Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Ijumaa, 12 Machi 2021

tego la kumuadhibu mwizi akija kuiba nyumbani,shambani au popote awe analia Kama mbuzi

Habari zenu wafuatiliaji wa ukurasa huu pendwa wa tibazetu,katika kuhakikisha tunatunza na kuhifadhi maarifa sahihi tuliyorithishwa na wazee wetu waliotangulia tunaendelea kuelimishana na kukumbushana juu ya sayansi ya kiafrika ambayo ilitumika na bado inatumika mpaka sasa katika kuwaadhibu wezi wanaoingia katika mashamba,majumba,maduka,na sehemu mbalimbali na kufanya uhalifu ambao unamrudisha nyuma na kumtia simanzi mfanyiwa.

Njia mojawapo ni uchawi wa kigozi Cha mbuzi
Njia hii hutengenezwa Kama ifuatavyo

Kinachukuliwa kipande Cha ngozi katika ngozi ya mbuzi,ngozi hiyo inachomwa na kusagwa mpaka upatikane ungaunga.

Unga huo sasa huchanganywa na usembe,mafuta ya nyemba,na Jani la kilele Cha mti wa mtomoko na kufanyiwa manuizi maalum,Kisha vinafungwa pamoja sehemu inayotaka kulindwa.

Kinachotokea Sasa pindi mwizi anapokuja na kuiba kitu sehemu hiyo
-akishaiba na kuondoka maeneo hayo tu ghafla ulimi unajitokeza nje na anaanza kulia meee! Meee! Meee! Mithiri ya mbuzi aliyepotea.huambatana na hali ya kushindwa kula chochote wala kunywa,muda wote Ni hivyo na asipowahiwa kunyweshwa dawa ya kutegua tego hilo basi hafiki siku tatu anafariki dunia.

Karibu katika group letu la WhatsApp ujifunze Mambo mbalimbali na jinsi ya kutatua changamoto nyingi kupitia sayansi ya kiafrika