kwanza niweke tahadhari ya picha! Baadhi zitakuwa
zinatisha
picha ya tai wanakula mfu, hiyo ni Tibet na kwa imani yao hao tai ni malaika kwahiyo kwa kuwalisha mfu wanapata thawabu ....
Mila na tamaduni pia vina mchango mkubwa kwenye haya mambo ya kiimani
Sisi wakati tukiwashangaa wanaochoma moto maiti, nao wanatushangaa kwakuwa kwao kuzika mfu kwa kumfukia ardhini ni kuinajisi ardhi, ni kuitia nuksi mikosi na balaa, kinachokufa kinapaswa kuteketezwa hii ni imani yao lakini wakati ukishangaa hawa wanaochoma moto maiti kuna hawa ambao wao hawachomi wanasema ni kuharibu chakula ambacho kingewafaa wengine
Kwa imani yao ni kwamba uliweza kuishi kwakuwa kuna wanyama ulikula nyama yao na ikakuponya na njaa na afya ukapata
Kwahiyo unapokufa ni zamu ya nyama za mwili wako kutumika kulisha wengine, huzikwi wala huchomwi moto... Huku Afrika kuna kabila wao maiti hujengewa kichanja na kuachwa hapo iwe chakula cha wanyama, lakini kwa wengine huiandaa kabisa kwa kuikatakata , zaidi kuna tamaduni nyingine maiti hulishwa kwa wanyama kwenye kusanyiko maalum
Ukishangaa ya Musa bado hujaona ya firauni......
Kumbuka umekula nyama ngapi mpaka umri huu? Usipokuwa mbinafsi na mchoyo nawe utakubali mwili wako uwe chakula cha wengine utakapokufa!