Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatatu, 3 Juni 2019

Sheria ya pili ya ugunduzi wa dawa ya nguvu za asili za miujiza


Sheria ya PILI  ya ugunduzi wa mimea ya dawa za nguvu za asili za miujiza inahusishwa mimea yenye uwezo wa kujibadirisha kuwa maji, moto, ardhi na hewa.

Sheria hii ya pili ndiyo ni elimu ya nguvu za asili za miujiza iliyoangamizwa na wakoloni wa kijerumani  kwa kunyongwa wahenga mashujaa   mababu zetu wa kingoni waliokuwa na elimu hiyo ili isirithishwe kamwe kwa vizazi vyetu.

Sheria hii ndiyo iliyowawezesha mababu zetu kuweza kubadirisha risasi kuwa maji. Hata hivyo bado sheria hiyo inafanya kazi kwa baadhi ya mimea kuweza kuambukiza nguvu za asili za miujiza kwa binadamu akaonekana kuwa moto.

Namna ya kugundua au kutambua mimea inayoambukiza moto wa nguvu za asili za miujiza
1)Kwa mtu yeyote mwenye nguvu za asili za miujiza akiona mara kwa mara mmea wa aina moja umevirigwa na nyoka kutoka mkia chini kichwa juu katika sehemu mbalimbali za mapori basi ajue kuwa mmea huo anaambukiza moto wa nguvu za asili.

Nyoka mwenye nguvu za asili hupenda kuvutiwa sana kupumzika kwenye mmea huo wa moto za nguvu za asili. Siri ya mmea wa moto za nguvu za asili za miujiza imevuja sana kwenye makabila na mataifa mengi duniani.

Ndiyo maana ya alama hiyo hupendwa kuwekwa kwenye noti za fedha za mataifa mbalimbali.

2)Alama ya pili ya kugundua mmea wa moto wa nguvu za asili za miujiza ni kuharibu vifaa vinavyotumika na wanadamu kukatia mti huo au kuung'oa mti huo kwenye ardhi yake ikiwa pamoja na kusababisha kifo kwa anayeudhuru kwa namna ya vitendo hivyo.

Na kama uking'olewa kwa bahati mbaya hukutwa umeoteshwa siku ya pili kama ulivyokuwa hapo nyuma.

Kiwango cha moto wa nguvu za asili za miujiza kinapishana. Mmea mwingine ina moto wa chini. Wakati nyingine ina moto mkubwa na mkali sana wa nguvu hizo za asili za miujiza.

Pia miti yenye moto wa nguvu za asili za miujiza hutumika kama ulinzi na balaka kwa kuambukiza nguvu zake za asili za miujiza kwa kutengenezea moto wa kupikicha kati ya kitiji chake na gogo lake na kisha kuugawa moto huo kwenye kaya za ukoo husika.

Licha ya kuambukizwa nguvu zake za asili za miujiza kupitia kutengenezea moto, mmea wa moto za nguvu za asili za miujiza hutumiwa mizizi yake iliyochemshwa kuogea na kujifukizia mvuke wake ili kujiwezesha kujiambukiza nguvu hizo.

Katika kabila la kingoni kuna mmea huo wenye nguvu za kati za moto wa nguvu za asili za miujiza unaoitwa mhoro. Nasikitika kwa sasa hautumika kimila kama mmea wa baraka ya ulinzi dhidi ya uchawi na majini kwa kugawa moto uliotengenezwa kupitia mmea huo.

Wakati mwingine aina ya mmea wa moto wa nguvu za asili za miujiza hulindwa na nyoka mkali sana ambaye kamwe hawezi kuuwawa. Pia ardhi iliyootesha aina hiyo yenye moto mkali wa nguvu za asili za miujiza huzuiriwa kimazingara au kimazingahombwe kuweza kutumika kwa shuguli za mashamba, ujenzi wa nyumba, ujenzi wa barabara na madaraja na kazalika.

Ili kuitumia ardhi yenye mmea wa moto mkali wa nguvu za asili za miujiza wahusika wa ardhi hiyo wanawajibika kutambika kwa ahadi ya kuhamisha nyoka huyo kumpeleka kwenye ardhi nyingine yenye mmea wa moto mkali za nguvu za asili za miujiza.

Namna ya kumhamisha nyoka huyo huchukua dawa iliyochemshwa ya mmea huo kutoka sehemu nyingine na kuitiririsha michirizi midogo sana kama ya sufuria iliyotoboka kutoka eneo linalolindwa na nyoka huyo mpaka eneo lingine la msitu uliootesha mmea mwingine wa moto mkali wa nguvu za asili za miujiza.

Nyoka atapita kwa kufuata mtiririko wa michiriza ya dawa mpaka ulipo huo mmea wa moto mkali wa nguvu za asili za miujiza. Nyoka akishaonekana kwenye eneo lingine analohitajika kuhamia inatengenezwa dawa nyingine ya kukatisha mahusiano ya kurudi alikotoka ili ardhi yake iweze kutumika kwa shughuli zilizokusudiwa.

Nitawaelimisha kwa posti maalumu kuhusu nyoka wa nguvu za asili za miujiza na namna anavyotumika. Ujinga wa namna ya kujinga na uhatarishi wa nyoka umepotoshwa maana na umuhimu wa nyoka wa kawaida na wale wenye nguvu za asili za miujiza kwa wanadamu wengi duaniani.


Kazi njema! Shukrani.