Tibazetu Afrika

Blog hii inahusu tiba za asili juu ya magonjwa mbalimbali ya kimwili na kiroho.Habari,burudani na mambo yote yanayoizunguka jamii.

Contact us

+255 657 739713
Whatsapp/call and sms

Email
Tibazetutz@gmail.com

Watembeleaji

Search

Jumatano, 28 Oktoba 2015

FAIDA MBALIMBALI ZA MATUNDA NA VYAKULA

FAIDA ZA KITUNGUU MAJI

 Baadhi ya faida za kitunguu maji ni

~kinaondoa ukali wa joto la mchana mwilini

~kinaongeza hamu ya mapenzi[nyege]

~kinatia nguvu tumbo

~ kinaongeza mbegu za kiume[manii]

~kinakata ukakasi wa mdomo 

~maji yake yakidondoshewa kwenye sikio matone matatu kutwa mara 2 huondosha uzito wa kusikia na kikipikwa kwa wingi kwenye chakula kinasaidia kuweka sawa mfumo wa mkojo kwa wale wanaopata tabu ya kupata choo hiki kidogo. 

 FAIDA ZA KITUNGUU THAUMU

Kitunguu thaumu kina faida nyingi sana katika tiba kwani katika tafiti mbalimbali vitunguu swaumu vimeonekana kuwa na uwezo wa kutibu maambukizi ya bakteria, fangasi na virusi vya aina mbalimbali. Aidha husaidia kuzuia magonjwa ya moyo ikiwemo kuondoa lijamu katika mishipa ya damu na hivyo kusaidia katika kurekebisha shinikizo la damu. Faida nyingine za vitunguu swaumu ni pamoja na

  • Kutibu saratani ikiwemo saratani ya tumbo na utumbo mkubwa. Tafiti zinaonesha idadi ndogo ya wagonjwa wa saratani katika nchi ambazo wakazi wake wana utamaduni wa kutumia vitunguu swaumu kwa wingi
  •  Vitunguu swaumu husaidia kudhibiti kiwango cha sukari katika damu. Hata hivyo inashauriwa kwamba wagonjwa wa kisukari wanaotumia sindano za insulin wasitumie kitunguu thaumu kwa wingi mpaka watakaposhauriwa na daktari   
  • Huzuia kusanyiko la chembe sahani zinazosaidia kuganda kwa damu (platelet aggregation)
  •  Husaidia ufyozwaji wa thiamin, hivyo kusaidia kuepusha mwili na ugonjwa wa beriberi  
  •  Ina kiasi kikubwa cha vitamini C ambayo husaidia kuzuia ugonjwa wa kiseyeye  
  • Hutumika kutibu magonjwa nyemelezi kama toxoplasmosis, hasa kwa watu wenye upungufu wa kinga mwilini. 
pia kitunguu thaumu huweza kutibu kifua,magonjwa ya moyo,pumu,magonjwa ya kuhara tumia kwa kutafuna punje 3asubuhi kabla ya kula na 3 usiku wakati wa kulala

FAIDA ZA NGANO

 Ngano pia ina uwezo mkubwa wa kutibu maradhi ya tumbo,homa kali,magonjwa ya figo,pumu na maumivu ya mwili na viungo,ugonjwa wa sukari nguvu za kike na kiume na hata tatizo la kukosa usingizi


yaponde majani ya ngano,yachemshe na uyachuje vizuri na anywe mgonjwa wa maradhi ya hapo juu,glass1 moja mara 3 kwa siku 21

 FAIDA ZA NYANYA
 Nyanya zinafaida kubwa mwilini,ukimenya nyanya unaondoa virutubisho vyote kwenye nyanya kwani virutubisho vya kwenye nyanya viko kwenye maganda yake.

Nyanya inaupatia mwili wetu faida zifuatazo.
• Vitamin C, A na K
• Pottasium
• Manganese
• Ufumwele
• Cromium
• Vitamini B1 na B6
• Chuma
• Kopa
• Vitamin B2 na B3
• Magnesium
• Folate, Phosphorous
• Protini ingawa kwa kiasi kidogo.
• Tryptohan, Folate na Molybdenum.

Lakini pia kikubwa zaidi nyanya ina lycopen ambayo husaidia kuponyesha ugonjwa wa tezi dume.ambao ni tatizo kubwa kwa wanaume wengi bila kujijua

pia nyanya hutibu ugonjwa wa kutapika na pia hupunguza mafuta mwilini

kata nyanya zilizoiva vizuri na ule pamoja na chakula,pia waweza kutumia juice ya nyanya
iliyokamuliwa ndimu kwani hii ni nzuri sana kwa kupunguza mafuta mwilini


 FAIDA YA TANGAWIZI
Ni dawa ya kikohozi, inasaidia kuondoa baridi mwilini, inasaidia kuondoa gesi ndani ya tumbo, inatibu mtu mwenye matatizo ya tumbo hasa likiwa linasokota, ukitumia tangawizi iliyopikwa kwa sukari, kuchanganywa na maji ya moto kisha mwenye tatizo akinywa glasi 3 za maji hayo kwa siku inasaidia kuchangamsha mzunguko wa damu mwilini.
Mbali na hayo tangawizi husaidia kuondosha ute wa mdomo.
 
Kuvumbiwa na kukosa hamu ya chakula
changanya vipimo vilivyo sawasawa vya juisi ya tangawizi na sukari mawe. Koroga vizuri, kunywa kabla ya kula.

Changanya juisi ya tangawizi, juisi ya limao na chumvi mawe kwa vipimo vilivyo sawa. Hakikisha umechanganya vizuri. Kunywa dawa hii kabla ya kula.
 Dawa hii husafisha ulimi na koo na hukuongeza hamu ya kula na kukufanya mchangamfu.

MAUMIVU YA KOO NA KUKAUKA SAUTI
Tafuna vipande vidogo vya tangawizi.

KWA KUHARISHA
Chua sehemu zinazozunguka kitovu kwa juisi ya tangawizi.

KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA
Kunywa mchanganyiko wa juisi ya tangawizi na juisi ya kitunguu.

BARIDI YABISI SUGU
Changanya kijiko kimoja cha tangawizi ya unga na vijiko 24 vya maji ya kunywa, mchanganyiko huu ukiwa wa vuguvugu. Ulale na ujifukize mpaka utoe jasho.

MAUMIVU YA JINO NA KICHWA
Chukua tangawizi ya unga koroga na maji kidogo iwe nzito kama tope. Jipake na uchue kwenye paji la uso kabla ya kulala. Kwa jino lipake na uchue kwenye shavu.Tangawizi si tu hutibu magonjwa mbalimbali bali pia ni kiburudisho. Mathalani 


unapokuwa na mafua makali na kikohozi, osha kisha twanga tangawizi na uichemshe katika maji kwa muda mrefu.
Unaweza kuweka majani ya chai au maziwa na kisha kunywa taratibu ikiwa ya moto. Fanya hivyo kwa siku mbili, mafua na homa hushuka.

Faida nyingine ni kurekebisha siku za hedhi kwa akina mama.

FAIDA ZA TANGO 
Watalamu wetu wanatueleza kuwa tango lina kirutubisho kinachojulikana kama ‘erepsin’ ambacho husaidia uzalishaji wa ‘amino acids’ ambayo ni muhimu kwa uzalishaji wa protini mwilini.
Vile vile tango lina kiwango kikubwa cha vitamin C hivyo kuwa na uwezo mkubwa wa kuondoa matatizo yatokanayo na ukosefu wa vitamin hiyo, kama vile fizi kuvuja damu, upunguvu wa damu kwa watoto wachanga na kuota meno na mifupa vibaya.

Kinga ya Saratani
Pengine faida kubwa kuliko zote unazoweza kuzipata kwa kula tango au juisi yake mara kwa mara ni kinga dhidi ya saratani za aina mbalimbali. Jambo hili linalotokana na ukweli kuwa tango lina kiwango kikubwa cha uchachu ‘alkaline’, na kufanya seli za saratani kuwa katika mazingira magumu ya kusambaa mwilini, kwani kwa kawaida seli za saratani haziwezi kuishi kwenye mazingira zenye uchachu. Hivyo ni vyema kujijengea mazoea ya kula tango mara kawa mara ili kujiwekea ulinzi na kinga ya saratani za aina mbalimbali.

Dawa ya magonjwa ya ngozi
Tangu enzi na enzi tango limekuwa likitumika katika masuala ya urembo wa ngozi. Watu wengi hutumia tango kwa njia mbalimbali kutunza ngozi zao na kupendezesha sura, hata baadhi ya vipodozi visivyo na madhara hutengenezwa kutokana na tango.


Pia tango linamsaidia mtu mwenye maradhi ya bandama,ini na figo kwa kula tango moja asubuhi,moja mchana na moja jioni

                       FAIDA ZA PAPAI


 HUIMARISHA MFUMO USAGAJI CHAKULA
Papai pia limeonesha kuwa na uwezo mkubwa sana wa kutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa saratani ya utumbo ambayo hutokana na mtu kuwa na matatizo katika mfumo wake wa usagaji chakula. Papai huboresha mfumo mzima wa usagaji chakula na kumfanya mtu kupata choo laini na hivyo kujiepusha na madhara ya kukosa choo kwa muda mrefu ambayo humuweka mtu katika hatari ya kupatwa na kansa ya tumbo.

KINGA DHIDI YA UVIMBE NA VIDONDA
Watu wanaosumbuliwa na majipu au kutokewa na mauvimbe ya ajabu ajabu na kupatwa vidonda mara kwa mara, inatokana na kutokuwa na virutubisho muhimu ambavyo hupatikana kwenye tunda hili. Imegundulika kuwa, watu wenye matatizo hayo wanapotumia papai au virutubisho vyake, hupata nafuu haraka na kupona.

KINGA YA MWILI
Vitamin C na Vitamin A ambayo inapatikana mwilini kutokana na kirutubisho kilichomo kwenye papai, ni muhuimu sana kwa kuimarisha mfumo wa kinga ya mwili dhidi ya magonjwa yanayojirudia mara kwa mara kama vile mafua, maambukizi ya sikio, kikohoo, n.k

NURU Y
A MACHO
Kama karoti inavyoaminika katika kuimarisha nuru ya macho, papai nalo ni miongoni mwa tunda hilo. Imeelezwa kuwa watu wanaotumia tunda hili hujipa kinga madhubuti ya macho na pia kudhibiti kasi ya kuzeeka ambayo hutokana na kuongezeka kwa umri wa mtu.



TIBA YA MAPAFU
Kama wewe ni mvutaji sigara mzuri au mtu ambaye katika mazingira yako unayoishi unakumbana na moshi wa sigara, basi utumiaji wa vyakula vyenye kiwango kikubwa cha vitamin A kama papai, kutakuepusha na kupatwa na madhara yatokanayo na moshi wa sigara.

SARATANI YA KIBOFU
Ulaji wa papai na chai ya kijani (green tea) kutakuepusha na hatari ya kupatwa na ugonjwa wa saratani ya kibofu cha mkojo Utafiti wa hivi karibuni uliochapishwa na Asia Pacific Journal of Clinical Nutrition umeeleza. Kwa faida hizi na nyingine, tupende kula tunda hili ili tujiepushe na magonjwa hatari yanayosumbua watu kila siku
.