Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatatu, 24 Aprili 2017

hafkaani ni ugonjwa unaompata mtu asiyetaka kuwatambua majini wake

Ninapozungumzia ugonjwa wa hafkaani ni aina ya ugonjwa wa akili ambao anaupata mtu yeyote mwenye majini pale inapofikia  anashindwa kuwatambua majini wake alikuwa nao mwilini mwake kwa makusudi japokuwa majini wale wanapatia habari mbali mbali lakini binadam huyo anashindwa kufuatilia kutokana na sababu yeyote lakini mara nyingi huwapata wale ambao wanapuuzia kwa makusudi . Ndipo majini hawa huamua kumsababishia mhusika wao huyo ugonjwa huu wa hafkaani ili kumkumbusha na kumtia adabu kutokana na dharau zake za kutowafuatilia na kuwatilia maanani hivyo wanamsababishia mtu huyo ugonjwa ambao unaitwa Hafkani.

DALILI YAKUONYESHA KUWA UNA UGONJWA WA HAFKANI.
Kwa mtu ambaye atakuwa sasa amefikia katika hatua hiyo moja ya dalili kubwa ya ugonjwa wa kijini wa hafkaani ni kuogopa ogopa

katika hali hii ni kwamba unajikuta unakuwa muoga muoga,huna amani,unahisi moyo kukulipuka kila wakati yaani wewe unakuwa na hofu na uwoga, japokuwa haupo sehemu yakuogopesha wala hujafanya jambo lakusababisha wewe kuwa na hofu au kuhofia.

 dalili kuu ya pili  nikufikia wakati wewe unajiona kama haupumui vizuri kama ni mtu unayetaka kukata roho muda wowote yaani unakuwa ni mtu wa uwoga woga moyo wako unakwenda mbio kila mara unaripuka ripuka tuu. Kifupi unakosa amani popote ulipo.