Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatatu, 28 Desemba 2015

TAFSIRI NDOTO ZAKO MWENYEWE [SEHEMU YA PILI]

Habari zenu wapendwa 
kama tulivyopata kuona tafsiri za ndoto zetu mbalimbali katika sehemu ya kwanza ya mada hii basi leo tunaangalia tena muendelezo wa mada yetu inayosema tafsiri ndoto zako mwenyewe,tuungane pamoja in shaa Allah


 UKIOTA MTU ALIYEKUFA ANASWALI
Ni ishara ya kuwa mtu huyo ambaye ni marehemu zimemfikia thawabu za matendo yake aliyokuwa akiyachuma duniani enzi za uhai wake au thawabu za vitu alivyotoa sadaka kwa ajili ya mungu.


KUOTA ALIYEKUFA ANAKUAMBIA UTAKUFA
Wakati mwingine kauli yake huwa ni kweli,


KUOTA MLANGO UNAANGUKA
Muotaji ataugua kwanza halafu atapona


UKIOTA UNAFUNGA MLANGO WA NYUMBA YAKO
Utampa talaka mke wako


UKIUOTA MSUMARI AU DARAJA
Humaanisha mtu anayesaidia watu katika kutatua matatzo yao  


KUPANDA NGAZI,MBAO AU MOTA
Utapata hadhi kubwa duniani[cheo]kama katika ndoto kutakuwa na jambo la kuhashiria hali hii


KUOTA NYUMBA YAKO IMETEKETEZWA
Utasumbuliwa na wenye mamlaka au ugonjwa wa mlipuko


KUOTA MTU ALIYEKUFA ANAKUPA MAWAIDHA AU ANAKUFUNDISHA
Utapata wema katika dini yako kwa kiasi cha mawaidha yale


KUOTA UNAMUOA MWANAMKE ALIYEKUFA 
unamuona kuwa yuko hai lakini kiuhalisia ameshakufa unamuoa na kuondoka nae ni ishara ya kuwa utafanya jambo litakalokufanya ujute


KUOTA UNAFUFULIWA 
uwe peke yako au na wengine ni ishara ya kuwa wewe ni dhwaalimu


KUOTA UMEINGIA JEHANNAM
Utafanya uchafu na madhambi makubwa,na kama umeota umeingizwa motoni basi yule atakayekuingiza atakupoteza na kukupelekea kwenye mambo machafu


 KUMUOTA JINI USINGIZINI
Ukimuona jini usingizini amesimama karibu na nyumba yako inakujulisha moja kati ya mambo matatu
1.udhalili[unyonge]
2.hasara
3.au nadhiri uliyoiweka 


UKIOTA MAJINI UNAWAONA WAMEINGIA NYUMBANI KWAKO NA KUFANYA MAMBO
Wezi wataingia nyumbani kwako na kukudhuru au maadui zako watavamia nyumba yako 


KUMUOTA MSICHANA AMEJIPAMBA KIISLAM
Utaskia habari zitakazokufurahisha katika njia ambayo hukuitegemea 

  
UKIMUOTA MSICHANA YUPO UCHI
Utapata hasara katika biashara zako


UKIOTA UNACHIMBA KABURI
Pia humaanisha utajenga nyumba


KUUOTA UKUTA
Kama utasimama juu ya kilele ni hadhi na nafasi yako kama utaporomoka utakuwa ni kiongozi wa uharibifu


 KUUZA NYUMBA
Kufikia kikomo cha maisha yake


 KUBEBA MLIMA
 Utabebebshwa mizigo mikubwa na watu wakorofi na wakali

 KUOTA UNAPANDA KUELEKEA SEHEMU YA JUU
Muotaji atapata heshima,atatukuzwa na kupanda cheo


KUOTA MIAMBA NA MAWE
Ugumu wa moyo,ukorofi,ukatili na kibri


 KUOTA CHANGARAWE
Usengenyaji na kutoa shutuma dhidi ya mtu fulani


KUOTA MCHANGA,VUMBI AU UDONGO UNAKURUKIA AU ANAKULA
Utakuwa tajiri jitume sana katika kazi zako


UNATEMBEA JUU YA MCHANGA AU KUOKOTA MCHANGA
Utafanya kazi ngumu za sulubu ili kuwa na mali


MCHANGA AU VUMBI KURUKA HEWANI AU MBINGUNIMambo ya muotaji yatavurugika 


KUMUOTA MTOTO WA KIUME
Ni adui dhaifu ambaye atakujia kwa kudhihirisha urafiki kisha atadhihirisha uadui wake


UKIOTA KWENU KUMEZALIWA WATOTO WENGI WA KIUME
Ni dalili ya majonzi na huzuni


 KUMUOTA BIBI KIZEE
Akiwa amejipamba na amaejifunua~utapata dunia yako na biashara za haraka
Amekunja uso~kuondoka kwa darja ya juu kwa mambo yako ya kidunia 
Ana sura mbaya~mambo yako yatageuka
yupo uchii~ ni dalili ya kufedheheka


UKIOTA USO WAKO NI MWEUSI KULIKO SEHEMU ZINGINE ZA MWILI
Mkeo atazaa mtot wa kike


KUOTA UMEKATWA SHINGO  KWA UPANGA
Kichwa chako kimetengana na mwili ni ishara ya kuwa kama mgonjwa utapona,una deni utalipa,utahiji,kama una vita utapata faraja.kama unamjua aliyekukata hivyo vyote vitapitia kwake


MWANAMKE KUOTA UMENYOLEWA
 Ni ishara ya kifo au utaachwa  


MWANAMKE AKIOTA AMENYOLEWA NA MUMEWE
Mumewe atamfungia nyumbani kwake kwani hakika ndege hubakia kiotani wakati amenyonyolewa mbawa zake 


UKIOTA UNASIKILIZA KWA MACHO NA KUONA KWA MASIKIO
Utampelekea binti yako au mkeo kufanya maasi 


UKIOTA KIGANJA CHAKO KINA JICHO AU NYAMA
Utapata mali


 KUANGUKA KISIMANI
Utakumbwa na huzuni na masikitiko mwishowe utapata furaha


 KUZAMA BAHARINI 
Kama maji ni safi ni ishara utazama katika mambo ya utawala na serikali,kama ni maji chumvi na yana taka utapata taabu itakayokusababishia kuangamia 



 Kwa maswali na ushauri usisite 
+255 653 532036
+255 764 995259
tibazetutz@gmail.com

au whatsapp 0653 532036
MUWE NA SIKU NJEMA