Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Alhamisi, 10 Agosti 2017

mganga wa kienyeji amchinja binti na kukichoma moto kichwa chake

Taarifa zilizotufikia hapa zinaeleza kuwa mama mmoja ambaye ni mganga wa kienyeji (jina halijafahamika)amefanya mauaji ya mtoto wa kike. Tukio hilo limetokea juzi maeneo ya Chang'ombe, wilaya Chamwino mkoani Dodoma.

Tukio hilo la kusikitisha limetokana na imani za kishirikina ambapo mganga wa kienyeji amemchinja binti mwenye umri kati ya miaka 12 hadi 16 na kisha akakichoma kichwa cha binti huyo akiamini kuwa ni kafara ya kuwatibu wateja wake waliokuwa wakitibiwa nyumbani kwake.

Kufuatia hali hiyo watu 17 wanashikiliwa na Jeshi la polisi akiwemo mganga huyo pamoja na mume wake.


sote kwa pamoja tunapaswa kupiga vita unyama wa namna hii na kuweza kutoa taarifa mapema kwa vyombo husika 

poleni wafiwa.