Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatatu, 17 Septemba 2018

TEVERI, ni kinywaji ambacho kimetokea kupendwa sana Burundi , Rwanda ,congo na hapa Tanzania

The vert, ( teveri) kahawa dawa , kinachopendwa katika vijiwe vya kahawa hasa Kigoma, Burundi , Rwanda

TEVERI, ni kinywaji ambacho kimetokea kupendwa sana Burundi , Rwanda ,congo na hapa Tanzania hasa mkoa wa kigoma, wao watumiaji wanakiita kama kahawa dawa . vijiwe vingi vya kahawa mkoani kigoma vianaagiza teveri kutoka Burundi na nyingine imeanza kulimwa hapa kukidhi hitaji. Kwa sasa ndoo ya lita 10 ikijaa hayo majani pasipo kushindilia ni 15,000/= Tshs. Kikombe cha kahawa kinauzwa kwa mia moja hadi mia mbili kutegemea upatikanaji. Teveri inachemshwa ikiwa mbichi au kavu na kunywa maji yake ambayo yana uchungu kiasi ,kama kahawa

TEVERI ni neno la kifaransa kwa kutamka yaani THE VERT, kwa kiingereza wanaita GREEN TEA . Kinywaji hichi kilikuwa introduced hasa Rwanda katika east Africa , kwa wananchi kuulima mmea huu , ambao mfumo wake wa upandaji ni kama matembele ya viazi .

TEVERI( the vert) au kwa jina lililopewa katika mkoa wa kigoma kahawa dawa , inadaiwa ni tiba ya magonjwa mbalimbali . kwa maelezo haya mimi nikaona ngoja nianze kufanya utafiti mdogo wa teveri . Nini hasa teveri na faida gani iliyomo katika teveri , kwa nini watu hawanywi kahawa wanakimbilia teveri.

TEVERI(THE VERT) GREEN TEA ni mmea unaojulikana duniani kote kwa jina la kisayansi CAMELLIA SINENSIS. Ukichemsha majani ya mmea huu , yana kiasi kikubwa cha chlorophyll( green pigment on leaves) yaani ule ukijani uliokolea , unatoka pamoja na polyphenol( virutubisho vilivyomo katika majani ), ambavyo ni antioxidant kubwa zaidi ya vitamin c , ambayo inazuia uzalianaji wa cell za mwili bila mpangilio.

POLYPHENOL ipo kwa wingi sana katika teveri ambayo ni antioxidant nzuri kwa kuzuia na kuharibu free radicals , yaani katika kuunda mwili wa mwanadamu sereially kunaanza na atoms,cell,tissue,organ kisha system (mwili). Free radicals ni atoms ambazo haziko sawa , kama haziko sawa maana yake muundo wa cell,tissue ,organ hautakuwa sawa, kuna athari. Atoms zikiharibika kibayolojia kinachoenda kutokea ni ugonjwa katika mwili na mambo ya kuzeeka kwa mwili .

FREE RADICAL zinahusishwa sana na uzee yaani ndiyo stop centre ya magonjwa .

THE VERT (TEVERI) GREEN TEA , kwa kuwa ina kiasi kikubwa cha polyphenol na kwa kuwa inaua free radicals , hivyo teveri inaonekana ni dawa zaidi ya dawa ,, kwa hoja hii ni kweli inatibu magonjwa mengi na kuzuia magonjwa kutokea mwilini .

Magonjwa ambayo yanaweza kuzuilika na TEVERI , hasa inapozingatiwa kwa unywaji wa bila kutumia sukari ni mengi mno kwa mujibu wa tafiti mbalimbali. Ila wengi wanahusisha na nguvu za kiume na mishipa kutokana na ule uchungu na wanakunywa kwa mrengo wa uzinzi, imebainika inatoa majibu chanya ndani ya ndoa kwa wale wenye ndoa.

TEVERI ikitumiwa ipasavyo inatibu magonjwa ya meno , kwa unywaji wa vikombe viwili kila siku . Magonjwa mengine yaliyokuwa confirmed ni kupunguza uzito , cancer, magonjwa yote ya moyo, mfadhaiko na stress, pressure ya kupanda , uyeyushaji wa chakula , allergy,cholesterol,magonjwa ya masikio , asthma , kutoa sumu ,flu and cold , majipu nk.

Kilichonishangaza ambacho kimenifanya niujue huu mmea ni kuwa wamebaini kuwa kiasi cha EGCG , yaani Epigallocetechin gallate katika mmea huu ambao unazuia ukuuaji na ueneaji wa virusi vya ukimwi katika mwili wa mwanadamu .

Chochote chenye faida nyingi kinaweza kuwa na hasara pia , sikutaka kuangalia faida tu , kwani kwa sisi tulio katika maswala ya kiroho dunia hii ni dunia ya uovu , shetani anatumia vitu watu kufanya ya kwake. HASARA ya kunywa teveri , kwa kuwa teveri ni jamii ya caffeine na ina caffeine , mtu yeyote anayekunywa teveri na yupo allergic na caffeine itamdhuru, kama insomnia ( kukosa usingizi), mvurugiko wa tumbo,kichefuchefu,kukojoa sana nk. TEVERI ukinywa inaondoa kiasi kikubwa cha madini chuma mwilini na kusababisha iron deffiency anemia , aidha inabidi uwe mlaji wa madini chuma kama nyama , mayai na fortified foods. Madhara ya upungufu wa madini chuma nayo ni makubwa , mfano kusikia kizunguzungu, mapigo ya moyo kwenda mbio, kupauka ngozi, kuvimba koo ,kutopumua vizuri nk.