Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumapili, 25 Septemba 2016

JE UNAIJUA MAANA YA NAMBA 666?


Kwa watafiti huru wa mambo ya UFO na New World Order ni kuwa serikali na ‘sayansi’ wanapigia debe taarifa hizo kwa lengo lilelile la New World Order ambayo kiongozi wake atakuwa na ‘damu takatifu’ na mwenye nguvu za maajabu.

Mmoja anaye tegemewa ni wazo ambalo liko kwenye imani ya dini mbalimbali duniani, ikiwemo kwenye Uyahudi, Uislamu na Ukristo na bila kusahau kwenye imani na dini za kishetani ukiwemo Freemasons. 


Hiyo ni 666 katika lugha yake ya asili ...

Wote wanasubiri juu ya kuja kwa Messiah, ambaye atakaye kuja kuuokoa ulimwengu. Kutokana na mafunzo na falsafa za kimasonia ni kuwa Masiha wa kwanza, yaani Yesu alikuja kwa ajili ya kusimamisha ufalme wa mbinguni, lakini Masiha wa mara ya pili ambaye ni …? Atakuja kuisimamisha New World Order chini ya utawala wake.

Kuhusiana na Masiha huyo, Freemasons wa daraja la 33 Manly P. Hall,katika kitabu chake cha “The Secret Destiny of America ameandika hivi,

Jawabu la mpango huu wa siri ni World Order chini ya mfalme mwenye nguvu za kimaajabu. Mfalme huyu anatokana na ukoo wa wenye damu tukufu; hii ni kusema, anatokea kwenye asasi ya Illuminati na walio na hekima, anatokana na familia ya mashujaa ya binadamu walio wakamilifu”

Mtu aliyetajwa na Hall sote tunamjua ni nani, ametajwa vizuri kwenye vitabu vitakatifu, hasa kwenye mafundisho ya Kiislamu. Wasomi na watafiti huru  dini zote watakubaliana na mimi kwamba hakuna dini iliyo weza kuelezea vyema maisha yatakayo kuja na alama zake, maisha ya kaburi na maisha ya motoni na peponi kama Uislamu, na mtu huyu ametajwa vilivyo na alama zake mbalimbali katika mafunzo hayo ya Uislamu.

... .... vurugu za New Age, lakini kwa kiasi fulani vurugu hizi zinawiana na yule mmoja anaye ngojewa, tumchambue kidogo kwa mustakabali wa sura hii  (Sura hii kwenye kitabu hicho nimeipatia jina la: Wageni Wanarudi Tena ...) Tukianza na kitabu cha Ufunuo kwenye biblia tunakutana na habari maarufu sana ya ‘mnyama’ kama ifuatavyo.

“Anataka kila mmoja – mkubwa na mdogo, tajiri na maskini, mtumwa na aliye huru wapewe chapa kwenye mkono wa kulia au katika paji la uso. Hakuna atakaye nunua au kuuza chochote pasipokuwa na chapa, ambayo ni jina la mnyama au ile namba inayowakilisha jina lake. Inahitaji hekima kufahamu mambo haya. Yeye aliye na ufahamu na aihesabu namba ya mnyama huyo, kwa kuwa ni namba ya kibinadamu. Namba yake ni 666” .

Mbali na kuwa na tafsiri mbalimbali juu ya mnyama huyo ni nani na anawakilisha nini kwenye maelezo hayo hapo juu, watu wengi wame chukuliwa sana na maneno ya mwisho ya kipengele hicho, yaani 666. Lakini mbali na hilo dunia ya leo tunaona ni namna gani ilivyo mezwa na vitu mbalimbali kutoka, alama na nembo, mpaka majina na herufi za 666. Nami pia sitajikita katika kutaka kufahamu pembe au kichwa au kinywa cha mnyama huyo kinawakilisha kitu gani ila nitakwenda moja kwa moja kwenye jina lake nalo ni 666.

Wakati nilipo kuwa nasoma hadithi za Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) kuhusu Dajjal na vitimbi vyake nilikuwa nashangaa kwa nini Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) amekuwa akituonya mara kwa mara juu yake, wakati ameshatuambia muda mrefu kuhusu alama zake ambazo itakuwa ni rahisi kwetu sisi kumtambua na kumkana, Mpaka nilipokuja kufahamu Freemasons ni nani na wanafanya nini ndipo nikafahamu kuwa ni kweli Mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) alikuwa na haja ya kutuonya sana juu ya mtu huyo. Wanao muandalia kiti chake cha Utawala wa Dunia tayari wameshatufunga kwenye minyororo yake hata kabla ya Dajjal mwenyewe hajafika itakuwaje ndugu yangu Dajjal mwenyewe atakapo kuja?

666 ---- Kwa Wagiriki wa zamani wakati kila namba ilikuwa ni sawa na herufi, namba 6=W, yaani namba sita inachukuliwa ni sawa na herufi W.www kwenye mtandao wa internet, ingeweza kuwa W, au WW lakini mtu fulani akachagua iwe WWW yaani 666! Hivyo ufunguo wa tovuti yoyote ni666! Yaani badala ya kuanza na jina la Mola Wetu mtukufu kama inavyo paswa watu Fulani wanataka tuanze na jina la ‘mnyama’, 666.

Sarafu ya Ulaya Euro ina Nyota 6 upande wa chini, na Nyota 6 upande wa juu na mistari 6 inayounganisha nyota hizo, hivyo kutengeneza jina la mnyama, 666!

 Bar Code ya bidhaa zote za duniani ambazo zitauzwa nje ya mpaka wa nchi husika lazima ziwe na namba 666, iko hivi, mistari mingi, mingi unayoiona katika Bar Code hizo, mistari hiyo huwakilisha namba, nayo nambari sita (6) huwakilishwa na ‘bars’ au mistari miwili mirefu kushinda mingine, daima utaiona mistari hiyo mwanzo kabisa, katikati na mwisho mwa Bar Code, wakati mwingine utaona wame kuandikia nambari sita (6) chini ya ‘bars’ hizo mbili au wakati mwingine hawaandiki chochote, lakini lazima utaitambua tu, kwa vile yenyewe ni mirefu kupita mistari mingine, huenda hata kwenye kitabu hichi unacho soma ukaiona, au tizama bidhaa yoyote kutoka nje ya nchi yako, au inayo uzwa nje ya nchi yako na utaiona. Namba ya kwanza daima ni 6, namba ya katikati ni 6 na namba ya mwisho ni 6 vilevile, jina la ‘mnyama’ yaani 666.


Bar Code mpya ya Urusi kwa ajili ya kufuatilia watu wake ni 666,hii ni sawa na microchip (somo kuhusu mikrochip nitaliposti wakati mwingine).

Bunge la Ulaya lina viti 679, kila kiti kimoja ni kwa ajili ya mtunga sharia mmoja, mathalani kiti namba 663 ni kwa ajili ya Rep Souchet, 664 kwa ajili ya Thomas-Mauro, 665 kwa ajili ya  Zizzner na kiti namba 667 kwa ajili ya Rep Cappato. Wakati siti hizo zikiwa na majina ya wanachama wanao vikalia, kiti kimoja hakina jina la mwanachama anaye kikalia, na pia vilevile hakikaliwi na yoyote, kiti hicho ni namba 666.
Haswa kiti hicho ni kwa ajili ya mmoja anaye ngojewa, ambaye bado kufika, lakini nafasi yake ipo tayari inamsubiri. Ni kama muhuri wa Marekani ‘The Great Seal’ wenye nembo ya jicho moja na piramidi ambalo halijakamilika, muhuri huu nao unasemekana unamsubiri mmoja anaye ngojewa ambaye mpaka sasa tunamjua kama mnyama mwenye jina la666!


Nembo ya Umoja wa Ulaya ni ngao ya mwanamke aliyepanda mnyama! Mwanamke huyu naye ametajwa kwenye kitabu cha ufunuo.


“Kisha, Roho akanikumba, akaniongoza mpaka jangwani. Huko nikamwona mwanamke ameketi juu ya mnyama mwekundu. Mnyama huyo alikuwa ameandikwa kila mahali majina ya makufuru; alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.”


Lakini tukiachana na Umoja wa Ulaya, sehemu nyingi duniani, makampuni, wasanii wafanya biashara, wanasiasa na hata viongozi wa kidini kwa namna mbalimbali wamekuwa wakiipeperusha alama na nembo hii ya 666 kwa kila mtu kuona, na mazingira hayakuonesha kama vitu hivyo vimefanywa kwa bahati mbaya tu, bali kwa makusudi mazima.


Lakini ni nini hasa maana ya jina hili 666? Je tunaweza kumjua mmoja anaye ngojewa kwa kutumia jina hilo?


  Wakristo wengi wanafahamu kuwa 666 ni alama ya Mpinga Kristo ambaye Waislam wanamuita Masih Dajjal. Katika moja ya hadithi za mtume (Rehema na amani ziwe juu yake) inasema. Hata kama ataleta machafuko makubwa, neno Kafir litakuwa wazi limeandikwa katikati ya macho yake (ana macho mawili ila moja ni chongo halioni ndiyo maana mara nyingi anajulikana kama mwenye jicho moja), maelezo mengine yanasema neno hilo litaandikwa ‘Kaf’, ‘Fa’, ‘Ra’ kwa uwazi kabisa ili kila mtu aone.


“Hakuna nabii aliyetumwa isipokuwa aliwaonya watu wake kuhusiana na muongo mwenye jicho moja. Yeye ana jicho moja, lakini Mola wako si mwenye jicho moja, na baina ya macho yake pata andikwa ‘kaafir.


Kwenye Lugha ya Kiarabu herufi zilizo tajwa hapo ziko hivi;  ر ف ق Kama tutazigeuza herufi hizo chini juu tutapata kitu kinachofanana na 666. Lakini kutokana na mafunzo ya mtume (Rehma na Amani ziwe juu yake) herufi hizo zitaonekana kama zinavyo tamkwa kwenye lugha ya Kiarabu.

Wasomaji waelewe kwamba alama/namba 666 inatokana na tafsiri ya namba za Kigiriki kuja kwenye lugha ya kingereza nazo zinawakilisha jina la mtu ambaye wengi wanamuita Mpinga Kristo. Kwa hiyo tukiangalia kwa undani tunaona kuna majina mawili hapo, jina la Kristo na kuna jina laMpinga Kristo.  Jina hili Kristo Kigiriki ni Christos ambapo katika maandishi ya Kigiriki lingeandikwa hivi Χ ξ ς, ambapo kwa Wagiriki namba zilitumika badala ya herufi, jina hilo lilisomeka hivi ,yaani (ChiXi na Sigma) kwa hiyo  (chi) = 600 nayo ni herufi ya kwanza ya jina lake.  (xi)= 60inawakilisha nyoka na ni mfano wa herufi ‘E’ na  (sigma) = herufi ya mwisho ya jina lake, na ambapo jumla yake tunapata ni 666 kama ilivyoelezewa kwenye ufunuo 13:18 Namba hizo za Kigiriki zilizotumika badala ya jina Kristo.

Ilikuwa ni miaka 60 ya baraza la Umoja wa Mataifa, lakini umeona wakuu walivyo idizaini hiyo sitni na kusoemka 666, si kwa bahati mbaya hiyo jooo!!!! Some one get paid and perfome his job so well

 Kama nilivyo elezea hapo juu ukizitamka namba hizo unapata sauti hii Xes au Ches sawa na sauti ya “Jes” kwa Jesus. Herufi “J” ni herufi inayotokana na herufi “I” nayo ni ya mwisho kuingizwa kwenye herufi za lugha ya kingereza mnamo karne ya 16 na inatamkwa kama “Ye” na hii ndiyo maana jina Jesus linapoingizwa kwenye Kiswahili linatamkwa kama Yesu ambayo ni sawa na “Xes” Kigiriki na “Jes” kingereza. Wagiriki jina hiliChristos (Kristo) wamelichukua kutoka kwenye lugha ya Kiaramaiki kwa Wayahudi wa kale ambapo lilikuwa na maudhui yaleyale ya Jesus (Yesu)/ Yeshua/ Messiah.

Nadhani jamaa unamjua, lakini umeona nyuma yake kuna kitu gani ...?!!!

Tunapo tizama moja ya maana ya majina hayo yaaniJesus/Yesu/Yeshua/Messiah/Kristo ni “Mpakwa Mafuta”. Kwa maneno mengine Kristo ni mtu mwenye upako, mtu aliye pakwa mafuta kama alama ya uteule wake. Leo duniani kuna wetu wengi wanao jinadi kuwa wanao upako, yaani wamepakwa mafuta, kwa maneno mengine watu hao ni Kristo na au Yesu, na au Yeshua na au Messiah. 

Unaiitaje tena hii? Mi sikumbuki labda geuza kompyuta yako chini juu, juu chini unaweza kuisoma .... lol

Watu hao pia wanafanya mambo ya maajabu, wanaponya watu maradhi mbalimbali, wanawapatia utajiri na kadhalika, yote haya hayana shida, kama mtu kapewa kipawa cha kuweza kufanya hayo si jambo la ajabu, lakini kuna wale wanao dai wanaweza kufufua watu, hili nina mashaka nalo, lakini jambo lililo na utata zaidi ni wao kujipamba na sifa isiyo yao, sifa ya Kristo, ni wazi watu hao wanajiita wao ni Yesu, hata hivyo kuja kwa watu hawa kumeshaelezewa katika vitabu vitakatifu ikiwemo Biblia na hapa si mahala pake na wale ambao wanahisi hili lina wagusa na warejelee vitabu vya dini zao kupata ukweli wa mambo.

Kerry yupo kazini, lakini mbele yake kuna 666

Hivyo namba/alama 666 inayo maana ya Kristo lakini kama tulivyoona mwanzo kuwa namba/ alama hiyo ni jina na ambapo tunapata majina mawili yaani jina la Kristo na Jina la Mpinga Kristo je Freemasons wanamaanisha jina lipi wanapo tumia 666?

Upo Hapo?????

Turudi kwenye lugha ya Kiarameiki ambapo neno Messiah lenye maana ya Kristo ndipo lilipotoka, neno hilo lina maana ya Msema kweli, Msema Uongo, mtu mwenye kasoro, mtu wa  kuzunguka dunia nzima, maana hizo chache zinatosha kutupatia jibu letu. Sifa ya kuwa na Kasoro ni sifa ya Masih Dajjal/ Mpinga Kristo kwani kati ya macho yake mawili moja ni chongo yaani halioni na hii inahusishwa na alama ya jicho moja kwenye nembo za Freemasons. Sifa ya kusema uwongo ni sifa ya Masih Dajjal/ Mpinga Kristo na hii pia ni sifa waliyonayo Freemasons. Sifa ya Kuzunguka dunia nzima nayo ni Sifa ya Masih Dajjal kutokana na mafundisho ya Kiislam ataizunguka dunia nzima kwa siku arobaini tu. 

Hivyo sifa moja inayobakia ya kusema Ukweli hii ni sifa ya Mtume wa Mungu Masihi Issa (Yesu) hivyo moja kwa moja tunapata picha kuwa Freemasons wanapotumia namba/alama 666 wanamaanisha jina gani,Masihi Dajjal/Mpinga Kristo. Jina hilo lipo kwenye shilingi mpya ya Euro, kwenye Bar Code ya bidhaa za Marekani , kwenye nembo za Microsoft  kutaja kwa uchache ila kiuhakika ziko kila kona na kwa njia moja ama nyingine tunazitumia kufanikisha mambo yetu ya kila siku bila kufahamu.

Wale wanao jinadi kuwa wa upako nao hawaunguki katika sifa za mtume wa Mungu Mmoja bali katika sifa za Mpinga Kristo, kama nilivyokwisha elezea kuna ambao wamepatikana wakijibadilisha na kuwa Nyoka, tuna waona wanavyozunguka dunia nzima leo kwa mahubiri yao, kuna wanao dai kuwa wanafufua watu, ni hii ni moja kati ya uwongo mkubwa atakao kuja nao Mpinga Kristo atadai ana fufua watu na atafanya hivyo lakini kiuhakika hatamfufua mtu bali mashetani anao shirikiana nao ndiyo watakao jibadilisha na kuwa katika umbile na sura ya mtu fulani aliyekufa na kudai yeye ndiye mtu huyo aliyefufuka.


Freemasons ni wasimamizi wa mlango, na punde tu au muda kidogo mwenye mlango atasimama mahala pake, naye si mwingine bali ni Dajjal / Mpinga Kristo ambaye  mtume (Rehema na Amani ziwe juu yake) amemtaja kama hivi,

 “Nimewaeleza mengi kuhusu Dajjal kiasi kwamba nahofia mtakuwa hamjamuelewa, Dajjal ni mfupi, vidole vyake ni vipana na mwili wake umejaa nywele, ana jicho moja linaloona na jingine lisiloona ... kama utamuona fahamu kuwa Mungu wako si jicho moja.”


Inajulikana kuwa kabla ya kuja kwake kuna watu wataandaa njia na mazingira ya kuja kwake, mfumo wa kufanya mambo ya watu hao utabeba sifa zote za Dajjal, kwa maneno mengine waandaaji wa njia hiyo si wengine bali ni Freemasons. Jicho moja ni mojawapo ya njia ya kumtambua Dajjal na jicho moja ni moja alama za Freemasons, Dajjal ni muwaji na katili kwa wale watakao mpinga, atakuwa na nguvu ya kuwapa watu aridhi kubwa zaidi au kuiharibu itategemea na jinsi gani watu hao watamfuata, sawasawa na Freemasons wa magharibi kupitia World Bank wanazishikilia na kuzivunja vunja nchi za Dunia ya Tatu kiuchumi kama haziendi na kufanya kulingana na sera zao. IMF na mikopo yake ya ‘maendeleo’ imekuwa kama mitego juu ya nchi hizi inawawekea riba kubwa ambayo daima inazifanya nchi hizo kuinama juu ya kila kitakachosemwa na Freemasons hao ambacho si kingine ila ni sera zinazo za kuporomosha uchumi wao na kuziacha masikini daima watumwa wa kuomba omba.


Njia nyingine ambayo Dajjal ataitumia kuwalazimisha watu wamfuate ni kwa kusambaza maradhi. Atakuwa na uwezo wa kusambaza maradhi na kuyatibu kiusahihi na sawasawa. Kwa kutumia nguvu hiyo atawavuta wengi katika dini yake, dini ya Freemasons au kiuwazi zaidi ni ya kishetani. Tunawaona Freemasons pia wakicheza na maisha ya watu kwa njia kama hii, ushahidi mwingi unaonesha kuwa aina nyingi za virusi wa maradhi mbalimbali ukiwemo UKIMWI vimetengenezwa maabara na baadaye vikatumiwa kwa majaribio kwenye miili ya binaadam. 

Dajjal atawadanganya watu kwa kujitangaza mwenyewe na sifa za Mungu aliyetukuka. Freemasons nao wanatumia kila walilo nalo kuziondoa amri za Mungu kwa kuweka amri zao kama wao ndiyo Mungu na ndiyo wanao uwezo wakufanya lolote watakalo, wanatumia teknolojia mbayo hawataki watu wajue kuwa wanayo kuyatawala maisha ya watu na kila kitu chao, wanata kuona na kusukia kila unachofanya, wanatumia genetic kuharakisha maumbile na kuyabadilisha kutokana na wanavyo taka wao. Waharibifu hawa hawaoni mipaka na wala hawatambui sheria kwani vyote hivyo ni wao wameviweka.


Kama ilivyo kwenye filamu ya Independence Day, watatujengea mazingira ya kukubali serikali moja chini ya kiongozi mmoja wa kidunia kama njia ya pekee ya kupambana na ‘adui kutoka nje ya dunia’. Watatupatia kiongozi wao huyo kama nembo ya umoja dhidi ya wote wanao pingana na serikali hiyo wakiwemo hao ‘wageni’.


Lakini pia wanaweza kutumia teknolojia yao ya ‘Project Bluebeam’ ....