Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumapili, 15 Novemba 2015

ELIMU JUU YA UWEZEKANO WA KUSHIKA MIMBA

Elimu ya kutambua uwezekano wa kushika mimba hujumuisha mambo yote yanayotumika kuamua wakati mwanamke anapoweza kushika mimba au kutokushuka mimba katika siku za mzunguko wake wa hedhi.

Mbinu hizi hutumiwa katika kuzuia mimba isiyotarajiwa,au kama njia ya kufuatilia afya ya uzazi ya mwanamke huyo.

Zifuatazo ni njia zinazotumika kutambua siku ambayo uwezekano wa mwanamke kupata mimba ni mkubwa sana

tibazetu.blogspot.com

JOTO LA MWILI 
Hili ni joto la mwili wa mwanamke linalochukuliwa wakati wa kuamka asubuhi au baada ya usingizi wa muda mrefu katika siku,miongoni mwa wanawake kudondoka kwa yai husababisha  kupanda kwa joto la mwili kati ya nyuzi 0.3 na 0.9 centigred au o.5 na 1.6 farenhait ambalo joto hilo hubakia hivyo katika kipindi chote hadi wakati wa hedhi ijayo.

mabadiliko haya ya joto yanaweza kutumika kubaini mwanzo wa kipindi cha kutokutunga  na hata kabla ya kudondosha yai.


KAMASI ZA MLANGO WA KIZAZI
Kuonekana kwa kamasi za mlango wa kizazi na muwasho wa uke ni ishara zinazoelezwa kwa pamoja kama ni ishara mbili zinazotumika kutambua kipindi cha kupata mimba,

kamasi za mlango wa kizazi huzalishwa na mlango wa uzazi ambao hutenganisha uterasi na mfereji wa uke,

kamasi za mlango wa kizazi zenye kuashiria uwezekano wa kushika mimba hukuza maisha ya manii kwa kupunguza asidi ya ukeni na pia huongoza manii kupita katika mlango wa kizazi kuelekea ndani ya uterasi

uzalishwaji wa kamasi za mlango wa kizazi zenye rutuba husababishwa na kichocheo cha stojeni ambacho pia huandaa mwili wa mwanamke kwa udondoshwaji wa yai.kwa kuangalia kamasi za mlango wa kizazi na kuzingatia hisia ya jinsi inavyopita ukeni mwanamke atakuwa anaweza kubaini wakati mwili wake unapojiandaa kudondosha yai na hata wakati wa udondoshwaji kupita 

uzalishwaji wa estrojeni hupungua na projestroni huanza kuongezeka na
kupanda kwa kiwango cha projestroni husababisha mabadiliko katika wingi na hali ya kamasi inayopatikana ukeni.

MKAO WA MLANGO WA KIZAZI
Mlango wa kizazi hubadilisha mkao kutokana na kichocheo kinachosababisha kutolewa kwa kamasi za mlango wa kizazi kukauka

wakati mwanamke yupo katika awamu ya kutoshika mimba ya mzunguko wa hedhi mlango wa kizazi hushuka chini katika mfereji wa uke ukiguswa huwa mgumu[km ncha ya pua ya mtu]na upenyo unaoelekea katika mlango wa kizazi utakuwa mdogo ikilinganishwa na wakati mwingine ambapo huwa wazi zaid

jinsi uwezekano wa mwanamke kupata mimba unavyoongezeka ndivyo mlango wa kizazi unavyopanda juu ya mfereji wa uke,unakuwa laini kama mdomo wa mtu ukiguswa na upenyo unakuwa wazi zaidi

,baada ya kudondoshwa kwa yai mlango wa kizazi hurejea katika mkao wake wa kawaida na hiki huwa si kipindi cha kushika mimba.