Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Ijumaa, 6 Novemba 2015

BAADHI YA MAMBO WANAYOYAFANYA WACHAWI ILI WAWE KARIBU NA MASHETANI WA KIJINI

Haya ndiyo mambo wanayoyafanya wachawi ili wajikurubishe zaidi na mashetani wao ili waweze kuwa na nguvu na uwezo mkubwa pindi wanapofanya mambo yao ya kishenzi katika kuwaharibia maisha na mipango viumbe wenzao.

Wachawi hawa ili kuweza kutimiza uwezo wa kufanya maajabu makubwa zaidi basi ni sharti wawe wanafanya mambo ambayo ni makubwa zaidi katika ukafiri,kadri anavyozidisha ubaya ndiyo anapanda cheo na kuwa ni mwenye kuogopwa na kuheshimiwa kuliko wachawi wengine,Mungu atunusuru kuwa miongoni mwao


KUVAA KITABU KITUKUFU MIGUUNI KAMA VIATU NA KUINGIA NACHO CHOONI 
~Hapa mchawi anachukua kitabu kitukufu cha kurani na hukivaa chini ya nyayo zake za miguu hali ya kuwa anajua kuwa kufanya hivo ni dhambi na ukafiri mkubwa kisha anaingia nacho chooni kwenye najisi na kukanyaga uchafu huo huku akisema maneno ya kuwatukuza na kuwasifu mashetani,nao kwa kuiona kazi kubwa anayoifanya binadamu huyu kwa kukidhalilisha kitabu kitukufu basi wanamfurahia na kumkimbilia kumpa msaada.



KUANDIKA AYA ZA KURAN KWA KUTUMIA DAMU YA HEDHI 

~Muna wengine wao hutafuta damu ya hedhi ya mwanamke kwa njia na gharama yoyote ile,kisha wanachukua karatasi nyeupe na wanaandika maneno hayo matukufu ya Allah[s.w], kwa kutumia damu ya hedhi ili wamkufuru mungu wao kimakusudi na kuwaridhisha mashetani ambao muda wote huo wanakuwa wanamuangalia na kumfurahia mja huyu aliyeamua kwenda motoni pamoja nao. 



KUANDIKA AYA ZA KURAN KWENYE NYAYO ZA MIGUU
~Hapa huwa wanafanya kama wanavyofanya katika kuvaa kitabu kitukufu miguuni na kuingia nacho chooni kama viatu...Mungu awalani na kuwaangamiza viumbe hawa 
 aamin







KUANDIKA SURAT FATHA KINYUMENYUME
~Katika kipengele hiki wao wanachukua karatasi nyeupe na wino wowote aghlabu huwa ni wino mweusi na huanza kuiandika sura hiyo nyuma mbele,mbele nyuma na kuiharibu kabisa maana yake halisi iliyokusudiwa na Mwenyez Mungu ili awafurahishe mashetani wake hawa.





KUSWALI BILA UDHU
~Wengine wao huamrishwa na mashetani wao ili wawape nguvu zaidi katika uchawi lazima waswali bila kutia udhu au wawe na janaba,hapo ndiyo hupendwa zaidi na mashetani na kazi zake za uchawi huwa rahisi zaidi.lakini kumbuka yote haya shetani anakulingania umkufuru mungu wako ili muingie wote kwenye moto wa milele.




KUCHINJA BILA KUMTAJA MUNGU NA KUMPELEKA MNYAMA KWA SHETANI
~Wengine huwa wanaamrishwa watafute mnyama mwenye rangi maalum na amchinje bila kutaja BISMILLAH kisha mnyama huyo anatumwa akamtupe sehemu maalum aliyoelekezwa ambapo aghlabu huwa maskani ya shetani huyo anayemchinjia,naye shetani huyu baada ya kuona amemchinjia yeye badala ya kuchinja kwa ajili ya Mungu basi anafurahi na kufanya kazi yake ya uchawi iwe rahisi zaidi.  





KUZISUJUDIA NYOTA NA KUZIABUDU
~Wamo miongoni mwao huzisujudia nyota na kuziabudu kama vile anavyotakiwa kuabudiwa Mungu.Wanafanya haya yote  ili waweze kupata nguvu zaidi ktk uchawi kutoka kwa shetani wao na lengo la shetani huyu ni lilelile anataka apate kuwakusanya wanaadamu wengi wa kuingia nao motoni,maana kabla hujawa mchawi lazima ujikubalishe kumkataa Mungu.




 KUANDIKA MANENO YA KUFRU KWENYE  KARATASI KISHA KUIWEKA NDANI YA HIRIZI NA KUIVAA MWILINI MWAKE MUDA WOTE 
 ~Hawa wao huamrishwa waandike maneno mazito ya kumkufuru mungu kutukana mitume wake na kukashifu vitabu vyake,maandishi haya yanaweza kuandikwa kwa lugha yoyote kiarabu,kiyunani au hata kiswahili nk,na kisha mchawi anatengeneza hirizi ambayo ndani yake anaweka karatasi hiyo na muda wote anatakiwa avae hirizi hii bila kuivua,,,[mateso makubwa haya] 


hivyo hapa tunaweza kuona ni jinsi gani shetani hawezi kukusaidia burebure tuu ispokuwa mpaka ahakikishe kuwa amekukufurisha na kukutoa kwenye dini yako.

SHETANI NI ADUI YETU NASI TUMFANYENI ADUI NA SIO RAFIKI