Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Alhamisi, 14 Januari 2016

WACHAWI WANAVYOUTUMIA AINA YA UCHAWI UITWAO SIHRUL AAYUNI KUWATIA WATU MARADHI NA KUZINI NAO USIKU


 Uchawi huu ni miongoni mwa aina 410 za uchawi uliosambaa Africa na Dunia nzima kwa ujumla,Uchawi huu ni miongoni mwa uchawi ambao watu wake huutengeneza kwa kutumia miti miwili ambayo ni HANJARI NA FAIJALI.

Mchawi huchukua miti hii miwili baada ya kuwa ameshakusudia kuutengeneza uchawi huu na kisha anaichanganya pamoja na kuanza kuisemea maneno ya kishirikina na kuapiana na mabwana zake wa kishetani ambao ndiyo nyenzo kubwa katika kufanikisha uchawi wa aina yoyote ukamilike na kumuathiri mlengwa.

Baada ya kumaliza kuisemea miti hiyo maneno hayo ambayo si vyema kuyaandika, ghafla utaanza kutoka moshi mzito mweusi kwenye ile miti na hapo mchawi huvua nguo zake na kubakia kama alivyozaliwa na mamake na huuamuru moshi ule umkinge na kumficha,ndipo moshi ule humvaa mchawi huyo  na kuanzia hapo sasa anakuwa hawezi kuonekana kwa macho ya kawaida.

IKIWA AMEKUSUDIA KUMTIA FULANI MARADHI
 ~Ikiwa mchawi amekusudia kumfanya mtu fulani aumwe magonjwa mazito basi huchukua sumu ya kichawi iitwayo TAILLA sumu hii kazi yake ni kutengeneza magonjwa makubwa kama vile UKIMWI,TAYPHOD,KIFUA KIKUU,EBOLA KIPINDUPINDU NK.

~Mchawi anakuja mpaka kwa fulani na anamvizia akiwa kwenye mlo anakuwekea sumu hii na wewe bila kujua utaendelea tuu kula na kuanzia siku hiyo utaanza kuumwa maradhi yaliyokusudiwa yakupate

IKIWA MCHAWI AMEKUSUDIA KUJA KUZINI NA WEWE
~Mchawi anakuja mpaka chumbani kwako ukiwa umelala na mumeo au mkeo[kumbuka ule moshi alioutengeneza kwa miti ile miwili ndyo unaomfanya asionekane kwa msaada wa shetani wake mshirika].Akifika hapo ndani kama ni mchawi mwanamume anataka kumzini mkeo  anakupulizia wewe mwanaume sumu ya kichawi inayoitwa NUNII na mtu akipuliziwa sumu hii hulala fofofo anakulaza chini kisha anapanda na kufanya mapenzi na mkeo huku mkeo akijitahidi kumfurahisha mchawi huyu huku akijua ni mumewe sababu mchawi huyu hujibadilisha na kufanana kabisa na wewe baba mwenye nyumba kwa kila kitu,akimaliza anakurudisha na kuondoka zake.na mchawi akiwa ni mwanamke naye anafanya hivyohvyo na kujisevia kisha anaondoka zake.


ATHARI ZA UCHAWI HUU
~Kuhisi tumbo limejaa na kuhisi maumivu makali tumboni muda mwingi 

~kupoteza nguvu za kiume na kike

~kutopata hamu ya kufanya tendo la ndoa 

~kuota ndoto mbaya za kutisha na ukishtuka mapigo ya moyo kudunda sana

~kuumwa sana mgongo,mbavu,kichwa na kiuno

kama una swali lolote usisite kuniuliza
+255 653 532036
+255 777 145913