Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatatu, 2 Novemba 2015

JINSI MCHAWI ANAVYOMWITA JINI NA KUMTUMA

                             NJIA YA UANGALIZI

 Hii pia ni miongoni mwa njia wanazotumia wachawi hawa katika kumuita kafiri mwenzao wa kijijini na kumtumia katika shugli zao za kiuchawi na kuwasababishia matatizo binadamu wenzao au hata wanyama mbalimbali wa kufugwa bila sababu yoyote ya msingi.


katika njia hii mchawi ambaye anataka kumuita jinni huyu aliyehasi amri za mola wake ni lazima avizie iwe usiku sana nyakati za giza, hutafuta sehemu nzuri ambayo ataweza kuziona nyota angani kisha hukaa hapo huku akiangalia nyota fulani na kuisubiri itokeze angani.


Ikishatokeza nyota hii huinuka mchawi huyu na huanza kuiomba kwa visomo na maneno ya kichawi  halafu anaanza kusoma tarasimu yenye maneno mazito ya kichawi na kuwaita majini waje kumtumikia,hakika maneno haya wanayoyasema ni mazito mno yasiyoweza kuandikika au kusemwa hadharani na mtu mwenye kumuogopa muumba wake.


Baada ya hapo anafanya harakati fulani kwa kupeleka mikono yake juu na kuishusha chini[kama anavuta kitu]mwenyewe anadai anateremsha pepo wa nyota iyo lakini kwa hakika hii ni ibada anayoifanya kuiabudu nyota hii badala ya mungu hata kama mchawi huyo alipofundishwa njia hiyo hakuambiwa hayo.


Basi kinachofuata hapo ni kuwa Mashetani yanaitikia amri ya mchawi huyu aliyelaaniwa baada ya kuona na kupenda harakati zake anazozifanya kumkufuru mungu na kuliongezea idadi jeshi la Ibilisi,na wanamfanyia kile kitu chake alichotia nia kukifanya huku yeye anaamini kuwa ile nyota ndiyo iliyomsaidia.


Nyota hii ambayo imesingiziwa uongo huu maskini huwa haijui kitu chochote kinachoendelea  hapo bali ni maujanja tuu ya shetani katika kumzuga binadamu na kumtia dhambini.


Wachawi wenyewe wanaamini kuwa ukiwa umerogwa uchawi anaotumiwa jini wa namna hii,hauwezi kupona mpaka uaguliwe ndani ya siku ambayo nyota hiyo itaonekana tena  na kuna nyota ambazo zenyewe kwa mwaka hutokea mara moja tuu,yaani uisubiri ile nyota tena na ikitokeza uiombe ikufungulie uchawi uliorogwa kwa kutumia jini wa njia hii.


Lakini ukweli ni kwamba hakika wayafanyayo wachawi ni vitimbi tuu mbele ya mkuu na mmiliki wa viumbe vyote, kwani kwa wale ambao tunatibu kwa kutumia kurani tunaibatilisha na kumtibu mtu mwenye matatizo haya mara moja Inshaa Allah.



kwa tiba na ushauri kuhusu masuala ya afya ya mwili na roho wasiliana nasi kwa 
+255 653 532036
+255 764 995259
tibazetutz@gmail.com