Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumanne, 3 Novemba 2015

JINSI MCHAWI ANAVYOMWITA JINI NA KUMTUMA

                                                  NJIA YA KIGANJA CHA MTOTO

Habari zenu wapendwa natumai mko salama
tibazetu.blogspot.com
Njia hii ya kumuita jini muovu aliyehasi na kumtumia kwa kutumia kiganja cha mtoto mdogo ambaye hajabalehe ni njia inayofahamika sana na wachawi sababu ni miongoni mwa njia wanazozipenda sana kutokana na urahisi wake na wepesi wa kuleta majibu kwa kuhudhuria kwa jini husika anayeitwa eneo hilo. 

Katika njia hii ya kutumia kiganja cha mkono wa mtoto mdogo anachokifanya mchawi wakati ameshakusudia kutaka kumroga fulani bin fulani au kuafnya kitu chochote kile humchukua mtoto huyo ambaye ni lazima awe hajabalehe  na awe hayupo msafi wa mwili na mavazi yaani awe amejikojolea,amejinyea,au apakwe kinyesi,mkojo,damu ya hedhi au chochote kile ili mradi hatakiwi awe ni msafi.

Mtoto huwekwa chini na kisha mchawi akachukua kiganja cha mtoto huyu na huchora mraba[pembenne]na kando ya huu mchoro anaandika maneno ya kichawi na mara nyingi huandika maneno mazito ya kufru na kumtukana mungu pamoja na kuwatukuza majini wao,maneno hayo wanaandika pande zote4 za mraba.

Kisha pale katikati ya mraba huu anaweka maua ya alizeti na maua ya rangi ya blue au maua ya alizeti na wino rangi ya blue hapo kwenye mraba uliochorwa katikati ya kiganja cha mtoto huyo asiyejua chochote kinachoendelea maskini.

tibazetu.blogspot.com
Kisha anaandika tarasimu fulani kwa herufi mojamoja juu ya karatasi ndefu ya pembe nne,halafu karatasi hii inawekwa juu ya uso wa mtoto na anavalishwa kofia halafu anaambiwa atazame kiganja chake na kama ataona chochote aseme,hapo sasa mchawi huyu aliyelaaniwa anaanza kusoma matarasimu na maazima yake mazito ya kichawi kutokana na jini husika anayemwita kuja kumtumia.

Ghafla yule mtoto ataanza kuhisi mwangaza unatokea kwenye kiganja chake na huanza kuziona picha zinachezacheza kwenyenye kiganja chake na hapo mchawi huyu atamuuliza mtoto ''unaona nini?'' mtoto atasema ''naona sura ya mtu ananitazama''basi mchawi huyu anasema ''mwambie waambiwa na mwenye matarasimu haya ufanye  kadhaa wa kadhaa..na picha ile itaashiria kukubali kulingana na amri ile na kuitekeleza...

Basi hii ndiyo njia mjawapo katika njia nyingi wanazotumia wachawi, laana za Mwenyez mungu ziwe juu yao,katika kumuita mshirika mwenzao shetani wa kijini na kufanya uharibifu kwa watu wengine...........................................................................................