Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatatu, 24 Aprili 2017

kijana anayetafuna chupa na misumari


KIJANA mmoja aliyejitambulisha kwa jina la James John mkazi wa Mchikichini jijini Dar es Salaam ameonakana kuwashangaza watu wengi wa maeneo ya Kariakoo jijini Dar es Salaam baada ya kuwa kivutio kikubwa kwao alipoonekana  akitafuna vitu vya ajabu vikiwemo vipande vya chupa na misumari.

Mtandao huu ulipata fursa ya kuzungumza na kijana huyo ambaye alieleza kuwa yeye ni mzaliwa wa Wilaya ya Kasulu mkoani Kogoma na alikuja jijini Dar es Salaam kwa lengo la kupanua uwezo wa kipaji chake cha sanaa.

Ameeleza kuwa katika sanaa yake anao uwezo mkubwa wa kufanya vitu vya ajabu vinavyoweza kushangaza watu kiasi cha  kutokuamini kile anachokifanya.  Miongoni mwa matukio yaliyoshuhudiwa na kamera yetu ni  kutafuna vipande vya chupa, kulalia kibao chenye misumari bila kumchoma na kutafuna misumari.

Mbali na hayo,  kijana huyo ameeleza kuwa pia anayo staili ya kubadilisha mkanda kuwa nyoka na kunywa maji lita 20 papohapo.

Katika kuonyesha shoo yake,  hutoza kiasi cha Sh. 100 na kuendelea kulingana na wananchi wanachomchangia.