Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Ijumaa, 15 Januari 2016

TUANGALIE UTAWALA KATIKA ULIMWENGU WA WACHAWI

Habari zenu wapendwa......................................................

Wachawi wana serikali na utawala wao kama ilivyo kwenye maisha ya kawaida ya binadamu wa kawaida,wachawi wana utawala unaoanzia katika ngazi za mtaa,kata,kijiji,tarafa,wilaya,mkoa,taifa mpaka uongozi wa kimataifa........

Tibazetu.blogspot.com
Watu hawa wachawi wana heshima kubwa sana juu ya viongozi wao na huwatii bila kubisha au kupinga kwa kila jambo watakaloamrishwa.Kuna mikutano ya kijiji hufanyika,hapa hukusanyika wachawi wa kijiji fulani katika viwanja maalum vilivyotengwa aghlabu huwa ni  chini ya miti mikubwa na kujadili mipango na kazi zao za kichawi ikiwemo kula nyama za watu wao kwa kupeana zamu,kuwaadhibu jirani zao na kuleta malalamiko yao kwa mkubwa.vilevile huwa wana siku maalum za kukutana kiwilaya na mkoa mpaka ngazi ya  taifa,na pia hutembelewa na kiongozi wao wa kimataifa kila baada ya muda fulani na huandaa mapokezi makubwa kama mfano vile ambavyo viongozi mbalimbali wanavyokuja kuitembelea tz na kupokewa kwa furaha kubwa.
Tibazetu.blogspot.com
Wachawi wanapoingia kwenye ulimwengu wa kichawi huwa ni marufuku kuchukua kitu cha mtu yeyote ambaye wameingia ndani kwake kumchawia,au kumuonea aibu,kumkingia kifua au huruma mtu yeyote hata akiwa mama yako mzazi,pindi mchawi anapokuwa ashavaa vazi la kichawi anatakiwa awe na nafsi mbaya sawa na ya shetani wa kijini na akijifanya kuwa na huruma basi mkuu wa kundi atamuadhibu.
tibazetu.blogspot.com
pindi wachawi wanapomchukua mtu msukule na akaonekana kama amekufa machoni pa watu wake,wachawi hawa humchukua mtu huyu na kwenda kumtumikisha kazi ngumungumu,kumuadhibu na kumtesa  pamoja na kumbebesha maiti za watu waliokufa jana au leo


sasa mtu huyu unapofika muda wake wa kufa kiukweli yaani muda ambao amepangiwa na aliyemuumba kuwa ndiyo khadari yake{muda wake wa kufa}akifa wachawi wale humchukua mtu huyu na wanajisevia kwa kumla nyama huku mtawala wao akiwagawia mapaja,mikono,na sehemu za steki nzuuuuri wanakula wenye vyeo ikiwemo sehemu za matako nk.

 AYATUR KURSIYYU
~Hii ni bakora tena ni radi na ndiyo kiboko ya wachawi wote katika kujinasua na vitimbi na balaa zao isome hii mara kwa mara nyumbani kwako Inshaa Allah utakuwa salama.


kutoka kwa Ally Bin Abiy Twaalib{r.a} amesema mtume{s.a.w} "haitasomwa aya yaani{ayaturkursiyyu}katika nyumba yoyote ispokuwa masheitwaani huikimbia nyumba hiyo kwa muda wa siku 30 na wala hataweza kuingia katika nyumba ya mtu fulani,hatoweza kuingia mchawi wa kiume wala mchawi wa kike katika nyumba hiyo kwa muda wa siku40.

Ally chambas
0653 532036......whatsapp
0777 145913