Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatano, 30 Novemba 2016

DAWA YA ASILI YA KUSAFISHA DAMU

MAJI YA LIMAU NA KITUNGU SAUMU



Kitungu saumu na limau zinajulikana kuwa na uwezo mkubwa wakusafisha mishipa ya damu, kupunguza lehemu (cholesterol), kukaza kuta za mishipa ya damu na kupunguza uwezekano wa kupata maradhi ya mishipa ya damu yanayotokamana na uvimbe au mafuta kuganda katika mishipa ya damu.

Kusafisha mishipa ya damu huondoa sumu ndani ya damu nakufanya damu iweze kutembea ndani ya mwili kwa urahisi binadamu hutumia njia mbali mbali kusafisha damu ima njia za hospitali ambazo mara nyingi huwa zina madhara na unashauriwa utumie njia za hospitali kama njia ya mwisho iwapo njia zote zingine zimeshindikana.

 Tiba mbadala za kinyumbani huwa hazina madhara lakini zinahitaji upate mwenye ujuzi wa tiba hizo akushauri aina ya dawa ya kutumia, vipimo husika na muda wa matumizi ili usidhuru afya yako.

Maji ya limau na kitungu saumu imetumika karne nyingi kutibu kansa. Wanasayansi wamesema kitungu saumu inazalisha na kuuwa seli mbovu ndani ya damu tukio ambalo linasaidia sana wanaogua kansa.

VINAVYOHITAJIKA
- Kitungu saumu 4,
- Limau 4 (kata slesi nyembamba),
- Maji safi lita 3

NAMNA YA KUTAYARISHA
- Chambua vitungu saumu na usafishe.
- Kata slesi nyembamba za limau kisha utie kwenye maji yanayochemka.
- Ponda au saga kutumia blenda
- Tia rojo ndani ya jagi kisha umimine yale maji ya moto lita 3 mpaka yajae.
- Funika kisha weke ndani ya friji kwa mda wa siku 3.
- Chuja maji hayo baada ya siku 3 na uendelee kuhifadhi maji ndani ya friji.

NAMNA YA MATUMIZI
Tia vijiko 5 vya meza ndani ya glasi ya maji na unywe mara 3 kila siku kabla ya kula. Ila kama wasafisha mishipa ya damu utaanza na kijiko 1 au 2 vya mezani mara 3 kila siku ndipo sasa kama hutohisi dhiki uongeze idadi ya vijiko kadri siku zinavyoongezeka mpaka ufikie vijiko 5 mara 3 kwa siku.

Utumie kwa siku 40 mfululizo na iwe mara moja kila mwaka. Damu yako itarudi kuwa nyepesi na mzunguko wa damu ndani ya bongo na ya mwili kwa jumla utakuwa bora.