Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatatu, 7 Novemba 2016

JE UNASUMBULIWA NA MATATIZO YA NGUVU ZA KIUME NA UUME WAKO HAUNA NGUVU YA KUSIMAMA VIZURI?PATA TIBA YA BURE SASA

Image may contain: one or more people and text
1. Kitunguu swaumu
Kitunguu Swaumu
Chukuwa punje 10 mpaka 15 za kitunguu swaumu, menya na uzikate vipande vidogo vidogo kisha meza na maji vikombe 2 kutwa mara 2 kwa mwezi mmoja.

2. Tikiti maji
TikitiMaji
Kula tikiti maji kila siku huku ukitafuna na zile mbegu zake, fanya hivi siku zote.

3. Ugali wa dona
Ugali wa Dona
Kula ugali wa dona kila siku. Ni mhimu kuachana na mazoea ya kula ugali wa sembe. Ugali wa dona una virutubisho vingi na mhimu kwa ajili ya afya ya mwanaume. Kama ugali wa dona unakukera jaribu kufanya hivi, chukuwa mahindi kilo 10 ongeza ngano kilo 3 na usage kwa pamoja, ugali wake huwa ni mlaini, mzuri na mtamu na unaweza kula na mboga yoyote tofauti na lile dona la mahindi peke yake. Fanya hivi katika familia yako kwa maisha yako yote.
4. Chumvi ya mawe
Chumvi ya mawe
Chumvi ya mawe ya baharini ile ambayo haijasafishwa au haijapita kiwandani ina mchango mkubwa sana katika kutibu tatizo hili. Tumia chumvi hii kwenye vyakula vyako kila siku.

5. Maji ya kunywa
Maji ni Uhai
Kunywa maji ya kutosha kila siku bila kusubiri kiu. Kila mtu anahitaji glasi 8 mpaka 10 za maji kila siku. Maji ni mhimu katika kuongeza damu, kusafisha mwili na kuondoa sumu mwilini.

6. Mbegu za maboga
Mbegu za Maboga
Ziloweke katika maji yenye chumvi, zikaushe. Zikaange kidogo bila kuziunguza. Tafuna mbegu 30 kutwa mara 3 kwa muda wa mwezi mmoja. Mbegu hizi sifa yake kubwa ni kuongeza wingi wa mbegu za kiume (manii), kama unatatizo la kuwa unatoa manii machache (low sperm count) basi hii ni mhimu sana kwako.

7. Asali na Mdalasini
Asali & Mdalasini
Chukuwa lita moja ya asali safi ya asili ambayo haijachakachuliwa, ongeza vijiko vikubwa 4 vya mdalasini ya unga changanya vizuri pamoja. Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila unapoenda kulala. Fanya hivi kwa mwezi mmoja.

8. Unga unga wa udishe
Unga wa Udishe
Unga unga wa mti wa udishe ni mzuri sana katika kutibu tatizo la nguvu za kiume na pia unasaidia sana kwa wanaume wenye tatizo la nguvu za kiume lililosababishwa na kujichua au kupiga punyeto kwani huimarisha sana mishipa ya uume. Kuna matangazo mengi juu ya mitishamba inayoweza kutibu tatizo hili lakini naweza kukuhakikishia kuwa mti huu kweli unafanya kazi, utakupa nguvu sana hata kwa watu wenye umri mkubwa sana. Pia unaweza kuutumia hata kama unasumbuliwa na tatizo la kisukari pia unao uwezo mkubwa katika kuongeza hamu ya tendo la ndoa hata kwa kina mama. Chemsha maji nusu lita ongeza kijiko kidogo cha chai cha unga huu, unaweza kuongeza pia asali vijiko viwili na unywe kama chai kutwa mara 2. 
Kwa maswali, ushauri au tiba
0764 995259 whatsapp