Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatano, 2 Septemba 2015

TIBA ZA ASILI ZA VIDONDA VYA TUMBO

                                                                              MAJI
Tiba ya maji inafaa sana kwa kutibu vidonda vya tumbo vilivyo katika hatua ya awali,

Mgonjwa anapaswa kunywa lita moja ya maji safi na salama alfajiri kabla ya jua kuchomoza na kabla hajapata kifungua kinywa,kisha mgonjwa ni lazima asubiri kwa dakika 45 mpaka saa ndipo apate kula chakula cha asubuhi

Wakati wa mchana mgonjwa anapaswa kunywa tena maji lita 1 dakika45 kabla ya kupata chakula cha mchana,na asinywe maji yoyote baada ya kumaliza kula chakula hicho cha mchana  kwa dakika 45.

Wakati wa usiku mgonjwa anapaswa kunywa tena maji lita1 dakika45 kabla ya kula chakula cha usiku na akae dakika 45 kabla ya kwenda kulala.

Tiba hii huchukua muda wa siku10 mpaka mwezi mmoja kabla ya kupona kwa vidonda vya tumbo vilivyopo katika hatua ya awali.kipindi chote hiki mgonjwa ni lazima kufuata utaratibu na kuacha vyakula vyote ambavyo vinamuathiri mtu mwenye vidonda vya tumbo


                                                                            KABEJI

~Kunywa juice ya kabeji mbichi baada ya kuikatakata vipande na kuisaga kwenye mashine[blenda]tia kwenye kikombe cha chai kunywa mara4 kwa siku.Tiba hii huweza kutibu tatizo la vidonda vya tumbo kwa siku10......................................................................................................................................



                                                                  ASALI

~Asali ina chembechembe za asili zenye kuua bacteria na virusi ambavyo vina uwezo wa kuua helicobacter pylory ambao ni wadudu wanaosababisha ugonjwa huu wa vidonda vya tumbo,hivyo asali ina uwezo wa kutibu vidonda vya tumbo.kingine ni kwamba asali ina uwezo wa kulainisha umio,mfuko wa chakula na utumbo hivyo huweza kufunika vidonda vilivyopo tumboni.Kutokana na kufunika vidonda maumivu ya kuchoma,pamoja na dalili zingine za vidonda vya tumbo hupungua

~Asali pia huweza kuondoa uvimbe na kusafisha vidonda ambavyo hujitokeza kwenye njia ya chakula.Asali inayopaswa kutumika kwa kusudio hili inapaswa iwe mbichi na isiwe imeongezewa kitu kingine...kula vijiko vitatu vya asali kwa siku.


                                                       VITUNGUU THAUMU
Viungo hivi ni tiba nyingine inayofaa sana katika kutibu vidonda vya tumbo kutokana na kemikali zinazoua wadudu pamoja na virusi zilizomo ndani yake, na hivyo huweza kupambana na kuua bacteria wanaosababisha vidonda vya tumbo.viungo hivo hufahamika katika kusaidia kutibu vidonda vya tumbo hata pale vinapotumika vikiwa vimechanganywa na  vyakula vingine kutokana na nguvu nyingi iliyomo ndani yake pamoja na chembechembe zenye kuamsha na kuboresha mwili zilizomo ndani ya kitunguu thaumu ambazo huwezesha kuukinga mwili dhidi ya maambukizi kama vile vidonda vya tumbo.Kula punje3 mpaka 4 za kitunguu thaumu ambacho kimechanganywa na vijiko2 vya asali kwa kila siku.


                                                                        JIBINI NGUMU
~Kula jibini ngumu husaidia kufunika vidonda vya tumbo hivyo hupunguza maumivu makali ya vidonda kwa  mtu mwenye tatizo hili anashauriwa kula kwa wingi na kwale ambao vidonda vyao vina muda mfupi tangu kujitokeza hupotea baada ya matumizi ya muda mrefu ya chakula hiki...................................