Kiukweli kuna baadhi ya akina mama wamekuwa na tatizo la kutoshika mimba kwa muda mrefu au wapatapo ujauzito basi mimba huaribika mara kwa mara na kuambulia patupu. Kuna baadhi ya wanaume wenye uelewa mdogo hudhani kwamba kutopatikana kwa mimba katika ndoa ni tatizo la wanawake tuu,kumbe laa hasha tatizo hili linaweza kusababishwa hata na mwanaume pia,cha msingi ni wanandoa wote wawili kuweza kumuona mtaalam wa afya kwa ajili ya vipimo na kugundua tatizo,ili aliye nalo aanze tiba mara moja na sio kulaumiana na kutoleana lugha chafu kila siku. Kama tatizo litaonekana analo mwanamke basi atumie njia hii ifuatayo ambayo ni ya asili kwani imeweza kuwasaidia wanawake wengi waliokwisha kata tamaa na kupata watoto. .MIZIZI YA MPERA Tibazetu.blogspot.com Naamini wengi wetu tunaujua mti wa mpera ambao matunda yake hutumika kama tunda kiburudisho na hupendwa sana na watoto. Mizizi ya mti huu ni tiba nzuri ya uzazi kwa wale wanaosumbuliwa na tatizo hili la kutoshika ujauzito basi na atumie mizizi hii ya mti huu. JINSI YA KUTUMIA MIZIZI YA MPERA ~Chukua mizizi ya mpera ya kutosha uioshe vizuri halafu weka lita1 ya maji safi na ichemshe ichemke vizuri,baada ya hapo ipua jikoni na acha ipoe kiasi,kunywa lita yote kwa siku1 uimalize yaani nusu asubuhi na nusu usiku wakati wa kulala. Endelea kufanya zoezi hili walau mara2 kwa mwezi kwa muda wa miezi 3 mpaka 4 kisha uwe unashiriki tendo la ndoa kwa uwezo wa mungu utapata mimba. TATIZO LA KUHARIBIKA KWA MIMBA
~Naam kuna baadhi ya wanawake wao hushika mimba vizuri lakini wanasumbuliwa na hili tatizo la kuharibika kwa mimba mara kwa mara,wengi wao wamehangaika kutafuta tiba sehemu mbalimbali bila mafanikio na hivo wamebaki mashakani bila kujua nini cha kufanya ili kujinusuru. Lakini kutokana na utafiti wa kina imegundulika kwamba kuna tiba ya asili ambayo inaweza kutokomeza kabisa hali hii na mimba kutoharibika tena,na muhusika kuweza kujifungua salama kabisa. MIZIZI YA MTI WA MUEMBE
tibazetu.blogspot.com tibazetutz@gmail.com 0653 532036 ~Embe ni tunda tamu sana na hakuna asiyelijua kwa vile ni tunda maarufu sana duniani,lakini sidhani kama wengi wanafahamu kuwa mizizi ya mti huu ni tiba nzuri inayoweza kutibu na kumaliza kabisa matatizo ya kuharibika kwa mimba. JINSI YA KUTUMIA ~Chukua miziz ya kutosha ya mti wa muembe wowote ioshe vizuri na uchanganye na maji kiasi cha lita1na uiache ichemke vizuri.baada ya hapo epua jikoni acha ipoe kidogo na utumie glass1asubuhi na moja jioni Utatumia dawa hii kwa wiki1 kwa uwezo wa mungu tatizo litakoma na mimba haitoharibika na mzazi atapata alichokitarajia.

