Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumanne, 18 Aprili 2017

MAFUTA ASILIA KWA AJILI YA KUKUZA NYWELE ZAKO NA KUZIFANYA ZIWE LAINI

Watu wengi hupenda sana nywele zao ziwe katika muonekano mzuri na zenye afya tele,katika hali ya kutafuta mafuta ya kuweza kuziboresha zaidi watu wengi hujikuta wakitumia gharama nyingi katika kununua mafuta mbalimbali yenye makemikali na hatimaye kujikuta wanapata athari ktk nywele zao bila kutegemea.

Le nitazungumzia mafuta mafuta mazuri ya asili ambayo yana uwezo mkubwa wa kujaza nywele zako,kuzifanya ziwe imara na zenye kupendeza muda wote


MAFUTA YA PARACHICHI


Mafuta haya yana virutubisho vingi kama vile A,B,D na E,Protin,iron,magnesium ambazo husaidia kukuza nywele 

Mafuta haya pia hurekebisha nywele zilizokatika,yanalainisha na kungarisha nywele na pia kuzilinda kutokana na kuungua na jua kali.

pia unaweza kuyatumia kwa kuchanganya na shampoo wakati unaosha nywele zako.


MAFUTA YA MNYONYO

Mafuta haya yana vitamin E na protini kwa wingi ambayo inasaidia kukuza nywele na kuziepusha na kukatikakatika,kama nywl zinakusumbua jaribu mafuta haya sasa uone maajabu yake,
~huondoa mba kichwani mwako
~kuponya vidonda vya magonjwa ya ngozi kichwani
~zinakuza nywele zako mara3 zaidi ya ukuaji wa kawaida
chukua haya mafuta na uwe unamassage polepole kichwani
wengi waliotumia mafuta haya wanakiri nywele zao kukua kwa haraka kuliko kawaida


MAFUTA YA NAZI

Mafuta haya husaidia sana kuzipa nywele unyevunyevu kama zikiwa ni nywele kavu sana,unaweza kutumia mafuta haya kama conditioner,ukishaosha nywele zipake haya mafuta yanasaidia kukuza nywele pia kuondoa mba.