Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumapili, 11 Novemba 2018

Utabiri wako wa leo kwa kutumia namba 1-9

Utabiri wa leo utachagua namba moja kati ya moja hadi tisa huruhusiwi kuchagua namba mbili yani labda tatu na tisa au kuchagua namba kumi
Pia katika kuchagua hutakiwi kufikiria andika tu namba inayokujia kichwani haraka
1
2
3
4
5
6
7
8
9
Ukishaandika sasa soma hapa maana ya hicho ulichokiandika
1 Hapo ulipo unawaza sana kuhusu pesa utaipataje au unasubiri kupewa pesa aidha unayodai au uliyoiomba nyota zinaonyesha pesa hiyo utaipata licha ya kuwa kuna changamoto nyingi.Tegemea kupata furaha zaidi siku ya leo na utapata marafiki wapya au utakutana na watu mliopotezana kwa kipindi kirefu ni kipindi cha furaha kwako au kwenu licha ya kuwa mnauguliwa lakini mgonjwa wako atakuwa sawa muda sio mwingi.
2
Leo kuwa makini utatofautiana na watu au utahitilafiana na watu au kukwazwa na watu hivyo ni vizuri kutulia  pia siku ya leo jitahidi kuwa mpole au mtu usiyejibizana ili kuepusha shari.Tegemea kupata faraja hapo badae kutokana na kazi au biashara zako.
3 Kuna fitna na migogoro katika ndoa au mahusiano yako mtagombana au mmeshagombana na mtu wako wakaribu na sababu kubwa ni usaliti au pesa ya matumizi.Ugomvi huu hauna ukomo ila kwa juhudi zako.Tegemea kufanikiwa sana katika maisha yako hapo mbele na hata kama watu wanaongea usisikilize wewe pambana utafanikiwa.
4 afya yako au ya ndugu yako anaeumwa atapona.Tegemea kupata matumaini  katika mambo yako.Pia mahusiano yatakurejeshea furaha upya na utapata fanaka zaidi.
5 Utafanikiwa au haja zako zitatimia .Leo wapigie simu marafiki au watembelee ndugu zako au rafiki zako kuna jambo utafanikiwa leo ni siku nzuri ya kukidhiwa haja zako itumie vyema.
6 kuna mtu mmegombana ugomvi wenu utaisha kabisa kabisa baada ya mwaka kuisha.Pia maradhi unayougua ni mtihani wako hayataisha kiwepesi pia unaonywa tabia ya kulipa kisasi hii ndio inayokukwamisha.Pia acha tabia ya chuki zisizo na msingi au wivu mbaya wakimaendeleo pia maneno maneno hayafai jitahidi kuwa mstaarabu.
7
Punguza tabia yako ya udanganyifu na kuongopa ili ufanikiwe hii itakukwamisha mno katika maswala yako yakiuchumi.Pia punguza starehe au mambo ya raha pangilia mipango yako utafanikiwa.Hali yako ya kupotelewa pesa ina sababu za msingi ndani yake unashauriwa kufanya ibada na kuwasaidia wenye shida.
8 Hapo ulipp una hasira au kuna mtu amekuudhi pia huna amani sana na hali ya kiuchumi unayoipitia kwa sasa lakini yote yanapita safari hii ina ukomo.
9
Tegemea fanaka katika mambi yako na safari yako itatimia vizuri na utafarijika sana uendapo licha ya kuwa mwisho wake hautakuwa mzuri sana kuna makwazo yatatokea huko ila yavumilie.Huu mwaka utakuishia vizuri mno tegemea kupata bahati kubwa.
Kwa utabiri.kusoma nyota,tafsiri za ndoto,dawa na tiba mbalimbaji pamoja na ushauri wasiliana na tibazetu.
0764995259.
0657739713.
whatsapp and call.
Email.
Tibazetutz@gmail.com.