Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumapili, 13 Septemba 2015

ZIJUE FAIDA KUMI ZA MAFUTA YA ZAITUNI

Mafuta ya zaituni yana faida kubwa sana katika kutibu maradhi mbalimbali yanayotukabili binadamu,leo ntakupatia faida kumi za mafuta ya zaituni katika kutibu maradhi mbalimbali ya mwili wa binadamu.

                                                               1.MAUMIVU YA TUMBO
~Kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku,kwa muda wa siku7 hadi siku11

                                       
                                                         2.KUFUKUZA MASHETANI MWILINI
~Yasomee kisomo cha rukya mgonjwa ajipake mara moja kwa siku,pia atafune vitunguu thaumu punje3 wakati wa kulala kwa siku 40


                                                                            3.MAFUA
~Paka juu ya pua na ndani ya matundu ya pua mara3 kwa siku utapona mafua


                                                             4.VIDONDA VYA TUMBO
~Tia vijiko viwili vikubwa vya mafuta ya zaituni kwenye uji,mara mbili kwa siku kwa muda wa siku 90


                                                       5.ALIYEKUNYWA SUMU
~Pia hutumika kama huduma ya kwanza kwa mtu aliyekunywa sumu,anywe mafuta ya zaituni ujazo wa nusu kikombe cha chai kisha muwaishe hospitali


                                                         6.WADUDU TUMBONI
~Pia mafuta haya hutumika kuua wadudu wabaya waliopo tumboni kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku kwa muda wa siku7


                                           7.KUONGEZA NGUVU ZA KIUME
~Kunywa kijiko kimoja cha mafuta ya zaituni kwa siku,na ujichue uume kwa mafuta ya zaituni yaliyochanganywa na kitunguu thaumu kwa muda wa siku7 hadi 11


                                           8.UGONJWA WA KUSAHAU
~Paka mafuta haya katika paji la uso kutwa mara mbili,pamoja na kunywa kijiko kimoja cha chai mara moja kwa siku...siku saba hadi kumi na moja

                                                        9.DEGEDEGE
~Ajipake mwili mzima mafuta ya zaituni yaliyosomewa rukya,mara mbili kwa siku kwa muda wa siku 7 hadi 21


                                        10.KUKOJOA KITANDANI
~Kupakaa mafuta ya zaituni mwili mzima kutwa mara mbili,huku akilamba matone mawili ya mafuta hayo kwa muda wa siku7 hadi 21 husaidia kuondosha tatizo la kukojoa kitandani kwa watoto na wakubwa