Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumapili, 19 Machi 2017

KUJUA TABIA YA MTU KWA KUTUMIA RANGI.


Je Wajua kwamba waweza kujua tabia ya mtu kwa kutumia rangi.?
Na hii itakufanya kujua tabia hata ya mwanaume uliyenaye au mwanamke uliyenaye kabla hata ya kuanza mahusiano na kujua jinsi ya kuishi naye.
Rangi ndio tabia ya mtu.
Rangi ina maana kubwa sana japo haijachumbuliwa sana kidini lkn dalili za umuhimu wake zilianza kuonekana kwenye maisha ya mitume.
Kwa waarabu rangi nyeusi ni uturivu,usikivu,upole na usimamizi wa familia.
Mwenye kuvaa rangi nyeusi sana hata kama alikuwa mkorofi tabia itabadilika na kuwa muelewa na kupenda amani.
Ndio maana mavazi ya wanawake ya waarabu wengi ni meusi.
Nyeupe ni taa,busara,hekma,nguvu ya kuona mbali, busara ya amani,kivutio cha mafanikio.
Mavazi ya wanaume wengi ya kiarabu ni meupe kwa imani kwamba wao ndio watafutaji na watunzaji wa familia zao.
Hiyo ni mifano tu kuhusu rangi
Lkn Leo nakuletea kitabibu ktk shuhuri zetu za kiganga.
Rangi humu elezea mtu. Vile anavyojisikia kwa siku hiyo, pia tabia ya mtu huyo kiujumla unaweza kufahamu kutokana na rangi anazozipenda.
Pia itakufanya kujua majini yanayomtawala mtu huyo kwa kuwa kila mtu ana majini.
1.Nyeusi.


Mtu mwenye kupenda sana kuvaa nguo nyeusi. Tabia yake hupenda vitu vya asili, wasuruhishaji wa migogoro, hupenda kujishusha, wana hekma na bahati ya kupewa madaraka ya uongozi.
Huheshimiwa hoja zao na wapenda rangi zingine japo wakati mwingine hudharaulika kwa kujifanya wanabusara sana.
Watu hawa miili yao hutawaliwa na mila pamoja na mizimu.
Ndoto zao nyingi zitahusu kijijini ama kuota wazee wa kule anapotokea kwenye asili yake.
Wakati mwingine nyeusi huashiria uchawi na mwili kuwa mchafu.
Mwenye kuota rangi nyeusi au amevaa nguo nyeusi basi maana yake amerogwa na anatakiwa atibiwe haraka kusafishwa.
Mwenye kuota anakimbizwa ama kushambuliwa na mnyama ama nyoka mweusi basi amerogwa uchawi mkubwa kuliko yote na ni ngumu kupona mtu huyu bila kupata tiba ya haraka na uhakika

Mwenye kupenda rangi nyeusi anakuwa na nguvu ya kimaamuzi na mingi wa kukabiliana na changamoto za watu.
Hupenda vitu vya asili, hapendi kujikweza, hupenda ndugu na watu wa ukoo wake.
Hawapendi kuishi kifahari pia hupenda maisha ya mitimiti na si kubanana.
Ukienda kwa mganga ghafra ukajikuta umeamua kuvaa nguo nyeusi basi jua umerogwa na kutiwa kiza kichawi,
Mwenye kuumwa ugonjwa wa hospital na akajikuta kavaa nguo nyeusi na si kawaida yake basi ugonjwa wake ni mkubwa sana na inatakiwa itumike njia hasa kujua tatizo.
Mgonjwa mahututi akilazinisha kuvalishwa nguo nyeusi basi mauti yatamfika.
Pia nyeusi na ufalme na nguvu ya heshima .
Mwenye kupenda mavazi meusi ndoto zake zinakuwa za vijijini,wazee wake,kuota watu aliokuwa nao.
Pia inaaminika mwenye kujilazimisha kuvaa nguo nyeusi basi atapata nguvu ya kutiiwa na jamii.
Mwenye kuota anashambuliwa na wanyama weusi ama nyoka mweusi basi ametumiwa uchawi mkubwa ama atafukwa na tatizo kubwa.
Mwenye kuota amevakishwa nguo nyeusi anatakiwa atambikiwe ama atibiwe kiasili.
Mwenye kuwikiwa na kuku mweusi mbele ya uso wake basi atapata safari ya kwenda kijijini kwao.