Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatatu, 24 Aprili 2017

TFDA: Yatoa ufafanuzi kuhusu usalama wa mafuta ya alizeti

Mamlaka ya Chakula na Dawa(TFDA) imefanya uchambuzi wa awali wa matokeo ya utafiti uliofanywa mwaka 2014/15 na wataalamu kutoka Michigan State University Marekani wakishirikiana na SUA kuhusu mbegu za alizeti na mashudu kuchafuliwa na Aflatoxins.

Uchambuzi huo umebaini kuwa utafiti huo ulihusu mbegu za alizeti na mashudu pekee hivyo hautoshelezi kuthibitisha kuwa mafuta ya Alizeti yanachafuliwa na Aflatoxins kwa kiwango hatarishi.

Hivyo wamesema wananchi waendelee kuyatumia mafuta ya Alizeti hasa yaliyothibitishwa na TFDA.

Hata hivyo TFDA itafanya uchambuzi wa kina wa matokeo ya utafiti huo na kufanya ufatiliaji na uchunguzi zaidi wa mbegu, mashudu na mafuta ya alizeti yanayozalishwa nchini.

Rai inatolewa kwa vyombo vya habari kuwasilisha tafiti za kisayansi zinazohusu usalama na ubora wa chakula, dawa, vipodozi kabla ya kuchapisha ili kuondoa uwezekano wa kuleta hofu kwa jamii.