Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Ijumaa, 23 Novemba 2018

abrus precatolius ni mmea wa dawa wa tiba na wa kukuambukiza nguvu za asili za miujiza

0764 995259.
0657 739713.
whatsapp.

Abrus precatorius ni mmea wa dawa ya familia ya fabaceae ambao hutibu magonjwa ya binadamu ya kibakteria na pia kuambukiza nguvu za asili za miujiza za ulinzi dhidi ya uchawi.

Majani mabichi ya mmea huu hutwangwa na kuanikwa hadi kukauka kisha hutwangwa tena kupata unga wake ambao kila baada ya masaa nane mgonjwa wa magonjwa ya bakteria anapaswa anywe kijiko kimoja cha chai cha unga huo kwenye maji ya kuchemsha ya kikombe kimoja cha chai. Hii ina maana atakunywa mara tatu ndani ya masaa 24 kwa siku tano na kufanikiwa kuponyesha kikohozi, kuharisha, upele na kazalika.

Kunde za Abrus precatorius hutengenezwa cheni ya kuvaa shingoni, kiunoni na mkononi kwa ajili ya kuambukiza nguvu zake za asili za miujiza zenye ulinzi mkali dhidi ya nguvu za kichawi.

Baada ya viongozi wa imani mbalimbali za dini kugundua uwezo mkubwa wa nguvu za ulinzi dhidi ya nguvu za kichawi walishawishi mashirika na makampuni yao ya kidini kutengeneza rozari kwa wakristo wa Roman Katoliki ili waitumie kama ulinzi ulioaminika kuwa ni ulinzi wa Bikira Maria wakati ukweli wake ni ulinzi uliotokana na kunde za mmea huo.

Kunde za Abrus precatorius zina sumu kali sana ya kuuwa uhai wa binadamu. Kutokana na sumu yake kunde hizo Abrus precatorius zimeonywa kutotafuna hata punje moja kwa sababu punje hiyo moja inatosha kupoteza maisha ya binadamu.

Majani ya mmea huu yana kiasi kidogo cha nguvu za asili za miujiza zenye uwezo wa kupigana na nguvu za uchawi. Hata hivyo wamasai, wairaq, wabarabeig na wasandawe wanategemea sana mmea huu kujilinda dhidi ya nguvu za kichawi.

Kwa wale wanaotumia majani ya mmea huo kwenye chai kwa miezi miwili mfululizo wanawezeshwa ulinzi wenye uwezo wa kupigana na uchawi.