Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumamosi, 23 Januari 2016

JE WAJUA KUWA WACHAWI WANAWEZA KUMBADILISHA MNYAMA KUWA MTU NA MTU KUWA MNYAMA?????

Amani ya Allah iwe juu yenu wapendwa

 karibuni tena katika blog yenu muipendayo,leo nataka niwajuze kuhusu mchezo huu wa kichawi ambao ulianza tangu enzi za nabii Mussa[a.s]na mpaka sasa upo na unaendelea kutumika na wachawi mpaka leo hii.

Enzi hizo Baada ya kuwa wamepita mitume wengi na wengine wengi kuuwawa  ndipo watu waliacha njia ya kumfuata Mwenyez mungu na kuanza kuabudia uchawi,mizimu,mapango,na makaburi ya watu maarufu.Na ikafikia kipindi yule mwenye uchawi mkubwa na maajabu mengi ndyo huabudiwa badala ya Mungu

KISA CHA KWELI CHA MZEE THAALABU
Huyu mzee alikuwa na binti anaitwa US WAANI na ilifikia kipindi alikuja mtu kutaka kumuoa binti huyu na mzee THAALABU akapokea mahari na kumuhaidi bwana yule aje kuoa jumamosi ya kwanza katika mwezi ujao,basi bwana yule akaondoka akiwa na furaha tele akijua kwamba jumamosi ya mwanzo katika mwezi ujao anakuja kumuoa mtoto mzuri US WAANI.

Baada ya kuondoka bwana yule baada tu ya kupita muda mfupi akaja mwanaume mwingine kwa lengo la kutaka kumuoa binti yuleyule[US WAANI],Basi mzee huyu baba yake mtoto wa kike akachukua tena mahari kwa bwana mwingine  na kumuhaidi aje kuoa jumamosi ya kwanza ya mwezi ujao,na bwana huyu akaondoka huku akijua jumamosi ya kwanza mwezi ujao anakuja kuoa bila kujua kuna mwingine kama yeye amefanyiwa hivyo.

Baada ya kuondoka huyu bwana wa pili kwa kuwa binti US WAANI alikuwa ni mtoto mrembo anayevutia kwa muda mfupi tuu akatokea bwana mwingine ambaye naye alikuwa anataka kumuoa.Alipofika kwa baba yake mtoto wa kike kama kawaida yake akachukua mahari ya yule bwana na akamuhaidi aje kuoa jumamosi ya kwanza ya mwezi ujao.Basi imekwenda hivyohivyo mpaka wakafikia wanaume7 ambao amechukua mahari zao na kila moja amemuhaidi aje kuoa jumamosi ya kwanza ya mwezi ujao na kila mmoja kwa wakati wake anafanya maandalizi bila kujua kama wapo7.

Waswahili wanasema usiku wa mdaiwa huwa mfupi na haya ndyo yaliyomkuta Mzee THAALABU kwani mpaka anashtuka imebaki siku moja tuu,kila mtu katika wale watu 7 aliokula mahari zao wanakuja kuoa naye ana binti mmoja tuu akawa anaumiza kichwa nini afanye na tamaa zimemponza pesa za watu ameshazitumbua zimekwisha.

Akapata wazo la kumtembelea baba yake mzazi yaani babu wa binti yake US WAANI ili aone vipi atasaidiwa kwa maana babu huyu ndiyo alikuwa mchawi mkubwa katika mji wao na ndiye alikuwa anaabudiwa kama Mungu.Basi mzee huyu gwiji la wachawi akamwambia mwanae THAALABU yaani baba wa binti US WAANI amletee watoto 6 wa wanyama hawa
1.mtoto wa punda 2.mtoto wa fisi 3.mtoto wa mbwa mweusi 4.mtoto wa paka mweusi 5.mtoto wa kondoo 6.mtoto wa mbuzi

Basi THAALABU akaondoka kwa babaye na kwenda kutafuta wanyama hao ndani ya saa1 tuu yaani dakika60 tayari alifanikiwa kuwapata wanyama wote na akawaleta kwa baba yake gwiji la wachawi.Basi mchawi huyu akaanza kuchanganya vitu vyake vya kichawi na akambadilisha kila mnyama na kuwa na umbile sawasawa na alivyo binti US WAANI  kuanzia sura,rangi,umbo na kila kitu na mabadiliko haya hufanyika ndani ya dakika 1~3 tu kwa kila mnyama anamuweka pembeni na kumbadili mwingine kwahiyo wanyama wote 6 si zaidi ya dk18 wakawa tayari wamegeuzwa binadamu.

Sasa ilipofika siku ya jumamosi ya kwanza ya mwezi uliofuata yaani siku ya ahadi ya wote kuja kuoa kila mmoja katika mabwana wale kwa muda wake alifika nyumbani kwa mzee THAALABU akakaribishwa ndani na akaozeshwa mtu wake na akaondoka naye bila kujua mchezo uliopo.Hii ni kazi ya shetani na wafuasi wake wachawi wakiwa katika balaa zao ambazo watu wengi hawazijui.

Sasa mzee huyu mwenye mtoto wa kike akawa amechanganyikiwa jinsi gani ataweza kumtambua mtoto wake wa ukweli katika hao watoto 7 maana wote wanafanana kwa kila kitu.basi mzee yule akiwa kwenye mawazo mazito yaliyosababishwa na tamaa yake ya pesa  ghafla akapata jibu kwamba tabia za wanyama ni tofauti na tabia za binadamu hivyo akaamua kutembelea nyumba moja baada ya nyingine ili aweze kumtambua mwanae wa ukweli.

 NYUMBA YA KWANZA

 ~Alipofika baada ya salamu akamuuliza mwanaume ''jee ni kero gani unayoipata kutoka kwa mkeo''??au tatizo gani analo mkeo kwako unaona ni kero''??bwana yule akajibu ''kero ya mke wangu ni kuwa hafui,hapiki wala hafanyi lolote kama sijamtandika bakora''Mzee THAALABU akapata jibu huyu atakuwa ni yule mnyama punda tuliyembadilisha na sio mwanangu wa ukweli''

NYUMBA YA PILI
~Kutoka hapo akaelekea nyumba ya pili na alipofika akamuuliza mwanaume ''jee ni kero gani unayoipata kwa mkeo''akajibu''mke wangu ana tabia mbaya na inanikera kwani akipita kuku,bata,mbuzi au mnyama yeyote wa watu humvamia na kumla''mzee huyu kwa kuwa anajua siri za watu hawa akatambua kuwa huyu si mwanae wa ukweli bali ni mnyama fisi.


NYUMBA YA TATU
~Alipofika nyumba ya tatu akamuuliza mume ''ni kero gani unayoipata kutoka kwa mkeo'' mume akajibu ''muda wote mke wangu ameinamisha kichwa humjui ameshiba wala ana njaa,hashauri baya wala zuri''yule mzee akajua huyu ni mnyama kondoo na sio mwanae wa ukweli

NYUMBA YA NNE
~Alipofika nyumba ya nne pia akamuuliza mume "ni kero gani unayoipata kutoka kwa mkeo''??mume akajibu hakuna hata siku moja utamkuta nyumbani iwe mchana au usiku anazurura ovyo tuu.basi mzee huyu akatambua huyu ni mnyama mbwa na sio mwanae wa ukweli.


NYUMBA YA TANO
~Alipofika akamuuliza mume aliyemuozesha ''hivi ni kero gani unayoipata kutoka kwa mkeo''??mume akajibu''ukifika muda wangu wa kufanya tendo la ndoa yaani kuweza kujilia kile kilichopo chini ya nguo zake basi mke wangu huanza kupiga makelele na kulia kama paka''.Mzee akajua huyu sio mwanangu original bali ni yule mtoto wa paka.


NYUMBA YA SITA
~Akamuuliza mume wa mtoto wake ''ni kero gani unayoipata kutoka kwa huyu mke wako''??mume akajibu baba hazipiti dakika5 ila utaskia zogo la watu kuwa mke wangu amekula vitu vya watu.basi mzee akatambua huyu ni mnyama mbuzi na sio mwanangu wa ukweli.

NYUMBA YA SABA
~Akaenda nyumba ya 7 Mzee THAALABU  pindi alipokaribia kwenye nyumba hii US WAANI akamuona baba yake anakuja akamfuata mbio mbio na kumpokea kwa shangwe na furaha ndipo mzee akatambua huyu ndiyo mtoto wangu wa ukweli.

ILIVYOTOKEA HABARI HII NDIPO MWENYEZ MUNGU AKAMTUMA MTUME MUSSA BIN MANSHA AJE KUWALINGANIA WATU WAACHANE NA KUABUDU WACHAWI NA MIZIMU NA HATIMAYE WAMUABUDU MUNGU ALIYE HAI AMBAYE NI ALLAHU SUBHAANAHU WATAALA. 

LAKINI MPAKA SASA WASHIRIKINA WA KICHAWI WAMEKUWA WAKIENDELEZA UCHAWI HUU NA KUUFANYA KIDIGITALI ZAIDI KAMA SI MJUZI HUWEZI KUWAJUA...........