PUNDA
Punda ni wakali na wachangamfu, wenye hisia na wanaoweza kujieleza wakiwa na ari ya kufanya chochote. “SASA HIVI” hayo ndio mambo wanayotaka kusikia.
Ni watu wasiokuwa na subira, kila kitu kinafanyika kwa msukumo na haraka haraka. Ni viongozi majasiri ambao hawaoni karaha kuchukua majukumu, wakati wote wanajiona kwamba “Wanajua sana”.Kwa ujumla wenye nyota ya Punda ni watu wenye mapenzi motomoto, tatizo lao kubwa hawapendi kusikiliza ushauri wa kimapenzi, na hawakubaliani na mambo nusu nusu. Ni watu wenye kutegemea mazuri wakati wote na hawakubali kushindwa. Hupenda kukimbilia katika mapenzi bila kufikiri, wanapohisi wamepata mpenzi wa kweli. Ni wepesi kuvutwa katika mapenzi na ni wenye miamko ya ghafla au misukumo ya kiwazimu ambayo wakati mwingine inawafanya waonekane wapumbavu
MAPACHA
Watu wenye nyota ya Mapacha wanajulikana sana kwa hadhi yao ya kuwa na sura mbili. Kuna wakati wanakuwa na hisia tofauti na muda si muda wamebadilika.
Pamoja na kwamba hawapendi kubanwa sana , ni watu wachamgamfu na wenye mahaba mazuri.
Ni watu wenye asili ya mawasiliano na ni vigumu sana kuwafanya wajinga hivyo basi wakishampenda mtu wanahakikisha kwamba hawamchoshi huyo mpenzi. Watatumia muda mrefu kuzungumza maneno mazuri na wapenzi wao ili kuhakikisha kuwa uhusiano unazidi kuwepo.
Katika mapenzi, wao wanapenda vitu tofauti tofauti na wanahisi wamechoshwa basi huwa wa kwanza kuondoka aidha kwa muda au moja kwa moja.
Uaminifu ni kitu kigumu kwa watu wenye nyota hii na wanahisi kwamba kuna kitu wanakikosa nje hivyo basi wanatoka sana nje hata kama wakiwa wana ndoa yenye furaha.
Wengi wao wanafikia hatua ya kuishi maisha ya sehemu mbili; mke na bwana au bwana na mke.
0653 532036 whatsapp
0764 995259
tibazetutz@gmail.com
Watu wenye nyota ya Mapacha wanajulikana sana kwa hadhi yao ya kuwa na sura mbili. Kuna wakati wanakuwa na hisia tofauti na muda si muda wamebadilika.
Pamoja na kwamba hawapendi kubanwa sana , ni watu wachamgamfu na wenye mahaba mazuri.
Ni watu wenye asili ya mawasiliano na ni vigumu sana kuwafanya wajinga hivyo basi wakishampenda mtu wanahakikisha kwamba hawamchoshi huyo mpenzi. Watatumia muda mrefu kuzungumza maneno mazuri na wapenzi wao ili kuhakikisha kuwa uhusiano unazidi kuwepo.
Katika mapenzi, wao wanapenda vitu tofauti tofauti na wanahisi wamechoshwa basi huwa wa kwanza kuondoka aidha kwa muda au moja kwa moja.
Uaminifu ni kitu kigumu kwa watu wenye nyota hii na wanahisi kwamba kuna kitu wanakikosa nje hivyo basi wanatoka sana nje hata kama wakiwa wana ndoa yenye furaha.
Wengi wao wanafikia hatua ya kuishi maisha ya sehemu mbili; mke na bwana au bwana na mke.
0653 532036 whatsapp
0764 995259
tibazetutz@gmail.com
KAA
Hisia ni kitu muhimu sana katika mapenzi kwa wenye nyota hii pamoja na kwamba kimaumbile ni watu wanapenda kujilinda na wanaogopa sana kuumizwa kimapenzi na wapenzi wao.
Wanapenda sana kuwa karibu na wanayempenda na kuwaonyesha huba na upendo mkubwa. Kwao hakuna mapenzi ya nusu nusu na wanapenda sana kuwa na mtu ambaye atadumu nae milele.
Wenye Nyota hii bila ya kuwa na mpenzi hujihisi hawajatimiza lengo lao katika maisha hivyo basi huwa hawana raha.
Ni wapenzi waaminifu na wanategemea wapenzi nao wawe waaminifu kama wao.
Ni wagumu sana kuachana na wapenzi na inapotokea huwa hawaagi wako radhi wao waumie kuliko kuachana na anayempenda.
SIMBA
Wanapenda sana kuwa karibu na wanayempenda na kuwaonyesha huba na upendo mkubwa. Kwao hakuna mapenzi ya nusu nusu na wanapenda sana kuwa na mtu ambaye atadumu nae milele.
Wenye Nyota hii bila ya kuwa na mpenzi hujihisi hawajatimiza lengo lao katika maisha hivyo basi huwa hawana raha.
Ni wapenzi waaminifu na wanategemea wapenzi nao wawe waaminifu kama wao.
Ni wagumu sana kuachana na wapenzi na inapotokea huwa hawaagi wako radhi wao waumie kuliko kuachana na anayempenda.
SIMBA
Tabia ya Simba ni kujitanua, Ukarimu na ulezi ikichanganyika na ujeuri na kujionyesha, huwaharibu wale wanao wapenda.
Furaha haina mpaka katika mapenzi ya simba, mioyo yao mikubwa na hisia zao nzito hutokeza dhahiri wanapompenda mtu.
Baada ya hapo ndipo sura kamili ya Simba hujitokeza. Wao wanathamini sana mapenzi na juu ya jambo lolote, na wanaweza kuwa waaminifu sana na wakati mwingine huwaabudu wapenzi wao.
Wanapenda kujishughulisha sana na mambao ya mapenzi lakini mambo yakiharibika basi inakua vigumu sana kuyatengeneza.
Tatizo lao kubwa ni wao kujisahau kwamba ni upande mmoja wa penzi na wanajifanya wao ndio viongozi.
Kwa nje wanaonekana ni wenye kujiamini katika mapenzi lakini kwa ndani wanaweza kuwa wanaumia lakini hawawezi kukubali. Hata hivyo mara nyingi hutegemea kupata hisia kama walizonazo wao kutoka kwa wapenzi wao.
MASHUKE
Pamoja na kwamba wanaonekana ni watu wenye aibu kwa undani na kujiamini, wenye nyota hii hupumzika na kunawiri wanapokuwa katika mapenzi.
Ni watu ambao inawawia vigumu kuonyesha penzi lao. wana mtizamo wa kufikiri kabla ya kujitumbukiza ndani ya penzi lolote, wanachunguza kwa makini matokeo ya penzi lenyewe.
Wanapotafuta mpenzi wanaweza wakakupumbaza na maneno matamu na raha zisizo na kifani. Ni vizuri kufikiria mara mbili kabla hujajiingiza katika mapenzi na Mashuke.
Inawawia vigumu wao kukuanza wewe kimapenzi kwa sababu wana uhakika kwamba watashindwa.
Kinachowasaidia ni subira na kuwaelewa wapenzi wao ndio maana mapenzi yanakua.
Mara wakishapata mpenzi wa kweli wanakuwa waaminifu sana na watafanya kila njia kuhakikisha mapenzi yanakuwa hai na yenye kupendeza.
Hata hivyo wanaweza kuwa wasumbufu, wenye kulalamika na wenye mtizamo wa makosa ya mpenzi wake ili amshutumu.
Kwa sababu ya hali yao hii mara kwa mara kunakuwa na ugomvi wa wapenzi ambao wanataka kutekeleza malengo yao.
MIZANI
Kujihusisha na suala la mapenzi kwa wenye nyota hii ni kitu cha kawaida kabisa pamoja na kwamba wenye nyota hii wanachukua muda mrefu kufanya maamuzi na inawawia vigumu sana kuchagua kati ya wapenzi wawili yupi anaefaa. Kwao kuishi vizuri ni kuwa na mpenzi au uhusiano wa kimapenzi.
Watu wa mizani wanathamini sana mapenzi kuliko hata maisha yao wenyewe na wanapenda sana kujionyesha kwamba wanapendwa.
Kwa sababu hizo wengi sana wanapumbazwa na mapenzi na ndoa zao zinakuwa zina matatizo na zisizo na raha kwa sababu ya kuoa mapema bila kuangalia. Wenye nyota hii wanaonelea bora kuishi katika ndoa yenye matatizo kuliko kuishi peke yao.
Katika suala la mahaba (Romance) na ngono (Sex) wao ni mabingwa. Wanajua sana kumpendeza mwanamke kwa maneneo matamu yenye mpangilio na zawadi za thamani na wawapo kitandani wanatumia muda mrefu kuwachezea wapenzi wao sehemu nyeti.
Kwa ujumla wenye nyota ya Mizani wanapenda kuishi vizuri na wanapenda wapenzi wao nao waishi katika hali nzuri.
NGE
Watu wenye nyota ya Nge wanapenda sana kutumia fursa ya kufanya mapenzi kama njia mojawapo ya kuonyesha ujasiri wao katika mapenzi na namna wanavyojua kufanya tendo la ndoa.
Ni watu wenye ashki na hasira wakiwa wamedhalilishwa au wameumizwa na wapenzi wao na wanapofanya tendo la ndoa hasira zao huisha mara moja.
Ni watu wasiri sana katika masuala ya mapenzi na wanakuwa hivyo ili waweze kuwapata wapenzi wengi kukidhi matakwa au kiu yao kubwa ya ngono.
MSHALE
Pamoja na kwamba wenye nyota hii wanapenda wawe huru na wenye kujiamulia mambo yao wenyewe huwa wana starehe na kuona raha wanapokuwa ndani ya uhusiano wa kimapenzi.
Wenye nyota hii wanapenda sana kujihusisha na makundi makundi lakini huwa wanapata muda wa kuwa na wapenzi wao. Ni watu wachangamfu na wenye kupenda lakini tabia yao ya kutojali inawafanya wapenzi wao wajione kwamba wanakosa ulinzi wa kimapenzi.
Wanapoingia katika mapenzi wanakuwa waaminifu. Mwanzoni wanakuwa wagumu sana kujihusisha. Wanapenda sana wakati wote kuwa na wapenzi wapya au mapenzi ya kawaida kwa sababu wanaamini mapenzi ya kudumu yanawanyima uhuru.
Wapenzi wao wanaponyesha dalili ya kuwapenda basi wao huwa wanajiondoa kwa hofu ya kubanwa na kutokuwa na uhuru.
Ni watu wanaopenda kufanya ngono kwa muda mrefu na hisia zao ziko mbali na inashauriwa kwamba wapenzi wao wawe wamekula kabla ya tendo la ndoa vinginevyo itakuwa taabu.
MBUZI
Ni watu wanaoogopa sana kuachwa na wapenzi wao hivyo basi huwa wanakuwa waangalifu sana katika kuchagua wapenzi.
Jambo jingine ni kuwa huwa wao wenyewe hawajiamini kimapenzi, mara nyingi wanashindwa kuingia katika mapenzi kwa woga tu hivyo kukosa nafasi nzuri ya kupendwa.
Kwa ujumla ni wapenzi makini na huwa hawaoi mpaka wapate uhakika wa kutosha kutoka kwa wapenzi wao. Ni wapenzi makini, waaminifu na wanaoweza kuaminiwa. Lengo lao katika mapenzi ni usalama.
NDOO
Wenye nyota ya Ndoo ni watu wanaopenda uhuru na hawawezi kabisa kukubali kudhibitwa katika mapenzi, mawazo yao na miono yao inaweza kubadilika mara moja na kuwa wakaidi na wasumbufu. Pamoja na kwamba ni waaminifu na wanatoa msaada mkubwa kwa wapenzi wao.
Wako tayari kutulia katika mapenzi iwapo watahakikishiwa uhuru wao na haki ya kutoingiliwa katika mambo binafsi. Niwa watu ambao hawapendi kuonyesha hisia zao halisi na wanachukua muda mrefu kuingia kikamilifu katika uhusiano wa kimapenzi.
Mara nyingi inakuwa vigumu kwao kuwaamini wapenzi wao lakini wakisha waamini wanakuwa waaminifu.
Ni watu ambao wenye kusema mambo bila kuficha na mara nyingi hawaeleweki kwa wapenzi wao.
Katika ngono kwa sababu ya kupenda uhuru huwa wanapenda kufanya mambo wanavyotaka wao na hawakubali kuingiliwa.
Wakati mwingine hushindwa kuelewa hisia za wapenzi wao jambo ambalo linawafanya wapenzi wao washindwe kuwaelewa.
SAMAKI
Wenye nyota ya Samaki ni wenye kukamilika na Mahaba mengi na wanapenda sana kujitumbukiza na kuzama kwenye dimbwi la mapenzi.
Kuwa katika mapenzi ni kitu wanachokipenda na kukifurahia sana. Ni waangalifu wazuri kwa wapenzi wao wana huruma nyingi.
Ni watu wenye hisia kali za kimapenzi na ni wepesi kuathirika.
Mara nyingi huwa waoga wa vitu vya kimapenzi kwa sababu ya kuogopa kuvurugika kwa mipango yao ya baadaye.
Ni watu wenye kuyachukulia mapenzi kama ua la waridi na wanawaona wapenzi wao kama binaadamu wasio wa kawaida.
Tatizo lao kubwa la kimapenzi ni kwamba wanawaamini sana wapenzi wao na wanakuwa na mawazo au firika za kimapenzi ambazo hazipo katika dunia hii.
Kwa ujumla wenye nyota hii wanapokuwa katika mapenzi wanakuwa wamejawa na shauku na mifano ya kuvutia na wanapenda wapenzi wao waishi kiroho. Mategemeo yao yanakuwa makubwa na yasipotimia huwa wanavunjika moyo.