Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatatu, 16 Novemba 2015

NJIA HARAMU ZA KUMTOA JINNI MWILINI MWA MGONJWA

NJIA YA AZ-ZAAR
 watu wamezusha sherehe za kitiba ambazo hazikuwa katika mienendo ya watu wema waliotangulia,lkn ni katika uzushi wa zama hizi na munkar umeenea sana zama hizi.

miongoni mwa sherehe hizo ni az zaar zilizo na madhambi na ambazo zimewekwa kwa hoja ya kumponya mgonjwa na kumuondolea maradhi ya jini aliyoyapata

mwanamke anaweza kuwa mgonjwa na akapandisha mashetani na mashetani wale wakamchezea akili yake na kudai kuwa amepatwa na kifafa cha jini na wao wana uwezo wa kumuondolea na hapo wakataka matakwa mazito na gharama kama dhahabu,kila aina ya kuku,kondoo,mbuzi,ngombe nk

wakati mwingine wanapoona mtu huyu ni matajiri basi hutaka vitu vikubwa zaidi na hafla inapoanza mgonjwa huyu hupewa jina la biharusi,wanamvisha nguo za thamani sana kwa muda mfupi kisha wanampandisha juu ya ngamia au fahali na kando yake wanawasha mishumaa huku wakipiga vinubi,kelele na nyimbo zinazovutia nyoyo  

wakati huo mgonjwa huwa akipata furaha kutokana na athari ya madufu,nyimbo na vinubi na furaha hiyo husambaa ndani ya moyo wake kutokana na sherehe hii kubwa nao humuona kana kwamba tayari matatizo yamekwisha. 

lakini baada ya muda fulani maradhi humrudia mwanamke yule kwani yule jini anayedai kumweza kumsaidia anataka afanyiwe yale mambo km kuridhishwa yeye tuu nafsi yake na watu wanapoishiwa pesa hawawezi tena kufanya hizo sherehe mgonjwa huweza kufariki kutokana na afriti huyu wa kijini anayechezea watu akili zao.


NJIA YA AL-ISTIRDHAA[KUTAKA RADHI]
Katika njia hii yule mganga anayetibu humtaka radhi yule shetani aliyepanda kichwani mwa mgonjwa na kumuomba kwa upole na unyenyekevu,shetani huyo anaweza akataka achinjiwe mnyama au kuvaa dhahabu au hata avute sigara au mengineyo katika mambo ya haramu,ni lazima mganga ayakubali haya yote  


NJIA YA KUOMBA MSAADA
  anayetumia njia hii yeye humuomba msaada jini anayemtumikia katika mambo yake ili amsaidie kumtoa jini anayemsumbua mgonjwa,mara nyingine yule jini wa mganaga huyu huwa ni dhaifu kuliko yule aliyemuingia mgonjwa kwani majini wanazidiana nguvu na uwezo basi hapo hawezi kabisa kumtoa jini huyo..


NJIA YA KUAPA
Hapa katika njia hii ni kuwa yule anayetibu humuapia jini anayemsumbua mgonjwa kwa wakubwa zake wa kijini kwa sababu majini wana makabila na uongozi wao km tulivyo sisi[kama vile mtoto wa fulani akikusumbua unamsemea kwa baba yake naye anamuadhibu ili aache utundu] kwenye majin kuna wenye nguvu na madhaifu,watawala na watawaliwa,wakuu na wanyonge.basi hapo huyu anayetibu akishajulishwa kabila la jini anayemsumbua mgonjwa basi humuapia kwa mkubwa wa kabila hilo na mtawala wake basi yule jini msumbufu kwa mgonjwa akaogopa na kutoka na katika njia hii muna ushirikina usiofichika.


NJIA YA KUMFUNGA JINNI ANAYESUMBUA
Hapa ni kwamba huyu anayetibu hujikaribisha kwa viongozi wa kabila hili la jini anayemsumbua mgonjwa kwa aina fulani ya ushirikina kisha anawaomba wamfunge jini huyu anayemsumbua mgonjwa wake  basi viongozi wa kijini kwa kuwa wamefanyiwa wanalolipenda wanamfunga jela jini huyu msumbufu

KILA NJIA ILIYO NA USHIRIKINA AU JAMBO LILILOHARAMISHWA BASI NI HARAMU