Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatatu, 29 Mei 2017

jinsi wachawi wanavyoweza kumteka jini wa mwilini mwako anayekusaidia

Habar zenu wapendwa ndugu zangu


jana nilikutana na mgonjwa mmoja mwenye shida kama hii,hivyo nimeona nishee uzoefu na nyinyi kidogo juu ya jambo hili.

kawaida kuna watu ambao wanakuwa na majini wao wa mwilini(jini wa kichwa)majini hawa mara nyingi huwa ni majini wa asili na mara nyingi wapo kwa ajili ya ulinzi na kumsaidia kiti wake katika mambo mbalimbali ya hapa na pale,katika hali kama hii hata kama wachawi watakusudia kumfanyia jambo baya mtu mwenye majini wa namna hii wanapata tabu sana sana sana na wakati mwingine hufikia hata kuhatarisha maishao yao kwan huweza hata kuuwawa na majini hawa walinzi.

Saasa wachawi wanapokuwa na shida sana ya kukudhuru na wakigundua una ulinzi huo wa kijini wenye nguvu kubwa ya kuwasumbua kutokutimiza malengo yao wanatafuta njia ya kumteka jini huyo na kumfunga kabisa ili asiweze kutawala vyema rasio yake mwilini mwako na hapo watakuwa na uwezo wa kukufanyia jambo lolote wanalotamani na likakupata kama linavyokusudiwa 

ili kuweza kumfunga jini wako huyo wanafanya hivi
Kwanza ni lazima wapate athari yako(yaani nguo,nywele,kucha n.k)baada ya kupata vitu ivo wanachukua kifaranfga cha kuku kilichoanguliwa leoleo wanakinyonga na kukifunga shingoni kwa kitambaa cheusi,chekundu ama cheupe yategemea na jambo wanalokusudia kwako

baada ya hapo mzigo huo huwakilishwa kwenye kikao cha wachawi na kuanza kufanyiwa mambo ya kichawi na kisha ni lazima uchawi huo uje kufukiwa hapo nyumbani kwako nyuma ya nyumba ama kwenye njia kubwa ya kuingilia hapo kwako.hili huwa ni jini la kichawi lenye nguvu kubwa ambalo hutegeshwa hapo ili likamilishe kazi hiyo.

baada ya hapo utahisi dalili zifuatazo
~kutoota ndoto na ukiota hata ukishtuka huzikumbuki tena tofauti na ilivyokuwa mwanzo
~kuumwa umwa mara kwa mara
~kufunga hedhi kama ni  mwanamke
~kama una mimba ya miezi kadhaa inakomea hapo na hujifungui tena hata ipite miaka mingapi unabeba mimba tu hiyohiyo lakini hujifungui
~kuharibika mimba mara kwa mara
~kuwa na mimba na baada ya muda ukienda kupima unaambiwa hauna.
~kuota sana tendo la ndoa na mwanaume au mwnamke wako 

TIBA YAKE
Hili kumrudisha jini huyu mlinzi ni lazima apatikane mganga mwenye uwezo mkubwa wa kutoa majini,kwana anatakiwa aitwe huyo jini maradhwi aliyetumwa na atavutwa kwa nguvu na akipanda tu anapigwa kombora moja la nguvu anapotea,pia waganga wengine mgonjwa akipandisha jini maradhw humpiga kichwa na kumchukua jini yule anamuingiza mwilini mwake na majini ya mganga yanammaliza .