~Kuna baadhi ya akina mama wanapotoka kujifungua
katika kipindi kile muhimu cha kunyonyesha huwa
maziwa yanakuwa kidogo sana kiasi cha kutomtosheleza
mtoto
~tatizo hili ni baya kwa sababu mtoto anapozaliwa
anahitaji sana kupata maziwa ya mama ya kutosha kwa
muda usiopungua miezi 6
~maziwa ya mama yana lishe zote zinazohitajika kwa
mtoto na kama mtoto huyu atapata maziwa ya kutosha
basi bila shaka atakuwa ni mwenye afya njema na
watoto wanaopata maziwa kidogo afya zao huwa si
njema sana.
JINSI YA KUONDOA TATIZO HILI
~Kuna njia nyingi za asili katika kuondoa hili tatizo,lakini
kwa leo ntazungumzia njia chache tuu ambazo ni
muhimu zaidi na ndizo zinazojaza haraka maziwa kifuani
kwa mama mwenye mtoto mchanga
SUPU YA NG'OMBE,MBUZI NA KONDOO
~Mwanamama anapotoka kujifungua ni vizuri apate supu
kila asubuhi na ni vizuri zaidi akapata supu ya
kongoro,nyama ya ngombe au supu ya kondoo kwani
supu za namna hii ni tiba nzuri kwa mama mwenye
matatizo ya kutopata maziwa ya kutosha kwa ajili ya
mtoto wake na pia hurejesha nguvu zilizopotea wakati
wa mshikemshike wa kujifungua.
NDIZI ZA KUCHEMSHA
~Pia ndizi za kuchemsha ni nzuri sana kwa kuondoa hili
tatizo la kukosa maziwa kwa mama
mjamzito,zichemshwe vya kutosha mpaka ziwe laini na
hata mtori pia unafaa katika kutibu hali hyo
MAJI
~Mzazi anapaswa awe ni mwenye kujitahidi kunywa maji
ya kutosha kila siku kwani nayo humsaidia kuongeza
maziwa kwa ajili ya mwanae mpya,pia mzazi kukandwa
maji ya moto sehemu za siri si chini ya wiki moja ni
vizuri zaidi kwani humsaidia kupata nguvu na kuufanya
uke hurudi katika hali ya kawaida kwa muda mfupi.
UJI WA PILIPILI MTAMA
~Aidha mzazi anashauriuwa anywe uji wenye pilipili
mtama na sio pilipili hizi za chachandu,kwani pilipili
mtama zina faida mbili kwa mzazi
1.huondoa haraka makovu yaliyotokana na msuguano
wa mtoto tumboni
2.husaidia ongezeko la maziwa ya mama ili yapatikane
ya kutosha kuweza kumnyonyesha mwanae na akapata
afya njema
KWA TIBA NA USHAURI WASILIANA NASI
KWA
0653 532036
AU TUANDIKIE BARUA PEPE
TIBAZETUTZ@GMAIL.COM