Mwenyez mungu alipoiumba mbingu na ardhi na kila kitu kiumbe wa mwisho kuumbwa alikuwa ni bin adam,hii ina maana kwamba majini waliumbwa na walikuwa wanaishi duniani hata kabla ya kuumbwa kwetu sisi binadam na kuishi kwenye ardhi hii
Wakati majini hao wanaishi duniani mwenyez mungu aliwapa sheria ya kuwa wasivuke mipaka na kumuasi yeye mola wao aliyewaumba na wamtii kwa kila atakalowaamrisha.
Lakini majini wakaanza kumuhasi mungu na kufanya ufisadi ardhini na hapo sasa ndipo aliyewaumba akalituma jeshi la malaika kuja kuwafukuza majini hao na kuwapokonya mamlaka yote waliyonayo ardhini,na ndiyo maana majini wengi wakawa ni wenye kukimbia ovyo na wengine wakakimbilia milimani,mapangoni,baharini,mitoni,kwenye mapori makubwa,na katika hali hiyo wakawa ni wenye kufanya makazi yao kwenye maeneo kama hayo
Hapo sasa mwenyez mungu akakusudia kumuumba binaadamu na kumleta duniani awe ndiye khalifa na ndiyo maana tunayaona maneno hayo kwenye kitabu kitukufu mwenyez mungu anaposema ''INNII JAAILUN FIL ARDHW KHALIIFA
Khalifa maana yake ni mtu ambaye anakuja baada ya fulani kutoka au kutolewa na hapa baada ya kufukuzwa majini ndiyo mwenyez mungu amemleta binadamu kuja kuitawala dunia na kuwa kiongozi baada ya majini kutolewa
Majini hawa ambao walifanikiwa kukimbilia sehemu tofauti hapo ndipo walipoanza kujenga chuki na kiumbe huyu binadamu baada ya kuona kuwa nafasi yao waliyokuwa nayo wamepokonywa na amekabidhiwa binadamu ndipo ulipozuka uadui mkubwa baina ya viumbe hivi viwili.
fuatilia sehemu ya 2