Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumapili, 2 Aprili 2017

KAMA UNA NYOTA YA NG'OMBE TAZAMA TAARIFA ZAKO ZOTE HAPA

Hii ni nyota ya pili katika mlolongo wa nyota 12.Wenye nyota hii ni wale ambao wamezaliwa kati ya tarehe 20 April na May 20 ya mwaka wowote.

  • Sayari yao ni Venus (Zuhura).
  • Siku yao ya bahati ni Ijumaa.
  • Namba yao ya bahati ni 6.
  • Rangi yao ya bahati ni kijani.
  • Asili ya nyota yao ni Udongo.

KIPAJI CHA NG'OMBE

(BODY-CENTERED)
Wenye nyota hii wana kipaji kikubwa kilicho ndani ya mwili wao ambacho ni pamoja na kuelewa mambo kimbele, hesabu, kuponya kwa kutumia mikono na kwa kumwagia mtu maji.

TABIA YA NG'OMBE:
 


Wenye nyota hii ni watu wanaopenda kujishughulisha katika shughuli nyingi. Ni watu wakarimu na wanaopenda kusaidia watu, na wana tabia ya uvumilivu na subira katika jambo lolote wanalolifanya.
Ni watu wenye malengo na wenye msimamo thabiti, wasiopenda kupindishwa na wana tabia ya ubishi na ukaidi hasa katika jambo lao wanalolitaka.

TABIA YA NG'OMBE KATIKA MAPENZI:


Wenye nyota hii ni waaminifu sana katika mapenzi na wanaohitaji ulinzi katika mapenzi na njia au mwenendo unaoeleweka.
Pamoja na kwamba asili yao ni udongo, wanaweza kuwa ni wenye mahaba na mapenzi 

makubwa kwa wapenzi wao.
Uhakika wa mapenzi ndio jambo kubwa ambalo wenye nyota hii huangalia kwanza na baadae Penzi hilo liwe lenye hisia na mpangilio.

Pamoja na hisia kali walizonazo, wao ni watu imara na wasiobadilika hivyo kuwafanya watu wenye shauku kutovutiwa nao.
Uaminifu ni jambo la pili ambalo wenye nyota hii wanalo hivyo kuwafanya wao wawe watu wenye kuaminika na hiyo inasababisha wawe wenye wivu kupindukia.

Wanachotakiwa kufanya ni kujitahidi kuwapa nafasi wapenzi wao la sivyo watajikuta wako peke yao. Ndoa kwao ndio uamuzi mzuri kuliko kuishi na wapenzi. Tabia yao ni ya kudumisha jambo fulani wanaloliamini au walilolianzisha na hawapendi kubadilishwa.
{mospagebreak}

MATATIZO YA KIAFYA:


Nyota hii inatawala shingo, koo, koromeo, kidevu na sehemu ya chini ya taya.
Kwa asili wenye nyota hii ni watu wabishi na wenye kufanya mambo kwa upole na wagumu kubadilika.

Wanapenda sana vyakula vitamu na vyenye mafuta na huwezi kuwabadilisha katika hilo na wengi wao wanakuwa wanene kupita kiasi na inakuwa ni vigumu sana kuwashawishi kuamka na kufanya mazoezi ya mwili.

Tatizo lingine ni kufanya kazi kupita kiasi ambalo linawafanya wapate matatizo ya mvutano na misuli hasa katika sehemu zilizotajwa. wenye nyota hii wanatakiwa wajihadhari na mpangilio wao wa chakula na wafanye mazoezi kwa wingi.

KAZI ZA WENYE NYOTA YA NG'OMBE:


Wenye nyota hii wana falsafa ifuatayo kulingana na kazi; "panda mbegu iote, mti uote halafu ule matunda". Ni watu ambao wanafuata mpangilio wa kikazi na wanaopenda kujituma na kujishughulisha. Wengi wenye nyota hii ni wafanyakazi wazuri na wanapenda 

wapewe muda kujenga vipaji na utaalamu wao wa kazi.
Kazi zao zinakuwa kazi za muziki, kazi zinazohusiana na chakula, hoteli, migahawa, kazi za ujenzi, kazi za mashamba, kazi za uhasibu, na kazi za sanaa hasa uchoraji au uchongaji vinyago.

FAMILIA ZA NG'OMBE:


Wazazi wa familia za Ng'ombe ni watu wenye msimamo, wakutegemewa na wanaothamini familia zao, na wako tayari kugombana na mtu yeyote kwa ajili ya watoto wao.
Ni wazazi wanaopenda kufuata mambo ya kizamani au ya asili hasa katika masuala ya nidhamu. wanapenda sana kuheshimiwa na watoto wao na huwashawishi au kuwashauri wawe huru.

Ni wazazi wanaotegemea watoto wao wafuate nyayo zao hasa katika biashara au kazi wanazozifanya, hivyo watoto wa wazazi Ng'ombe wanakuwa na muda mdogo wa kufikiria mambo mapya.

Ni wazazi ambao hufanya kazi kwa bidii kuhakikisha watoto wao hawakosi wanachokitaka na wanapenda watoto wao wawe na elimu nzuri. Hata hivyo ni wazazi ambao wanategemea watoto wao wafuate wanavyotaka wao vinginevyo inakuwa matatizo.

MADINI YA NG'OMBE:


Wenye nyota hii wanatakiwa wavae vito vinavyoitwa ALMASI au EMARALD.
Mawe haya yanawafanya wenye nyota ya ng'ombe wawe katika hali yao ya kike kike (Feminine) vili vile thamani ya mawe haya ni uthibitisho wa nyota hii katika fedha.

UHUSIANO WA KIMAPENZI:


(NG'OMBE NA N'GE):

Tabia ya uaminifu na ukweli waliokuwa nao wenye nyota ya ng'ombe inakuwa ni faraja kubwa kwa nyota ya Nge ambao wana tabia ya wivu kupita kiasi na kudhania maovu, kutuhumu na kushuku.

VYAKULA VYA NG'OMBE:


Wenye nyota hii wanashauriwa wapende kula vyakula vifuatavyo ambavyo ndivyo vinavyotawaliwa na nyota yao; Tofaa (apple), (oysters), viazi mbatata (potatoes), na dover sole.

NCHI ZA NG'OMBE:


Ili kupata mafanikio ya kinyota, kwa wale wenye uwezo wanashauriwa aidha kuishi au kutembelea nchi au miji ifuatayo ambayo inatawaliwa na nyota yao; baadhi ya nchi hizo ni USSR (Urusi), Ireland, St louis,na Lucerne (Switzerland).

RANGI ZA NGOMBE:


Wenye nyota hii wanashauriwa kinyota wapake au watumie rangi za kijani au rangi za pinki au rangi ya bluu ambayo haijakoza katika nyumba zao au sehemu zao ya biashara ili kuleta mvuto wa kinyota.