Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatatu, 7 Desemba 2015

JINSI YA KUONDOA MATATIZO YA KUNUKA KIKWAPA


Kikwapa  ni  tatizo la kutoa harufu mbaya  sehemu ya kwapani katika mwili wa binadamu. Tatizo hili husababishwa na bakteria wanaovutiwa na unyevunyevu  chini ya kwapa unaosababishwa na jasho au kuwa na manywele mengi sehemu hizo pasipo kunyoa.

Tatizo la Kikwapa ni kero kwa sababu husababisha mtu kutoa harufu mbaya inayokuwa kero kwake na kwa mtu mwingine aliyeko jirani yake.

Basi kama na wewe ni mmojawapo kati ya watu wanaosumbuliwa na matatizo haya ya kunuka kikwapa tumia dawa hizi hali hiyo itakuondokea 

~habbat sawda 
~habbat sufaa 
~sandali   

hakikisha dawa zote ziwe za unga,unaweza pia kuzisaga ili ziwe unga

pima vijiko viwili vikubwa kwa kila dawa  

 changanya pamoja na ukamulie ndimu 3 na utie mchanganyiko huo kwenye mafuta ya zaituni kiasi cha ml250 

utatumia dawa hyo kwa kujisugulia kwapani kwa kutumia pamba asubuhi na jioni kila unapotoka kuoga kwa muda wa wiki 2