natumai hamjambo na mnaendelea vyema na harakati za kila siku katika ujenzi wa taifa.
leo naomba niwajuze faida mbalimbali zitokanazo na majani ya mpera
Mapera ni matunda ya msimu yenye wingi wa vitamin A na C,Madini ya pottasium ,nyuzinyuzi za fiber na lycophene ambavyo vyote hivi ni muhimu kwa afya ya mwanadamu
FAIDA ZA MAJANI YA MPERA
1.Chai ya majani ya mpera inasaidia mwili kuwa stadi,inasaidia madini ya cabohydrates isigeuzwe kuwa sukari mwilini hivyo kupunguza hamu ya kula
2.Chai ya majani ya mpera pia husaidia kushusha kiwango cha sukari mwilini na kuzuia mwili kuondoa insulini hivyo wagonjwa wa sukari wanashauriwa kuitumia mara kwa mara
3.Chai ya majani ya mpera hupunguza lehemu mbaya mwilini bila kudhuru lehemu nzuri
4.Chai ya majani ya mpera ina uwezo wa kudhibiti vijidudu vya magonjwa mwilini hasa vinavyosababisha magonjwa ya kuharisha na kipindupindu
5.Chai ya majani ya mpera hutuliza mchafuko wa tumbo na husaidia kukabiliana na madhara yaletwayo na sumu za vyakula mbalimbali vya kila siku
6.Chai ya majani ya mpera inatibu matatizo ya pumzi na kukohoa
7.Majani ya mpera hutibu uvimbe wa fizi,maumivu ya kinywa na meno kwa kutafuna majani yake
8.Chemsha majani 10 ya mpera kwa maji glass mbili na nusu mpaka ibaki glass moja na nusu kunywa kutwa mara moja kwa siku 21 na zaidi hutibu matatizo ya homa ya dengue
9.Chai ya majani ya mpera hutibu kansa na prostrate kwa wanaume,pia hutibu matatizo y
10.Ponda majani ya mpera na weka kwenye kidonda kwani huzuia maambukizi,kwa maumivu ya nje ya sikio tia matone ya chai ya majani ya mpera iliyopoa sehemu iliyoathirka
11.Kwa muwasho unaosababishwa na aleji ponda na paka majani ya mpera eneo linalowasha
12.Ukiumwa na mdudu ponda majani ya mpera ubandike ni tiba nzuri
13.Pia hutibu mba na chunusi kwa wingi wake wa vitamin C
14.Kuondoa madoa meusi kwenye ngozi ponda majani ya mpera changanya na maji kidogo na ujipake
15.Kwa matatizo ya kukatika kwa nywele chemsha majani yakishapoa kanda taratibu kwa dakika 15 kwenye kichwa kisha acha kwa dakika 30 na uoshe kwa maji safi bila sabuni