Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumanne, 29 Novemba 2016

MASWALI YANAYOULIZWA SANA KUHUSU WACHAWI NA UCHAWI WAO


Image result for wachawi wakamatwaJE WACHAWI WANAWEZA KUONA MAMBO YATAKAYO TOKEA MBELENI.?

Wachawi wanazo ndumba zenye uwezo wa kuwasaidia kujua mambo yatakayotokea mbeleni, hivyo basi kama kuna hatari yoyote ile inaenda kutokea kesho yake kama vile ajali au shari yoyote ile nakadhalika, wao wanakuwa wameshajua siku moja kabla na hivyo wanakuwa na nafasi ya kuchukua tahadhari mapema.
JINSI WANAVYO FANYA ILI KUWA NA UWEZO WA KUONA MAMBO YATAKAYO TOKEA.
Zipo njia mbalimbali wanazotumia, ili kupata uwezo wa kuona mambo yatakayotokea mbeleni lakini kati ya njia hizo njia ifuatayo ni maarufu sana miongoni mwa wachawi na walozi.
i.Wanachukua ubongo wa fisi
ii.Wanachukua ubongo wa kunguru
iii.Wanachukua ubongo wa ndege anaitwa Mbesi. Ndege huyu hupatikana mtoni na chakula chake kikuu ni mizoga ya ndege, wadudu, samaki na wanyama. Katika ulimwengu wa wachawi, ndege huyu hujulikana kama mtaalamu wa kugundua mahali ilipo mizogo iliyo kufa.
Kwa mfano tuchukulie mkoa wote wa Dar Es Salaam ni pori, huyu ndege yupo mbagala halafu maeneo ya msasani kuna ndege,samaki,wadudu au mnyama amekufa, basi usiku wa siku hiyo ndege huyu ataota mahali ulipo mzoga huo, na kesho yake atapaa moja kwa moja hadi sehemu ulipo mzoga huo na kuufanya kuwa kitoweo chake.
Vitu vyote hivyo hapo juu hukaushwa na kusagwa kwa pamoja na kisha kuchanganywa na ndumba tatu za kichawi ambazo sitazitaja hapa kwa sababu maalumu.Baada ya hapo, mchawi husika atachanjiwa ndumba hizo kichwani pamoja na kwenye zote nne za mwili.Basi, mchawi huyo anakuwa na uwezo wa kuona ndotoni kila kitu kitakacho tokea kesho yake na kuendelea.
SWALI NAMBA MBILI : NASIKIA WATU WANAZUNGUMZA KUHUSU DUDUMIZI. JE DUDUMIZI NI NINI NA ANATUMIKAJE KATIKA UCHAWI ?
JIBU;
Dudumizi ni ndege anaye patikana porini. Katika ukanda wa Pwani, ndege hawa wanapatikana kwa wingi sana katika mapori ya Bagamoyo mkoa wa Pwani, Kisarawe vijijini ( Hususani katika vijiji vya Mwaneromango, Nzenga na Msanga ) pamoja na wilaya ya Pangani mkoani Tanga.
Ndege hawa wana macho mekundu, mkia mrefu pamoja na kucha ndefu sana.
Dudumizi hula wadudu, mijusi, nyoka, mayai,makinda, matunda, mizoga na wanyama wadogo pia.Dudumizi wengi wana mabawa yenye rangi ya kahawia nyekundu na kichwa cheusi. Lakini pia wapo Dudumizi wenye mkia wa rangi ya shaba, Dudumizi weusi,Dudumizi wenye koo lenye rangi nyeusi, Dudumizi wenye kichwa chenye rangi ya buluu, pamoja na Dudumizi wenye nyusi nyeupe.
MAAJABU YA DUDUMIZI.
Dudumizi ni ndege mwenye maajabu mengi sana, kwa muwa muda hauturuhusu, leo nitataja mawili tu.
AJABU LA KWANZA : Ana uwezo wa kujifungua kamba mwenyewe. Kwa mfano, ukienda kwenye kiota cha Dudumizi, halafu ukawafunga makinda wa Dudumizi kamba kisha ukafunga na kwenye mti. Kesho yake asubuhi unakuta ile kamba imejifungua yenyewe .
Ukimchukua Dudumizi ukampeleka nyumbani kwako, ukamuweka kwenye banda, halafu ukamfunga kamba akiwa bandani, ukafunga banda halafu kamba hiyo ukaenda kuifunga kwenye mti au kitu chochote kile, kesho yake unakuta Dudumizi amefungua hiyo kamba na kuondoka, hata kama kamba hiyo itakuwa kubwa na nzito kwa kiasi gani.
AJABU LA PILI : Kwa kawaida Dudumizi hutaga mayai kati ya mawili hadi matano. Dume la Dudumizi ambalo huwa dogo kwa umbo kuliko jike, ndio linalohatamia mayai na kutunza makinda.
JINSI WACHAWI WANAVYO MTUMIA NDEGE DUDUMIZI.
Katika ulimwengu wa wachawi, Dudumizi ana matumizi mengi sana kichawi. Leo nitataja mawili tu kwa sababu ya muda.
1.Kamba iliyo tumika kuwafunga Dudumizi na ikajifungua yenyewe, ikichanganya na ndumba za kichawi pmoja na vizimba vyake, hutumika kuwafungua kichawi, watu walio katika vifungo mbalimbali vya kichawi kama vile vifungo katika biashara, vifungo katika mapenzi na ndoa, vifungo katika rizki , vifungo vya mizimu, nakadhalika.
2.Dudumizi hutumika, kutengeneza ndumba maalumu kwa wale wanawake wanao penda kuwa inamisha waume zao.(Limbwata