Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatatu, 28 Desemba 2015

JINSI YA KUMTOA MTU UCHAWI WA ZONGO



Zongo ni aina ya uchawi wa kijinga na mwepesi kabisaaa kufanyiwa,uchawi huu hupendwa sana na wachawi wa mikoa ya Tanga na morogoro sehemu za Turiani na baadhi ya sehemu za mombasa,yaani huku uchawi huu ndiyo nyumbani kwao.

Wachawi wafanyaji wa uchawi huu huweza kukuathiri kwa kukuangalia tuu usoni na kukuminyia jicho utavimba tumbo na kuumwa sana au akaangalia chakula chako na akakibinyia jicho kama kipo jikoni hakiivi abadan hata kikae kutwa nzima jikoni na hata watakaokula wataumwa sana matumbo na kuvimbiwa wakati mwingine hadi kupelekea kifo,wakati huo ni lazima mchawi huyo awe ana hirizi ameivaa mwilini mwake sehemu za mabega,kiunoni au popote mwilini mwake  wakati anakuangalia na kukuminyia jicho au kukiminyia jicho chakula chako anapeleka mkono na kuiminya hiyo hirizi basi hapo athari zake zinakuvaa faster km upepo

Pia wanautumia uchawi huu katika kuyaroga hata mazao yaliyopo shambani yasiweze kukua na kustawi vyema au kama umeanika mahindi ,mpunga au zao lolote akipita mchawi wa aina hii ya uchawi na akakipiga zongo utakuta kimeoza ghafla na wadudu wamejaa

Nilipotembelea kijiji cha njungwa niliweza ona jinsi wazee wa kule uchawi huu walivyofanya ni kitu cha kawaida mpaka kufikia wanafanya mashindano kutupiana kwenye pombe wakati wapo kilabuni wanakunywa na kucheka yaani kama mchezo vilee.

Wana kawaida pia za kutumiana uchawi wa bundi mtu sana sana ukiwa ni mgeni unakaribishwa kwa style hiyo hata mm pia nilikutana na hiyo hali..turudi kwenye mada yetu

JINSI YA KUMTOA MTU UCHAWI WA ZONGO
Dalili za aliyepigwa zongo
~Kujaa tumbo
~Kupumua kwa shida
~Kukosa choo
~Kuumwa sana tumbo na ukienda chooni unatoa upepo tuu na hupati choo
Ikiwa wamekupata fanya hivi.

Vijiwe vidogo7 na yai 1

Tia maji safi kwenye sifuria au bakuri na hvyo vijiwe

Pasua yai kwa kulifikichafikicha kwenye maji hayo na livuruge mpaka upate povu

Chota kidogo anywe na.yanayobaki mpige nayo tumboni mara7 na umzungushie vijiwe hivyo tumboni kimoja baada ya kingine

Dawa itakayobaki imwage muache akalale ameshapona....


Ally chambas 
0653 532036
0764 995259