JE WACHAWI WANAWEZA KUONA MAMBO YATAKAYO TOKEA MBELENI.?
Wachawi wanazo ndumba zenye uwezo wa kuwasaidia kujua mambo yatakayotokea mbeleni, hivyo basi kama kuna hatari yoyote ile inaenda kutokea kesho yake kama vile ajali au shari yoyote ile nakadhalika, wao wanakuwa wameshajua siku moja kabla na hivyo wanakuwa na nafasi ya kuchukua tahadhari mapema.
JINSI WANAVYO FANYA ILI KUWA NA UWEZO WA KUONA MAMBO YATAKAYO TOKEA.
Zipo njia mbalimbali wanazotumia, ili kupata uwezo wa kuona mambo yatakayotokea mbeleni lakini kati ya njia hizo njia ifuatayo ni maarufu sana miongoni mwa wachawi na walozi.
Zipo njia mbalimbali wanazotumia, ili kupata uwezo wa kuona mambo yatakayotokea mbeleni lakini kati ya njia hizo njia ifuatayo ni maarufu sana miongoni mwa wachawi na walozi.
i.Wanachukua ubongo wa fisi
ii.Wanachukua ubongo wa kunguru
iii.Wanachukua ubongo wa ndege anaitwa Mbesi. Ndege huyu hupatikana mtoni na chakula chake kikuu ni mizoga ya ndege, wadudu, samaki na wanyama. Katika ulimwengu wa wachawi, ndege huyu hujulikana kama mtaalamu wa kugundua mahali ilipo mizogo iliyo kufa.
Kwa mfano tuchukulie mkoa wote wa Dar Es Salaam ni pori, huyu ndege yupo mbagala halafu maeneo ya msasani kuna ndege,samaki,wadudu au mnyama amekufa, basi usiku wa siku hiyo ndege huyu ataota mahali ulipo mzoga huo, na kesho yake atapaa moja kwa moja hadi sehemu ulipo mzoga huo na kuufanya kuwa kitoweo chake.
Vitu vyote hivyo hapo juu hukaushwa na kusagwa kwa pamoja na kisha kuchanganywa na ndumba tatu za kichawi ambazo sitazitaja hapa kwa sababu maalumu.Baada ya hapo, mchawi husika atachanjiwa ndumba hizo kichwani pamoja na kwenye zote nne za mwili.Basi, mchawi huyo anakuwa na uwezo wa kuona ndotoni kila kitu kitakacho tokea kesho yake na kuendelea.
SWALI NAMBA MBILI : NASIKIA WATU WANAZUNGUMZA KUHUSU DUDUMIZI. JE DUDUMIZI NI NINI NA ANATUMIKAJE KATIKA UCHAWI ?
JIBU;
Dudumizi ni ndege anaye patikana porini. Katika ukanda wa Pwani, ndege hawa wanapatikana kwa wingi sana katika mapori ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, Kisarawe vijijini ( Hususani katika vijiji vya Mwaneromango, Nzenga na Msanga ) pamoja na wilaya ya Pangani mkoani Tanga.

Ndege hawa wana macho mekundu, mkia mrefu pamoja na kucha ndefu sana.
Dudumizi hula wadudu, mijusi, nyoka, mayai,makinda, matunda, mizoga na wanyama wadogo pia.Dudumizi wengi wana mabawa yenye rangi ya kahawia nyekundu na kichwa cheusi. Lakini pia wapo Dudumizi wenye mkia wa rangi ya shaba, Dudumizi weusi,Dudumizi wenye koo lenye rangi nyeusi, Dudumizi wenye kichwa chenye rangi ya buluu, pamoja na Dudumizi wenye nyushi nyeupe.

MAAJABU YA DUDUMIZI.
Dudumizi ni ndege mwenye maajabu mengi sana, kwa muwa muda hauturuhusu, leo nitataja mawili tu.
AJABU LA KWANZA : Ana uwezo wa kujifungua kamba mwenyewe. Kwa mfano, ukienda kwenye kiota cha Dudumizi, halafu ukawafunga makinda wa Dudumizi kamba kisha ukafunga na kwenye mti. Kesho yake asubuhi unakuta ile kamba imejifungua yenyewe .
Ukimchukua Dudumizi ukampeleka nyumbani kwako, ukamuweka kwenye banda, halafu ukamfunga kamba akiwa bandani, ukafunga banda halafu kamba hiyo ukaenda kuifunga kwenye mti au kitu chochote kile, kesho yake unakuta Dudumizi amefungua hiyo kamba na kuondoka, hata kama kamba hiyo itakuwa kubwa na nzito kwa kiasi gani.

AJABU LA PILI : Kwa kawaida Dudumizi hutaga mayai kati ya mawili hadi matano. Dume la Dudumizi ambalo huwa dogo kwa umbo kuliko jike, ndio linalo hatamia mayai na kutunza makinda.
JINSI WACHAWI WANAVYO MTUMIA NDEGE DUDUMIZI.
Katika ulimwengu wa wachawi, Dudumizi ana matumizi mengi sana kichawi. Leo nitataja mawili tu kwa sababu ya muda.
JINSI WACHAWI WANAVYO MTUMIA NDEGE DUDUMIZI.
Katika ulimwengu wa wachawi, Dudumizi ana matumizi mengi sana kichawi. Leo nitataja mawili tu kwa sababu ya muda.
1.Kamba iliyo tumika kuwafunga Dudumizi na ikajifungua yenyewe, ikichanganya na ndumba za kichawi pmaoja na vizimba vyake, hutumika kuwafungua kichawi, watu walio katika vifungo mbalimbali vya kichawi kama vile vifungo katika biashara, vifungo katika mapenzi na ndoa, vifungo katika rizki , vifungo vya mizimu, nakadhalika.
2.Dudumizi hutumika, kutengeneza ndumba maalumu kwa wale wanawake wanao penda kuwa inamisha waume zao.
SWALI NAMBA TATU: JE NI KWELI KUWA WACHAWI WANA UWEZO WA KUMTIA MTU MIKOSI NA KUFUNGA RIZIKI YAKE?
JIBU;
Ni kweli kabisa,wachawi wana uwezo wa kumtia mtu mikosi . Zipo njia mbalimbali wanazo tumia wachawi katika kuwatia watu mikosi, ila kutokana na ufinyu wa nafasi, nitaelezea moja hapa;
Katika njia hii, wachawi wakitaka kumtia mtu mikosi, hufanya mambo yafuatayo :
i.Wanachukua hela ambayo haitumiki
i.Wanachukua hela ambayo haitumiki
ii.Mavi ya mbwa mweusi ambayo ameyanya usiku
iii.Mkaa ulio kwisha tumika, ambao umetumika mahali ambapo watu hawalali kama vile kilioni au kwenye bara na migawaha inayo kesha lakini mara nyingi, huchukua mkaa wa kilioni.
iv.Mavi ya ndege anaitwa Mumbi. Huyu ndege aitwae Mumbi anapatikana porini. Anafanana sana na bata na ana puyanga la rangi nyekundu.
v.Shahidi la kaburini pamoja na ndumba zingine za kichawi
vi.Kitu chochote cha mtu aliye kusudiwa kutiwa mikosi kama vile picha yake, mchanga alipokanyagia, mate, kucha, au chochote kile.Baada ya hapo, mchawi huyo atakwenda kaburini usiku wa manane na kuvizika vitu vyote nilivyo vieleza hapo juu, huku akisema maneno ya kichawi ambayo siwezi kuyataja hapa. Basi mtu aliye kusudiwa na uchawi huu, kama hana kinga, ata andamwa na mikosi mikubwa na mizito katika maisha yake yote.
SWALI NAMBA NNE : DOKTA, NINAPENDA KUJUA NINI KINGA DHIDI YA UCHAWI? NIFANYE NINI ILI UCHAWI USINIDHURU?
JIBU:
Kama wewe ni Muislamu, uwe mtu wa swala sana, kufanya duwa na visomo ( Ruqiya) na kutoa Dhaka na swadaka kwa mola wako, na kama wewe ni Mkristo, basi uwe mtu wa kusali sana, kufunga na kuomba bila kusahau kutoa sadaka na fungu la kumi kwa Mungu wako.

Lakini kama unajijua, hauwezi kufanya mambo niliyo yataja hapo juu, basi unatakiwa kupata kinga ya mwili wako.Zipo kinga nyingi zenye nguvu dhidi ya uchawi na ulozi. Zipo Kinga, mchawi akikutupia uchawi unamrudia mwenyewe ana kufa papo hapo au anapooza kwanza kwa muda mrefu kisha anakufa pia zipo kinga ambazo mchawi, akitaka kukutupia uchawi, anashindwa kukuona katika rada zake za kichawi.Hii ni kinga muhimu sana na haiishii kukukinga mwili wako pekee.Inakinga nyumba, biashara, kiti cha ofisi nakadhalika.
KINGA HII HUJULIKANA, KAMA KINGA YA KUFICHA KIVULI CHAKO.
Inaitwa Kinga ya Kuficha kivuli, kwa sababu wachawi wanapo taka kumloga mtu, huchukua na hushambulia kivuli chake. ( HAPA SIZUNGUMZII KIVULI CHA JUANI, NAZUNGUMZIA KIVULI CHAKO CHA KIROHO, YAANI NAFSI YAKO )Bila kuona kivuli chako, wachawi hawawezi kukuloga.
Kinga hii hukupa uwezo wa kutokuonekana kwenye rada za wachawi. Kwao unakuwa ni sawa na mtu aliye kufa tu, kwa sababu mtu aliye kufa kivuli chake hakionekani na pia hawezi kurogwa na uchawi wa aina yoyote ile.