Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumanne, 15 Septemba 2015

UCHAWI WA MAPENZI

Hii ni mojawapo kati ya aina 410 za uchawi,uchawi huu ulikuwepo tangu Enzi hizo ila kwa sasa ndiyo umepamba moto zaidi.Na uchawi huu sanasana hufanyiwa wanaume ingawa na wanawake pia ni waathirika lkn si sana.

Katika uchawi huu mwanaume anafanywa awe anampenda mwenza wake katika mapenzi makubwa mno na ya ajabu kabisa,kwani hata mwanamke huyo akiwa anafanya mambo maovu katika jamii basi kidume aliyefanyiwa uchawi huu anakenua tuu meno na kuona kila kitu ni sawa hata kama jamii yote inayomzunguka itamkanya basi yeye huwaona kama ni wapambe nuksi wanataka kumuharibia starehe zake,kumbe tayari ameshafanyiwa tiwaalah bila ya mwenyewe kujitambua.

                         
                                      JINSI WANAVYOFANYA UCHAWI HUU
Mara nyingi katika maisha ya ndoa hutokea khitilafu baina ya wanandoa,na haya ni mambo ya kawaida na huisha haraka na maisha yakachukua mkondo wake.Lakini muna baadhi ya wanawake wasioweza kuvumilia hayo hivyo hukimbilia kwa wataalam wa ulimwengu wa giza kwa ajili ya kuwatengenezea ili wawe ni wenye kupendwa sana na wenza wao na wawe na uwezo wa kumuamrisha chochote naye awe ni mwenye kutii bila kuuliza chochote.

Hapa mtaalam huyu anaweza kuagiza athari ya mtakiwa iwe ni nguo,kitambaa,kofia,shati,chupi n.k kwa sharti kiwe kimebeba jasho la mwanaume anayetakiwa yaani kisiwe kipya au kimefuliwa,na hapo anachukua nyuzi saba katika nguo ile anazipuliza mara kadhaa na anasema maneno Fulani[sitoyaweka hadharani wengine wasije wakafanya].kisha anazifunga mafundo saba na kwenda kuizika kwenye jumba lililohamwa.

Pia wakati mwingine uchawi huu unaweza fanyiwa katika maji au hata chakula,na iliyo kali zaidi ni ile wanayoifanya kwa najisi kama vile damu ya hedhi kisha kulishwa mhusika kupitia chakula chake,au kinywaji au hata pafyumu yake.


                           DALILI ZA ALIYEFANYIWA UCHAWI HUU
Mtu aliyefanyiwa uchawi huu huwa na dalili zifuatazo

1.Mahaba na mapenzi yaliyozidi kupita kiasiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii

2.Kujikuta anapenda muda wote afanye nae mapenzi

3.Kutoweza kuwa mbali[hata ukisafiri kikazi unatamani urudi nyumbani hata kabla ya kumaliza]

4.Shauku nyingi ya kumuona

5.Kumtii kiupofu[hata afanye mambo mabaya na maovu unaona sawa]


                       ATHARI ZA KINYUME ZA UCHAWI HUU
1.Mara nyingine kama utaalam wa mfanyaji ni mdogo mume anaweza kuugua sababu ya uchawi huu

2.Mara nyingine kama utaalam wa mfanyaji ni mdogo huwa kinyume chake,mume huweza kumchukia hadi yeye aliyeenda kumfanyia ili ampende na hii ni kutokana na wengi wanaofanya haya mambo kutojua misingi ya uchawi huu

3.Mara nyingine mke huweza kumfanyia uchawi mchanganyiko ili aweze kuwachukia wanawake wote na ampende yeye tu,na hii huweza kupelekea mume kumchukia hata dada yake,mama yake,shangazi yake na miongoni mwa jamaa zake wote wa kike.

4.Mara nyingine pakikosewa mume huweza kugeuka na kujikuta anawachukia wanawake wote hadi mwanamke ambaye ndiye ameenda kumfanyia[iliwahi tokea mwanaume mmoja alimchukia mkewe akamuacha na yule mke aliporudi kwa mtaalam wake bahati mbaya akakuta ameshafariki


kwa tiba na ushauri
docter Ally Chambas
+255 653 532036
+255 764 995259
au barua pepe
Tibazetutz@gmail.com