Sababu nyingi sana zinaweza kuchangia kulegea kwa misuli ya uke ikiwemo ujauzito, umri mkubwa, kuzaa watoto, upasuaji na kuwa na uzito mkubwa.
Mazoezi ya kegel husaidia sana katika kukaza misuli inayoshikilia viungo vya chini ya tumbo ikiwemo mfuko wa uzazi, kibofu cha mkojo, utumbo na uke..
Wanawake wengi ambao wana misuli iliyolegea hawafiki kileleni kirahisi wakati wa tendo la ndoa na wakati mwingine huhitaji uume mnene ili kusugua mishipa yao ya fahamu ya uke kirahisi na kufika kileleni kuliko wanaofanya mazoezi haya.
Lakini pia mzazoezi haya husaidia kuzuia mkojo kutoka wakati wa kucheka, kushindwa kuzuia mkojo ukikubana na kushindwa kuzuia choo kubwa ikikubana..
Elimu ya afya ya nchi ambazo hazijaendelea kama Tanzania hujali zaidi kutibu na kuzuia magonjwa ila sio matatizo kama haya..
Hivyo kama mwanamke una tatizo hili au mwenzako ana tatizo hili ungana nami kwenye mada hii ili uijue njia hii nzuri na nyepesi itakayokusaidia kuufanya uke wako kuwa mdogo na kubana
JINSI YA KUFANYA ….
Tafuta msuli sahihi…
Kuufahamu msuli wa kuufanyia mazoezi nenda chooni kukojoa alafu katikati ya kukojoa zuia mkojo. Ukifanikiwa kuuzuia mkojo basi huo ndio msuli sahihi..
FANYA MAZOEZI SASA
Baada ya hapo malizia mkojo wako kisha nenda kitandani..lala kwa mgongo kaza msuli uleule uliokaza wakati wa kuzuia mkojo. Kaza msuli kwa sekunde kumi kisha legeza kwa sekunde kumi.
Fanya mara tatu kwa siku..
Kaza na kuachia msuli huo mara kumi asubuhi, vivo hivyo mchana na jioni.. lakini pia unaweza kukaza msuli huo popote ulipo ata kama hakuna sehemu ya kulala kwa mgongo. Kwenye foleni ya benki, kwenye gari, ukiwa ofisini kwani hakuna mtu atakayegundua unafanya nini..