Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumapili, 18 Oktoba 2015

TIBA YA JINNI GHAWWAASWI KWA KUTUMIA MISKI





Fahamu kuwa majini wengi wenye kuwadhuru watu na kuwasababishia matatizo mbalimbali awe ametumwa na mchawi au ni mapenzi yake mwenyewe tuu shetani huyo,huwa hawapendi vitu vyenye harufu nzuri

Majini hawa wengi hupenda vitu vyenye harufu chafu,najisi na mambo mengine yote machafu machafu

Miongoni mwa dawa ambazo zimewasaidia watu wengi sana kwa msaada wa mwenyez mungu ni MISKI

Miski huweza kumsaidia mtu kwa uwezo wa mungu kumuondolea tabu anazozipata kutoka kwa majini wa aina nyingi ingawa kwa jinni Ghawwaasi ndyo uhathirika zaidi

JINNI GHAWWAASW

 huyu ni ambaye hupendelea sana kukaa sehemu za bahari,chemchem za maji,mito,maziwa na mabwawa pia

DALILI ZA MTU MWENYE JINNI HUYU
  
~kuwashwa mwili mzima na ukijikuna unatoka malengelenge

~kuvimba uso au kiungo chochote cha mwili kwa ghafla tuu na bila maumivu yoyote

 ~kutokwa na madonda mdomoni kama vile mtu anayeumwa madonda koo lakini cha ajabu madonda yake yeye kila dawa akitumia hayaponi

~mwanamke kuwashwa kwenye matiti,pamoja na kutokwa madonda sehemu nyeti kule kwa bibi

~mwanamke kutokwa na maziwa kwenye matiti yake hali ya kuwa si mwenye kunyonyesha

~mwanaume kuvimba uume wake halafu unasinyaa na kuwa kama umerudi ndani

USHAURI ILI KUMUEPUKA JINI HUYU

 ~Usiwaruhusu watoto kucheza kwenye chemchem za vyanzo vya maji na kuyachezea maji hayo kwani jinni huyu anaweza muingia mwanao hapo na akakaa nae hadi utu uzima wake

~usiogelee baharini,mitoni,ziwani bila kuomba dua kwa mwenyez mungu akukinge na shari za viumbe waliopo humo

~usipige makelele wakati wa kuogelea labda kwa dharura

~usikae pembeni mwa bahari ukiwa uchi[wale watu wa beach nafikiri mnanipata vidhuuri]kwani jinni huyu akiona uchi wako huweza kupata mfadhaiko wa nafsi na akatamani kukuingia......[nao pia ni viumbe kama sisi]

TIBA

~Upate mafuta ya miski nyeupe au nyeusi

  mafuta hayo yasomewe hivii

mswalie mtume x7

alfatiha x7

Ayatur kursiyyu x7

Surat bakhara nzima

surat yusuph aya ya 23 na 24

Surat Nnuur aya ya 1 mpk 20

 kabla hajatumia mafuta haya..............

~Siku ya ijumaa chukua maji ya mvua yaliyoshuka moja kwa moja kwenye chombo
yasomee surat Arrahmaan anywe na aoge siku hyo kisha anaweza akaanza kutumia mafuta hayo kama ifuatavyo

~ajipake kifuani,na kwenye sehemu zote za vitundu mwilini mwako kama vile juu ya midomo,pua,juu ya kifuniko cha macho,kitovuni na kwenye matiti

~azifukize nguo za kulalia kwa miski,na asilale mgonjwa huyo ila alale akiwa amevaa nguo zilizopakwa mafuta hayo

~na akioga ahakikishe mafuta yake ya kujipaka yamechanganywa na mafuta ya miski na afanye hivyo muda wote wa kutumia dawa ambao usipungue siku 21 au zaid

inshaa ALLAH mafuta ya miski huweza kuwa sababu ya kukuondokea matatzo yako ya siku nyingi.