Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumanne, 19 Januari 2016

KUKOSA HAMU YA KULA KWA MAMA MJAMZITO

Kuna baadhi ya wanawake wajawazito ambao wamekuwa wanakabiliwa na tatizo la kutojiskia hamu ya kula,jambo hili ni baya sana kwa vile mama mjamzito anahitaji apate chakula cha kutosha ili mwili uweze kufanya kazi zake kiufanisi,anatakiwa pia ale kwa wingi mboga za majani hasa matembele na mchicha  ambayo yanaelezwa kuwa yanaongoza kwa kuongeza damu.

Mwanamke wakati wa kujifungua hupoteza damu nyingi hivyo lazima ale chakula cha kutosha pamoja na mboga za majani na vitoweo kama samaki,nyama nk

Sasa inapotokea mama mjamzito akawa hana hamu ya chakula msimuache tuu na kusema ni mimba inamsumbua bali hili ni tatizo na uzuri ni kwamba kuna njia za asili ambazo zitamfanya awe na hamu ya chakula kwa sana .

1.MAJI YA MACHUNGWA
~Atengeneze juice ya maji ya machungwa kiasi cha lita moja,kisha awe anakunywa glass moja moja kila baada ya muda fulani katika siku hadi itakapomalizika kwani hii itamfanya awe na hamu ya kula vizuri na itakapomtokea tena ile hali ya kutotamani chakula basi na atengeze tena na kutumia kama hapo juu.


2.HABBATSAUDA NA LIMAO
~Dakika kumi kabla ya kutayarishwa kwa chakula chukua kijiko kidogo cha habbatsauda koroga kwenye glass ya maji na weka maji ya limao kiasi cha kijiko kikubwa humo kwenye glass na unywe,baada ya muda mfupi utajiskia njaa kali sana na utatamani msosi usichelewe kufika mezani.

Hapo sasa jitahidi kula chakula cha kutosha zikiwemo mbogamboga nilizozitaja hapo juu pamoja na matunda kama papai bivu,parachichi,nyanya,fenesi,machungwa na aina zingine za matunda yanayoweza kupatikana.