Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumamosi, 5 Septemba 2015

UNAJUA NINI KUHUSU KUJAMBA?

Kujamba kunasababishwa na kubanwa kwa hewa ambazo zinaweza kutoka mwilini kwa njia nyingi,hewa hyo huweza kuwa tuliimeza wakati wa kula au kunywa,au huweza kusababishwa na gesi tumboni,au gesi ambazo huzalishwa na kemikali ktk utumbo au hata bacteria.

Ushuzi anaojamba mtu hubeba asilimia59 ya gesi ya nitrojen,asilimia21hydrojen,na asilimia 9 ni carbon dioxide,asilimia 7 ni methane na asilimia 4tu ndyo oxgen.....ni asilimia moja tuu ndyo hubeba hydrojen sulfide na mercaptans ambayo ndyo ina sulphur ndani yake na hii sulphur ndyo hufanya ushuzi utoe harufu mbaya.

Kujamba mara nyingi huambatana na sauti na hii ni kutokana na vibration katika njia ya haja kubwa na ukubwa wa mlio wa kujamba hutegemea na presha inayosukuma gesi itoke nje na  na uimara wa misuli ya njia ya kubwa,

                                     KWANINI USHUZI HUTOA HARUFU MBAYA
Harufu mbaya ya ushuzi hutegemea na ulaji wa mtu husika kwani vyakula vyenye sulphur kwa wingi ndyo husababisha hali hii vyakula hivyo ni kama>>maharage,kabichi,soda na mayai na bin adam ana uwezo wa kujamba mara 14 kwa siku,mtu mzima anaweza kuzalisha hata nusu lita ya ushuzi kwa siku na inasemekana mtu akijamba mfululizo kwa kipindi cha miaka6 anaweza kuzalisha nishati ya kutosha kwa ajili ya kutengeneza bomu la atomiki......

Ushuzi husafiri mwendo wa futi10 kwa sekunde na harufu yake huanza kusikika sekunde10 hadi 15 baada ya mtu kujamba hyo ni kwa sababu huchukua muda mrefu mpk harufu kuifikia pua

Kuna watu hupenda mchezo wa kujizuia kujamba pale tuu anapohisi kufanya hivyo,ingawa madaktari hawajakubaliana kwa pamoja lkn inaonyesha kujizuia kujamba kunaweza kuhatarisha afya yako kwani kunaweza kusababisha tumbo kujaa gesi na hata ugonjwa wa bawasiri

Kuna baadhi ya tamaduni huwa kujamba hawaoni haya, hata kujamba hadharani na pia mtu anapojamba hufurahia tendo hilo. mfano mzuri kabila la yanomami huko america ya kusini kwao husalimiana kwa kujamba,na china unaweza kujikuta unapata ajira ya kunusa ushuzi,Katika roma ya zamani Mfalme  claudius akihofia kwamba kujizuia kujamba inaweza kuwa hatari kiafya alipitisha sheria kwamba ni ruhusa kujamba kwenye mikusanyiko ya watu na hata sehemu zao heshima km bungeni nk..

Ushuzi pia huweza kuwasha moto,kama nilivyosema hapo juu methane na hydrojen inayozalishwa na ushuzi ina uwezo wa kuwasha moto

pia mchwa ndye mdudu ambaye hujamba sana kuliko wanyama wote,ukiubana ushuzi mchana basi ujue utakutoka tuu usingizini,