheleweshwa.
Wakati wanapokuwa hawafanyi karamu au tafrija wanapenda chakula chochote
kinachotayarishwa upensi na ambacho kinaweza kulika huko wanatembea, kama vile asusa na vyakula vyepesi kama biskuti, chipsi n.k.
Wanapenda ladha iwe nyepesi na viwe na pili pili na viungo vingi. wanapenda sana vyakula vinavyopooza au kutuliza njaa kama viazi, tambi na maziwa.
Huwa wanapenda sana ladha za uchachu kama limao limao au ndimu ndimu au mbilimbili vile vile wanapenda sana mkate na Jibini au vyakula vilivyo kaangwa kama nyama.
Wanatakiwa wawe waangalifu katika kula mafuta hasa vyakula vya kipuuzi puuzi ambavyo vinaweza kuwaletea madhara.
Kwa ujumla wenye nyota hii wanapenda sana tafrija, na vyakula wanapenda viwe vile vinavyotayarishwa mbele ya wageni na viwe vilivyokaangwa na vyenye ladha nzuri. Vyakula hivyo viwe ni vyepesi kutayarisha visivyopoteza muda.
NYOTA YA PUNDA (VIPAJI VYAO)
Wenye nyota hii wanapenda sana kupambana na maisha na wanakuwa na mambo mengi sana vichwani mwao kiasi kwamba wakati mwingine wanasahau vipaji vyao vya asili.
Tabia hiyo waliyo nayo haiwapi muda wa kufanya mambo mengine kama ya ubunifu. Kwa
asili, wao ni watu wabunifu na wakati mwingine wanapata wasiwasi katika ubunifu wao.
Kuna wakati wenye nyota hii wanashindwa kutofautisha kati ya vipaji vyao na matakwa yao. ambayo yanakuwa makubwa na yenye shinikizo. Watapata msaada katika hili iwapo watafanya jitihada za maksudi za kuwasiliana na busara zao za asili kuwa kupata
mapumziko na kufanya taamuli (Meditation).
Kipaji cha wenye nyota hii kinahusiana na kichwa ambacho ndio nyota yao inapotawala hivyo Frenologia (Ujuzi wa tabia ya mtu kwa umbo la kichwa chake iko chini ya nyota hii.
Kwa kuongezea wenye nyota hii wana kipaji cha kutafsiri ndoto na kipaji cha kusikia sauti ndani ya kichwa.
Kwa ujumla watu wa Punda wanapenda njia ya utabiri ambazo zinatoa matokeo ya haraka kama vile kutumia karata , dhumna, au dadu (dice).
Taamuli (meditation) ni jina au mbinu nzuri kwa wenye nyota hii kuongeza kipaji chao. Ikiwa watafanya taamuli kwa dakika ishirini wakati wa usiku au kitu cha kwanza wanapoamka asubuhi, akili na miili yao itatuliza. Hivyo itawafanya wawe na uwezo wa kutumia nguvu zao za kimwili na kiakili pamoja na kuendeleza au kukuza vipaji vyao.
{mospagebreak}
NYOTA YA PUNDA (BAHATI ZAO)
Watu wa nyota hii wana tabia ya kitoto ya kuamini kwamba mazuri yatatokea kwa amri ya Mungu. Kwa hiyo inawawia vigumu kufikiria uwezekano wa kushindwa katika jambo lolote.
Wakiwa ni waliozaliwa katika nyota yenye kuasisi mambo, wengi wao hudharau kutopata matumaini katika jambo moja na kurukia jambo lingine.
Kwa sababu shauku yao ni ya kuambukiza mara nyingi hufanikiwa kuwashawishi wengine wakubali kuongozwa nao hata kama kuna khatari.
Mara nyingi hawana muda wa kutoa mashitaka wala kuwaza makosa yaliyofanyika mwanzoni, wao wanaamini kwamba wakati wote mafankii yapo na kwa vile wamezaliw ana roho ya ujasiri wa kupenda vituko wako tayari wakati wowote kuyaweka maisha yao katika hatari ili wafanikiwe.
Tabia yao ya kutojali na misukumo au mihemko ya ghafla inawafanya wawe na sifa zilizokithiri za kubahatisha mambo.
Hakimu kwa bahati, hii kwao inakuw asiyo tatizo kwa sababu hawafanya kitu kimoja kwa muda mrefu, ghafla huwa wanarukia katika jambo lingine.
Watu wa Punda wana moyo wa ujasiri wa ushindani na wanafanya vizuri iwapo katika hali hiyo kutakuwa na uadui hasa mtu na mtu.
Katika michezo ya karata ua kupimana nguvu au kuwekeana dau watu wa Punda wana pata bahati sana.
Kwa ujumla watu wa nyota hii wanapenda kubahatika na wanachukia sana kukosa pamoja na kwamba faida zoa wanazopata zinalingana na hasara zinazowafika.
NYOTA YA PUNDA (URAFIKI)
Wenye nyota ya Punda ni wachangamfu, wanaosema kweli na wenye uwazi katika urafiki wao. Kama walivyo katika kila kitu kwenye maisha yao.
Ni wazuri katika kuanzisha urafiki, wakati mwingine wanakuwa wawazi sana katika mazungumzo yao na vitendo vyao kiasi kwamba huwaogopesha baadhi ya marafiki.
Kwa upande mwingine wao wanapendwa kwa sababu ya uaminifu wao na kusema kweli.
Watu wa Punda wanathamini sana uhuru wao na wanapenda kufanya vitu katika njia zao wanachukia sana kufugika au kuogopa watu kwa hiyo urafiki sio kitu muhimu kwa wenye nyota hii . wakati mwingine huwa wanajisikia furaha wanapokuwa katika kundi la watu wanaopenda vituko na mambo ya ajabu.
Watu wa Punda wako katika kundi moja na wale wenye nyota zenye asili ya moto na tabia zao zinafanana. Mfano wale wenye nyota ya Mshale wanakuwa marafiki wao wazuri ambao wanachangia tabia ya kupenda vituko.
Hata hivyo huwa hawapendi au hawaoni umuhimu wa kuwa na rafiki mwenye nyota ya
Mapacha. Kwa wenye nyota ya Ndoo kwa vile wanathamini uhuru wao basi wao wanaweza kuelewana nao.
Watu wenye nyota zenye asili ya udongo Mbuzi, Ngombe na Mashuke wanakuwa marafiki wazuri wa Punda kwa Sababu wanamsaidia kutekeleza mipango yake kivitendo, pamoja na
kwamba madhari na akili za hao Ngoombe, Mbuzi na Mashuke kupunguza nguvu ya urafiki wa kudumu.
{mospagebreak}
Kwa ujumla wote wenye nyota zenye asili ya moto mara kwa mara wanakuwa na tofauti na wenye nyota ya Punda hasa katika masuala ya ushindani mfano ni nyota ya simba na Punda wote huwa wananeemeka kutokana na uadui usioepukika katika urafiki wao, kama ikiwa katika kazi au nyumbani au kwenye starehe au wanapokuwa pamoja katika michezo.
NYOTA YA PUNDA (MITINDO)
Mitindo ya Punda ni yenye kuchangamka na nguo zisizo na madoido. Wanapenda wawe wanavaa kulingana na wakati. Mavazi yao huwa yanaambatana na mabegi, saa nzuri au mikufu na vito vyenye kupendeza.
Hata hivyo watu wa Punda hawapendi kupanga kununua au kushona nguo. Wanapendeza sana wakiwa katika mavazi ambayo ni mepesi kuliko nguo zile zilizosanifiwa na zenye madaha.
Suti zilizotafauti yaani suruali na koti tofauti, zikiambatana na buti pamoja na skafu na glavu ndio mavazi hasa na nyota ya Punda. Mavazi hayo yanaendana hasa na tabia yao ya ujasiri na mambo ya ajabu.
Wengi wenye nyota hii huwa wanapenda kuvaa suti za michezo ambazo pia zinaendana na namna yao ya maisha.
Wanapoamua kuvaa nguo, waume kwa wake wanakuwa wavaaji wazuri. Wanapenda nguo zilizoshonwa vizuri na zinazoeleweka.
Rangi zao zinakuwa Nyekundu na Njano na mara nyingi hupendelea nguo zisizo na nakshi.
Wanapenda mitindo thabiti na vitambaa ambavyo ni vyepesi kuvitunza. Wanawake wanapenda sana mikufu ya dhahabu na hereni za kuninginia.
Kwa ujumla watu wa punda wanapenda kuvaa kulingana na mitindo na wanapenda nguo ambazo zinawafanya watu wakiwaona washituke wakiamua kuvaa nguo maalum basi mavazi hayo yataambatana na vitu vya ziada kama mikufu. Pete, saa visivyo ghali. Hiyo huwainawafanya waonekane na wakati katika mavazi ya aina yeyote.
NYOTA YA PUNDA (TASWIRA YA UMBO)
Inapofikia hali ya kuweka miili katika hali bora wenye nyota hii wana bahati kubwa kutokana na hali halisi ya maisha yao ya kujishughulisha. Kwa kuongezea labda wawe wanapenda kula lakini kama ilivyoanishwa na nyota yao ni watu ambao hawapendi sana vyakula vinavyoweza kuwaletea unene.
Hata hivyo wanafurahia chakula na wanapenda vyakula vyepesi. Kama ikiwa Kalori zinazoingia mwilini zinazidi zinazotoka basi uzito wao huongezeka.
Inapofikia hali ya kupunguza uzito wenye nyota hii wanakuwa hawana subira, wanapenda mlo ambao utapunguza uzito wao upesi na katika muda mfupi inavyowezekana ikiwa ni pamoja na kujiadhibu wenyewe kwa kujimyima chakula kwa muda mfupi wakiwa na imani yakupata matokeo.
Kwa wenye nyota hii muda wa siku chache au hata wiki moja ni muda tosha wa kujinyima chakula ili kupunguza unene.
Baada ya hapo ni juu yao kuwa na ratiba maalum ya ulaji wao ikiambatana na mazoezi ya kila siku, kama kuongelea, kukimbia, au kutembea kwa nguvu kwa muda mrefu wenye nyota hii wanahitaji mazoezi ya kila siku ili waweze kupunguza uzito. Vinginevyo itawawia vigumu baadaye.
{mospagebreak}
Kwa ujumla wenye nyota hii huwa wanapata uzito mkubwa kwa sababu huwa wanajishughulisha sana kula milo ya kawaida ikiambatana na vitu vitamu vilivyojaa Kalori wanapokuwa wamechoka.
Wanashauriwa kutumia muda wao kula tu milo ya kawaida hiyo itawasaidia kuondoa au kupunguza unene na kuboresha afya zao.
NYOTA YA PUNDA (USHINDANI NA UADUI)
Wenye nyota hii wanapenda sana ushindani na kuonyesha madaraka na uwezo wao, kwa sababu hii wanachukiwa na watu wengi. Wanapenda sana wawe wa kwanza na watatumia mbinu zozote ili wafanikiwe.
Punda wako wazi na waaminifu katika malengo yao ni watu wenye kusema ukweli na haamini visingizio, ulaghai wala kuficha siri.
Wanapenda kufanya mipango yao moja kwa moja na mtu yeyote akiingilia huwa unazuka ugomvi. Ikitokea hivi watu wa Punda huwaeleza wagomvi wao bila kuficha kinachoendelea.
Kutokana na ukweli na uwazi wao wenye nyota hii huwaudhi sana watu wengine kwa maneno yao na vitendo vyao.
Ni tabia yao kutojali hisia za watu na wala hawana muda wa kufikiri, maneno wanayosema au vitendo vyao vitawaathiri vipi wenzao.
Mara nyingi watu wa Punda, hushinda vita vyao kutokana na uwezo wao na nguvu zao za ukatili lakini ikitokea pakatakiwa kujieleza au kutoa hoja au diplomasia huwa wanashindwa kujieleza.
Wakiwa katika siasa hali ya uadui huibuka kutoka kila upande, wao huneemeka sana Kisiasa kutokana na upinzani na uadui mkali uliopo duniani ambao wao hufurahia.
Kwa ujumla watu wa Punda ni washindani katika sehehmu zote, ni madereva wanaopenda kwenda kasi hivyo wanapenda mashindnao ya magari. Mara nyingi watu wa nyota hii wanapenda michezo yenye ushindani au kutumia nguvu ikiwa kama jambo la kupitisha muda au kazi yake, na hii inawapa changamoto katika kuendeleza ushindani wao wa Asili.
NYOTA YA PUNDA (MANUNUZI)
Kama tulivyoona tangu mwanzo wenye nyota hii wanapenda ushindani, kushughulika na vitendo na hawapendi kabisa kufuata utaratibu kwa hivyo kununua vitu ni mojawapo wa mambo wanayoyapenda sana.
Vile vile wanapenda kupungua na kupanda kwa manunuzi au msisimko wa kwenda dukani
katika mitaa inayopendeza au katika nchi za nje.
Wenye nyota hii wanapokwenda kufanya ununuzi hufanya juhudi ya kuamka mapema ili wawakwepe watu, na manunuzi yao wanayafanya haraka haraka.
Huwa wanakwenda kutoka duka moja hadi jingine wakizunguka kiuerevu kufanya manunuzi.
Wanapenda kununua vitu vya wiki nzima na orodha yao lazima vitakuwepo vyakula vya kupikwa kwa haraka au vya kuliwa papo kwa papo kama nyama za kopo au Samaki wa Kopo. Mara nyingi hawana muda wa kupika na hawapendi kutumia muda wao mwingi jikoni.
Kwa hiyo kitu ambacho hawa watu wa Punda wanapenda kununua. Jibu ni kwamba wanunue chochote ambacho kitaharakisha mwendo wa maisha yao.
Mfano wanapenda magari yanayo kwenda kasi au vitu ambavyo wanaviota, kama ramani, glavu za kuendesha gari na viatu.
Kwa ujumla watu wa Punda huwa hawapendi kwenda dukani kila siku lakini wanaona raha ikiwa kwa kufanya hivyo watapata ushindani.
Wanapenda kushindana na rafiki zao ili kuonyesha nani atanunua mwanzo na kitu kizuri au kubishana katika bei ya kitu fulani, hiyo inawafanya wajisikie raha sana.