Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Alhamisi, 30 Mei 2019

Sheria ya kwanza ya kugundua mimea ya dawa za nguvu za asili za miujiza


Sheria ya kwanza ya kugundua nguvu za asili za miujiza inashangaza sana kwa vituko vyake vinavyojifichua kwenye utambuzi wa ufahamu wa mgunduzi.

Sheria hii inatofautisha mimea ya dawa inayoonekana mchana tu lakini usiku haionekani hata uwe na tochi yenye mwanga mkali kiasi hutaiona kamwe. Kama ilivyo kwa inayoonekana mchana tu, ipo mimea mingine inayoonekana usiku tu lakini mchana haionekani kamwe.

Zoezi ya namna ya kuingundua mimea hiyo unapaswa kuchukua upanga na kuweka alama kwenye mimea kwa mstari ulionyoka kwa umbali wa kilomita moja wakati wa mchana huku ukibaini idadi ya mimea uliyowekea alama.

Utakavyorudi usiku utagundua asilimia 3 hadi 15 haitaonekana. Ili kuijua isiyoonekana usiku unaiwekea alama kwa mara ya pili mimea yote iliyoonekana usiku huo.

Utapaswa kurudi mchana wa siku ya pili ili kuitambua mimea yenye alama moja tu ambayo ilikosa kuwekewa alama usiku wa jana yake. Mimea michache itakayokosa alama ya pili ambayo itaonekana mchana ndiyo ni mimea ya dawa za nguvu za asili za miujiza.

Vivyo hivyo zoezi linapaswa kurudiwa kwa upande mwingine wa pori ili kubaini mimea inayoonekana usiku tu lakini mchana haionekani. Utaratibu ni uleule wa kuweka alama kwa mstari ulionyoka wa kilometre moja.

Usiku huo ndio utakuwa ni mwanzo wa zoezi lako wa kuweka alama mimea yote kwa kutambua idadi yake. Utakapofika mchana wa siku ya pili utagundua asilimia 3 hadi 15 haitaonekana mchana huo licha ya jua kali.

Kwa hiyo utalazimika kuweka alama kwa mara ya pili ili uweze kubaini mimea yenye alama moja usiku ukifika. Kwa hiyo mimea yote utakayoigundua kuwa na alama moja usiku ndiyo yenye nguvu hizo za asili za miujiza.

Mtabibu baada ya kugundua mimea inayoonekana usiku na mchana haionekani na ile inayoonekana mchana usiku haionekani anapaswa kuifanyia utafiti na uchunguzi mkali iwapo kama inaweza kuratibiwa kwenye dozi ya kuliwa, kuogea, kupaka na kujifukiza kama pafumu au mvuke.

Kujiambukiza nguvu za asili za miujiza kutoka kwenye mimea kama hiyo kunamwezesha mtumiaji kutoonekana usiku au mchana kwa kadiri atakavyojipanga na dozi za mimea hiyo.

Shukrani.