Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Alhamisi, 11 Oktoba 2018

Vipi utajijua kama una majini ya uganga?

Baadhi ya watu wana majini ila hawajuhi kama majini yao ni ya uganga au ni majini ya kuwalinda tu au ni majini wabaya wanaojifanya ni wasafi.

Leo hapa kwenye jukwaa la tibazetu nakuletea baadhi ya dalili za mtu mwenye majini ya Uganga.

Kuota Mara kwa mara una msomea mtu quran,dua,ama unamfanyia mtu matambiko ya asili.

Kuoteshwa dawa za miti yenye uwezo wa kutibu matatizo mbalimbali.

Watu kukufuata na kukueleza shida au matatizo yao yanayohitaji tiba mara kwa mara na wana matumaini na wewe ikiwa wewe sio mganga.

Kuota unaonyeshwa vibuyu au tunguli,kuota vitu vyenye rangi tatu nyeupe,nyekundu na nyeusi.

Kuota unapigana na kundi la watu na wakati mwingine kuota unapaa,Kuota umepandisha,Kuota unapiga  ramli,Kuota una mtibu mtu,Kuota jambo na likawa kweli,

NB:Ukiwa na dalili zaidi ya moja kati ya hizo basi wewe utakua na majini wa uganga ama wa asili ya afrika au wa kiarabu.