Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumapili, 17 Juni 2018

Utabiri wa leo tarehe 17/06/2018

Punda(21 march-20 April)
Siku ya leo jihadhari na migogoro na watu na ukikutana na mtu kavaa vazi jekundu tegemea kupokea taarifa za kukukera au kukuudhi, pia siku ya leo jitahidi kuwa mpole na aliyekuwa adui yako wa muda mrefu anataabika (amepata udhalili)

Ng'ombe(21 april-21 may)
Siku ya Leo tegemea kupata taarifa nzuri kutoka mbali. Utapata ugeni na faraja kutoka kwa ndugu wa mume/mkeo, pia ukikutana na mtoto analia basi tegemea kukutana na mtu mliegombana bila sababu ya msingi na mtakuwa marafiki upya.

Mapacha(22 may-21 June)
Leo tafuta ulichokipoteza utakipata hata kama ni mtu mligombana mtaelewana na mambo yataenda sawa, tafuta karafuu jifukize kupata wepesi katika mambo yako, pia kuna dalili za mtu kukuhitaji kimahusiano jihadhari nae sio mtu mzuri kwako.

Kaa(22 june-22 July)
Siku ya leo Nyota zinaonyeaha kuna dalili ya wewe kupata ugeni au kusafiri jitahidi kuwa mkarimu na mchangamfu zaidi kuna vitu utajifunza na mitihani uliyonayo utaifuzu, dalili za kuthaminika zitajionyesha kwanzia hii leo kuwa makini na Mali zako na ujizuie na safar za usiku

Simba(23 july-21 august)
Kuna dalili za kupokea taarifa mbaya kutoka nyumbani au kazini. Mambo yako yatavurugika na dalili umeshaziona kwanzia wiki iliyopita migogoro ndani na kazini haioshi tafuta suluhu mapema,

Mashuke(22 august-22 September)
Afya yako au mgonjwa wako itakuwa nzuri tegemea kupokea habari ya mwaliko au ugeni hizuni uliyokuwa nayo itatowwka bila kutarajia.

Mizani(23 september-21 October)
Leo akitokea mtu kukuomba msaada wa kipesa kimali kiushauri mshauri mtu huyo kuna kheri kubwa na haja zako zitatimia na wepesi juu ya jambo lako utapatikana

Ng'e(22 october-21 November)
Jihadhari na mikutano ya watu au vikundi siku ya leo unaweza kupata aibu au fedheha au kero na maudho, Nyota zinaonyesha kuna vitu vingi unavyoviwaza huvielewi utavipatia majibu sahihi ndani ya wiki hii, pia usipokuwa na maamuzi yako waweza kuingia kwenye mtego mbaya(Fanya uamuzi sahihi kabla ya kufanya makubaliano yoyote vinginevyo utapata hasara).

Mshale(22 november-21 December)
Mambo yako kimahusiano yatakuwa mazuri na dalili za kupokea pesa zitapatikana. Makosa uliyoyafanya hapo awali jishushe, pia jihadhari na uongo utakupotezea muelekeo wako.

Mbuzi(22 december-19 January)
Mambo yako yatazidi kuvurugika jitahidi kutafuta ufumbuzi kadri inavyowezekana kuwa msiri na mipango yako sio kila rafiki ni rafiki wengine ni maadui waliojificha biashara au Kazi zako zitayumbayumba jitahidi kutumia ubani mushtaka kuchoma na kuchemsha na kunywa kidogo.

Ndoo(20 january-18 February)
Safari utakayoipata itakufundisha mengi na siri nyongi utazifahamu na timiza ahadi zako ulizoahidi zitatimizwa ahadi ulizoahidiwa katika mambo yako usitegemee kupokea pongezi tu bali tegemea na kukosolewa ni hali ya binadam stahmil ndo hali ya maisha na n mapito tu.

Samaki(19 february-20 march)
Leo kuwa makini na maongezi yako na uwe making zaidi usijekujichanganya katika siri zako, pia kuwa makini na vitu vyako leo unaweza kupoteza kitu cha thamani au pesa au simu pia mchinguze mwenzako kuna siri anayo kakuficha jitahidi asijue una mchunguza utaukosa Ukweli